Obama: Tanzania ni mfano wa kuigwa

Obama: Tanzania ni mfano wa kuigwa

Masatu

JF-Expert Member
Joined
Jan 29, 2007
Posts
3,276
Reaction score
131
Kwa wale wasio ona kazi na mafanikio ya serikali yetu walau wakubwa huko wanayaona.

Kweli wahenga walisema mitume haikubaliki makwao...

Tupate habari zaidi;

RAIS wa Marekani, Barack Obama, ameisifu Tanzania kuwa ni mfano wa kuigwa katika Bara la Afrika kwa kuwa na uongozi unaojali na kusaidia maendeleo ya watu wake. Obama amesema uongozi wa Tanzania umeonesha mfano kwa nia ya dhati ya kuwasaidia wananchi kwa kuboresha huduma muhimu za kijamii.

Rais huyo ambaye kesho anaanza ziara yake ya kwanza Afrika tangu kuchaguliwa kwake kuwa Rais akianzia Ghana, alisema jana kuwa kila atakakopita ataziambia nchi hizo za Afrika ziige mfano wa Tanzania. Katika mahojiano aliyofanya na waandishi wa tovuti ya All Africa, alisema nchi hiyo haitasita kuziunga mkono nchi zinazoonesha nia thabiti ya kuwainua watu wake.

Obama ambaye aliulizwa kama kuna nchi muhimu ambazo anazipa kipaumbele katika safari zake za kutembelea Afrika, alisema nchi zote ni muhimu lakini ujumbe atakaopeleka kwa kila nchi ni kuiga mfano wa Tanzania. "Msisahau, kwamba pamoja na kwamba ninatembelea Ghana, Waziri Mkuu wa Zimbabwe, Morgan Tsvangirai na Rais Jakaya Kikwete wameshatembelea Ikulu ya Marekani.

"Bila shaka mmeona kazi nzuri iliyofanywa na uongozi wa Tanzania ya kuelekeza nguvu zake katika kutoa huduma kwa wananchi wake, na popote marafiki wanapotaka kujikwamua wenyewe, tutakuwa nyuma yao kama washirika," alisema Obama.

Alisema anaamini Afrika ina uongozi mzuri ambao unataka kwenda mbele na Marekani inataka kwenda pamoja na Bara la Afrika katika juhudi zake za kujikwamua. Rais huyo alisema ushirika anaohitaji na Afrika si tu wa kutoa misaada bali wa kufungua fursa bora zaidi za kiuchumi kati ya Marekani na Bara hilo. "Hii ina maana ni pamoja na kuimarisha uwezo wa ndani ya nchi wa kujiendeleza na kuimarisha uhusiano baina ya Marekani na nchi moja moja," alisema Obama.

Kwa wale wenye wivu.... just do it!

suicide.jpg
 
Last edited:
na video ya kuthibitisha hilo hii hapa:

PART 1
[ame="http://www.youtube.com/watch?v=gfKq89flacE&feature=player_embedded"]YouTube - Obama Talks to AllAfrica at the White House - Part 1[/ame]

PART 2
[ame=http://www.youtube.com/watch?v=pp9MoDLYE08&feature=player_embedded]YouTube - Obama Talks to AllAfrica at the White House - Part 2[/ame]
 
Ni Huduma gani za jamii ambazo ni mfano wa kuigwa? Elimu hamna kitu, Afya ndo usiseme, Mawasiliano mabovu, maji vijijini, yaani unajua hawa wakubwa wanapelekewa maendeleo kwenye karatasi lakini ki uhalisia hali ni mbaya. Ngoja hao jamaa waje kujifunza watapigwa changa lamcho tu. Unacheza na wabongo...................
 
