Leo ni siku ya kipekee sana kwa watu wa kenya , afrika mashariki na afrika kwa ujumla pale Rais wa (MAREKANI) ambalo ni Taifa kubwa duniani katika nyanja zote za maisha atakapo tembelea nchi ya K
enya kwa mara ya kwanza akiwa kama Rais wa USA.
Karibu tuungane katika kupeana updates za kitachojiri katika ujio huo ikizingatiwa
Tanzania tuliisha wahi onja utamu na adha za ujio wa huyu mtu mkubwa na hata George W. Bush pia. Ziara yake ni kuanzia leo Ijumaa mpaka Jpili atapoondoka.
Shirika linalosimamia safari za ndege nchini Kenya, KCAA, limetangaza kuwa anga ya Kenya itafungwa kwa muda wa dakika hamsini siku ya Ijumaa wiki hii ili kuruhusu ndege ya rais wa Marekani Barrack Obama kutua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi.
Kwa mujibu wa shirika hilo, agizo hilo litatekelezwa katika viwanja vyote vya ndege nchini Kenya na kuwa anga hiyo itafunguliwa muda tu pale ndege hiyo ya rais Obama itakapokuwa imetua.
Shirika hilo limesema kuwa limeyaandikia mashirika yote ya ndege na pia kampuni zote za usafiri kuhusiana na agizo hilo na kuwa safari za ndege kadhaa zitacheleweshwa siku hiyo na pia siku ya jumapili wakati rais Obama atakapokuwa akiondoka nchini Kenya kuelekea Ethiopia kwa muda wa dakika arubaini.
Awali idara ya polisi nchini Kenya ilikuwa imetangaza kuwa anga yote ya Kenya itafungwa kwa muda wa siku tatu kabla ya ziara hiyo lakini kwa mujibu wa shirika la KCAA ndege zote zinazopaa chini ya futi elfu ishirini hazitaruhusiwa kutua katika uwanja wa Jomo Kenyatta na uwanja wa wilson mjini Nairobi kuanzia siku ya Ijumaa hadi siku ya jumatatu, wakati wa kongamano la kimataifa ya ujasiriamali litakalofanyika mjini Nairobi.
Agizo hilo sasa linamaanisha ndege zote ndogo ndogo ambazo uhudumu kati ya Nairobi na Somalia na viwanja vingine vidogo vidogo katika kanda ya Afrika Mashariki, havitaruhusiwa kutua Nairobi hadi mkutano huo utakapomalizika.
Rais wa Marekani Barrack Obama anatarajiwa mjini Nairobi siku ya Ijumaa usiku ambapo anatarajiwa kuwa mwenyeji wa kongamano hilo la kibiashara kwa pamoja na mwenyeji wake rais uhuru Kenyatta.
KWA MARA YA KWANZA
Obama amepanga pia kutembelea Makao Makuu ya Umoja wa Afrika yaliyo Addis Ababa, Ethiopia ikiwa ni ziara ya kwanza kwa Rais wa Marekani kuzuru umoja huo tangu kuasisiwa kwake
VIKOSI VYA ULINZI
Habari kutoka nchini humo zilidadavua kwamba, vikosi vya ulinzi vya Marekani, CIA, FBI na kile cha siri cha Secret Service vilitua nchini humo miezi kadhaa na kuungana na majeshi ya Kenya ili kuweka mambo safi.
MANOWARI ZA KIVITA Ilielezwa kwamba, meli na manowari za kivita vimepiga kambi eneo lote la pwani ya nchi hiyo katika Bahari ya Hindi, lengo likiwa ni kuimarisha usalama wa kiongozi huyo mkubwa duniani pamoja na jopo la wafanyabiashara atakaoandamana nao.
B52 YAEGESHWA PWANI
Ilielezwa kwamba, jeshi la kwenye maji la Marekani limejikita Bahari ya Hindi kwenye ukanda wote wa Afrika Mashariki kujiandaa kuzuia shambulizi la kivita wakiwa na silaha nzito ndani ya ndege ya B52 ambayo imeegeshwa pwani ya nchi hiyo.