Aje Tz ajione, VIONGOZI WETU WAKIENDA ULAYA WANADANGANYA Tu, Nenda north Mara, nenda singida hakuna maji, nenda DSM hakuna maji, Hospitali zenyewe hazina vifaa vya kisasa watu wakubwa wanaenda kutibiwa nje why?? Jicho tu LOWASA LIMEMPELEKA MAREKANI. Nchi kubwa hizi zinaisifia hii nchi sana kwa sababu wanapata dhahabu, Tanzanite na almasi. Mfano bush alikuja alipelekwa Manzese anapelekwa pazuri tu kama ARUSHA, Wangempeleka KIGOMA, Kigoma wana miaka nenda rudi hakuna UMEME barabara hazipitiki. Ni noma wala OBAMA AKAE KIMYA NA MATATIZO YETU. Kikubwa TZ HATUUAN NDO WANACHOSFIA. Be a think Tank
 
ama kweli kitanda usokilalia huwajui kunguni wake!
angejua huo moto unaofukuta chini chini sasa tanzania asingesema hayo ......
 
Ukiona Marekani wanakusifia ujue kuna jambo nyuma yake! Mifano iko mingi tu, yetu macho.
 
kejeli tupu!
nakumbaka mzee wa kaya alipokwenda marekani na wakati anongea na huyu obama

alikuwa ameshikiria makaratasi mengi sana amimsomea obama,obama bila kujua kuwa anadanganywa nae ameanza kupotosha nchi zingine!!

hii ndio tanzania zaidi ya uijuavyo
 
Ukiona Marekani wanakusifia ujue kuna jambo nyuma yake! Mifano iko mingi tu, yetu macho.

Hehehe itakuwa Kigamboni bila shaka mambo ya Africom.
Angekuja ajionee waTZ tunavyo teseka tunasoma kwenye shule za nyasi chini/sakafu vumbi shule ina walimu 3 nyumba za walimu za nyasi njoo Obama ujionee sio unaletewa makaratasi na bla bla kibao unawaamini hakuna kitu bora ungeisifia Rwanda na sio Tanzania.
 
Ukiona Marekani wanakusifia ujue kuna jambo nyuma yake! Mifano iko mingi tu, yetu macho.

Wewe umesema kweli hata Congo former Zaire waliisifu sana zile enzi za Mabutu Seseseko lakini kilichotokea baada ya hapo sote tunajua,wameendelea kupigana na kuuana mpaka sasa amani haijapatikana. Mungu tu ajuae kuwa Tanzania tunaelekea wapi.

Obama hana makosa anatumia information aliyopewa na JK wakati walipokutana katika Oval Office.JK kamuingiza kamanda mjini.
 
Kwa nini asiseme nchi yake ya kuzaliwa ya Kenya ambayo iko juu kiuchumi na kihuduma kuliko sisi?
Wale kwanza shule ni bure kabisa sisi tunalipa.
Hospitali ndio usiseme hadi viongozi wetu wengine wanakimbizwa huko.
Lakini mimi sishangai maana hawa wamarekani wanasifia mahali wanapodhani watapata maslahi. Si ajabu kapewa ahadi ya mgodi hapo.
Masatu umesikia?
Sisi si wamarekani wala hatusubiri wamarekani kuja kuwa kipimo cha maendeleo mfu yetu. Sisi waliwanchi ndio hasa kipimo chenyewe. Tunapima wenyewe Sisi hasa tunaoishi danganyika hii na si watanzania mlioamua kuishi ulaya au kuila nchi. Pole kama mnadhani Obama atakuwa mpima mafanikio yetu.

International diplomacy is full of hypocrisies and half truths disguised as the genuine article, Obama is so far removed he would'nt know the real problems if he was front row center in the drama.

This just goes to show you that the west does not apply it's own standards when it comes to Africa.
 
kejeli tupu!
nakumbaka mzee wa kaya alipokwenda marekani na wakati anongea na huyu obama

alikuwa ameshikiria makaratasi mengi sana amimsomea obama,obama bila kujua kuwa anadanganywa nae ameanza kupotosha nchi zingine!!

hii ndio tanzania zaidi ya uijuavyo

Pamoja na 'makaratasi' ya JK, zipo ripoti zinatoka Ubalozi wa Marekani nchini mwetu kuhusu Tanzania. Kwa jicho la 'jumla' Tanzania ni nchi ya Amani na Tulivu na yenye kutafuta maendeleo ya wananchi wake tangu nchi ilipopata Uhuru. Hilo peke yake linaweza kupelekea Rais yeyote anayelinganisha Tanzania na nchi zingine za Bara letu kuweza kusifia na kusema ni mfano wa kuingwa. Ukiweka kando uozo unaojitokeza hapa na pale bado nchi yetu ni mfano mzuri barani Africa. Obama hajakosea!
 