KAMERA, SATELAITI ZAFUNGWA
Ilisemekana kwamba, Jeshi la Kenya wameweka doria kwenye Jiji la Nairobi ambalo limetulia tuli huku likimulikwa kwa kamera maalum na satelaiti za kijeshi, barabara kufanyiwa usafi na nyingine kufungwa huku bendera za Kenya na Marekani zikiwa zimepamba Jiji la Nairobi.
AIR FORCE ONE
Imedadavuliwa kwamba, Obama atatua na ndege ya Rais wa Marekani ya Air Force One aina ya Boeing 747-200B kisha atapokelewa na gari analotumia Marekani ambalo lilitangulia kuwasili Kenya.
UWANJA WA NDEGE
Ilielezwa kwamba, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta atakaotua Obama, kumejaa ndege za Jeshi la Marekani na hauruhusiwi kutumiwa na ndege nyingine za biashara.
Hali ndivyo ilivyo kwa viwanja vingine pamoja na bandari, hakuna biashara inayoendelea hadi kiongozi huyo amalize ziara yake nchini humo.
MAMLAKA YA ANGA
Ilielezwa kwamba, Mamlaka ya Anga ya Marekani na Makao Makuu ya Jeshi hilo Pentagon wanafanya kazi kama siafu kuhakikisha anga lote lipo shwari.
Kuna taarifa kwamba, wafanyakazi wote serikalini wasiohusika na usalama na ziara hiyo watakuwa miguu juu pindi atakapowasili Obama kwani hawataenda kazini.
Kuhusiana na ulinzi wa Kenya, hata nchi za Tanzania, Somalia, Eritrea, Uganda, Rwanda na Burundi nazo zinamulikwa kusije kukatokea lolote.Hapa bibi yake Obama aitwaye Sarah Hussein Obama akifurahi ujio wa mjukuu wake.
More images, see post #2 on this thread
=======================
Updates: Rais Obama anategemewa kutua Nchini Kenya, katikati ya saa mbili leo usiku hadi saa tano.
Kwa sababu za kiusalama muda rasmi atakaowasili hauwekwi wazi.
Uhuru Kenyatta
UKenyatta
Welcome to Kenya
POTUS
5:31 p.m. - 24 July 2015
Update: Muda mchache uliopita, Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na msafara wake wametoka Ikulu kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) kumpokea Rais Barack Obama kutoka Marekani.

Endelea kufuatilia...
Update (19:42 PM): Rais Obama kuwasili saa 2 na dakika 10 usiku.
New: OBAMA AWASILI NYUMBANI: Naam, na sasa ndege ya Airforce One iliyomsafirisha Rais Obama imeshawasili katika uwanja wa ndege wa JKIA muda huu wa saa 2 na dakika 03 usiku.
Ulinzi katika Uwanja wa Ndege umezidi kuimarishwa wakiwemo mbwa wa kunusa na vikosi maalumu vya jeshi (Special Force Units) wakiwa wamejiandaa kwa lolote.
=========
Update: SAA 2 na DK 13 USIKU HUU

OBAMA USO KWA USO NA UHURU KENYATTA: Wakati uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu sasa umewadia. Rais Obama ameshatua na kushuka kutoka kwenye ndege na kupokelewa na wenyeji wake wakiongozwa na Rais wa KENYA, Uhuru Kenyatta.
Kinachoendelea sasa ni salamu za hapa na pale baina ya Rais Obama na Mabalozi, Waziri wa ulinzi wa ndani wa Kenya, na viongozi wengine wa juu wa serikali ya Kenya, pamoja na upigwaji wa picha mbalimbali kutoka kwa vyombo vya habari vilivyotanda eneo la Uwanja wa Ndege wa JKIA.
Visitor's book: Na sasa Rais Obama anatia saini kwenye kitabu cha wageni ikiwa ni Kumbkumbu ya ujio wake kama mgeni rasmi na wa kipekee.
Sura za bashasha zimefurika hapa!
THE BEAST: Rais Obama anaelekea kwenye gari yake ghali na ya kipekee zaidi duniani iliyopachikwa jina la The Beast yenye kila kitu ndani ikiwemo ofisi ndogo na mawasiliano.
KIVUTIO: Dada wa Obama anayeishi Kenya amepata bahati ya kipekee ya kupanda kwenye gari moja na Rais Obama (The Beast) na msafara unaelekea kwanza hotelini (haijatajwa ni hoteli gani) ambako atafikia kabla ya kuelekea IKULU hapo kesho.
Ratiba ya kesho ni Obama kuhutubia viongozi maalumu watakaoalikwa kwenye tukio hilo kwenye makazi ya Rais Kenyatta (Ikulu) asubuhi ambako pia atafungua Kongamano la kimataifa la Wajasiriamali mjini Nairobi.
Update: 09: 00 a.m
Ndege na helkopta za jeshi la marekani zimeanza kuzunguka katika anga la Nairobi kuhakikisha kuwa
kila kitu kuhusu usalama kina enda shwari kabisa.
Update: 09:45 a.m
Waandishi wa habari wanaanza kukaguliwa wao na vifaa vyao vya kazi kabla ya kuingia kwenye vyumba vya mkutano wa wajasiliamali na Rais wa Marekani.
Update:saa 10:15 mkutano umeanza Rasmi.
Mkutano wa wajasiriamali umeanza katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini Nairobi huku Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta akihutubia mkutano.
Rais Kenyata aelezea namna kenya ilivyokumbana na majanga mbali mbali ikiwemo yale ya kushambuliwa kigaidi na Al-shabab
lakini ilipambana nayo na hatimaye kuyashinda na kusonga mbele.
Asisitiza juu ya umuhimu wa nchi za Kafrika kujiirmarisha kiuchumi kwani haziwezi kuendelea kwa kuzitegemea nchi za barani ulaya .
Pia asema kuna wanawake wajasilia mali zaidi ya 1,600 barani Afrika amabo wakikuzwa vema watakuja kuwa wafanyabiashara wakubwa sana hapo baadae.
Pia USA imetoa dola milioni 100 kwaajili ya kuwawezesha wajasiliamali wanawake. Na pi kwa kipindi cha miaka 3 ijayo marfekani itatoa dola bilioni 1 kuwawezesha wanawake wajasilia mali wa Afrika.
Update :10:50 Obama aisifia kenya kwenye teknologia.
Asema nchi ya kenya imepiga hatua kubwa kiteknologia ikilinganishwa na miaka kumi aliyopita pindi alipokuja .
Asifia tena ukuaji wa teknologia ya mawasiliano na matumizi ya Mpesa.
Asema watafungua vituo na mifuko ya kudhamini biashara mbali mbali zitazoanzishwa na wanawake kwani kina mama ndio iniji ya maendeleo. Vituo hivyo vitafunguliwa katika nchi za Kenya ,Mali na Zambia.
Update :Obama atembelea kituo cha mradi wa Power Africa Innovation
Obama ametembelea mradi huo wa kuzalisha umeme kwa kutumia nguvu ya jua huko Nairobi. Ambapo alikutana na mkurugenzi wa huduma kwa wateja M-kopa bibi June Muli, amabo mradi wao unakwenda kwa falsafa ya "pay-as-you-go" wenye lengo la kusaidia kutoa nguvu ya umeme kwa makazi hasa ya watu wa kipato cha chini.
Update :11:02 a.m Obama na Kenyata wanaelekea Memorial Park .
Obama na Uhuru sasa waelekea katika eneo la shambulizi la kigaidi la mwaka 1998 jijini Nairobiambapo watu zaidi ya 200 waliuwawa, wakiwemo wamerekani 12 na wafanyakazi wasio wamarekani 34. Tukio hilo lilitekelezwa na kikundi cha kigaidi cha Al-qaida .
Update :Makama wa rais Ruto akutana na ujumbe wa Rais Obama.
Dakika chache zilizopita Mmakamu wa Rais wa marekani MH. Wiliam Rutto amewasili kunako viunga vya ikulu ya Kenya kwaajili ya kufanya mazungumzo (bilateral talks ) na viongozi waandamizi wa marekani ambao wameandamana na Obama katika safari yake .
amesisitiza wakenya kutumia fursa hii adhimu na adimu kupenyeza biashara zao Marekani na kwingineko duniani kwa maendeleo yao na ya kenya kwa ujumla.
Update za Bilateral Talks.
Mazungumzo yanaendelea katika Ikulu ya kenya huko Nairobi kati ya Rais Kenyata na Rais Obama
Tunategemea matunda mauzri yatapatikana baada ya haya mazungumzo kwani palipo na "wakubwa"
tunatarajia mambo kwenda bara bara.....