Takwimu za kwenye makaratasi..... Hali halisi ni mbaya ni mfano wa kuigwa kwa kuboronga mambo . Amani iliyopo ni woga wa kutetea haki zetu.
 
Kuna watu hapa hawataki kusikia jambo lolote zuri kuhusu Tanzania. Ndio tuna matatizo lakini huenda tu nafuu kuliko wenzetu wa nchi zingine za Afrika ambao wana hali kama ya kwetu.

Je hayo maneno yatufanye tukae na kushangilia? Hapana, ni changamoto kwamba tukiamua tunaweza kufanya yaliyo bora. Tanzania bado tuko nyuma na wananchi wetu wengi bado wanaishi kwa shida kubwa. Ila pia sio kweli kwamba serikali ya JK haijafanya chochote.

Tumuunge mkono JK badala ya kila siku kulalamika tu. Sisi wenyewe ndio tunaongoza kufisadi nchi badala ya kutumia muda wetu na resources zetu kujenga nchi yetu.
 
Pamoja na 'makaratasi' ya JK, zipo ripoti zinatoka Ubalozi wa Marekani nchini mwetu kuhusu Tanzania. Kwa jicho la 'jumla' Tanzania ni nchi ya Amani na Tulivu na yenye kutafuta maendeleo ya wananchi wake tangu nchi ilipopata Uhuru. Hilo peke yake linaweza kupelekea Rais yeyote anayelinganisha Tanzania na nchi zingine za Bara letu kuweza kusifia na kusema ni mfano wa kuingwa. Ukiweka kando uozo unaojitokeza hapa na pale bado nchi yetu ni mfano mzuri barani Africa. Obama hajakosea!

Kweli Bora Maisha, ndiyo sababu umeridhika haraka kwa vile Obama kasema.

Toka lini amegundua kuwa TZ ni mfano, kama ni hivyo tusingekuwa hapa tulipo, unless ni mfano wa kula pesa za umma.

Nimeanza kuamini kuwa USA kweli wana interest na TZ siyo bure. Kama JK ameshindwa kumalizia barabara zilizoachwa na Mkapa ambazo yeye mwenyewe aliahidi zitaisha by 2006 sasa hii ya sisi kuwa mfano sijui inatoka wapi.

Uzuri Wadanganyika tunaridhika haraka sana na ndiyo sababu hatutakuja endelea kwa kizazi hiki. Wenzetu wanasong mbele sisi tunaridhishwa na stories za Obama. Mwambieni aje ajionee mwenyewe ndiyo asema. Naona amekuwa miss informed!!!
 
Kwanza Sifa ya Jk itakwisha mwakani maana siku zote CCM wataweza kweli kuacha demokrasia ya kweli itachukua mkondo wake katika uchaguzi Zanzibar, Sisi mwenyewe tunajua matatizo yaani yeye Obama anapelekea taarifa za miradi na USAID lazima wafanye hivyo maana wao ndio wanatoa pesa. Ukweli TZ hakuna kitu kabisa, Chaguzi Ndogo Wizi Mtupu, UFisadi ndio usisime kabisa
 
Kwa nini asiseme nchi yake ya kuzaliwa ya Kenya ambayo iko juu kiuchumi na kihuduma kuliko sisi?
Wale kwanza shule ni bure kabisa sisi tunalipa.
Hospitali ndio usiseme hadi viongozi wetu wengine wanakimbizwa huko.
Lakini mimi sishangai maana hawa wamarekani wanasifia mahali wanapodhani watapata maslahi. Si ajabu kapewa ahadi ya mgodi hapo.
Masatu umesikia?
Sisi si wamarekani wala hatusubiri wamarekani kuja kuwa kipimo cha maendeleo mfu yetu. Sisi waliwanchi ndio hasa kipimo chenyewe. Tunapima wenyewe Sisi hasa tunaoishi danganyika hii na si watanzania mlioamua kuishi ulaya au kuila nchi. Pole kama mnadhani Obama atakuwa mpima mafanikio yetu.

Hujaelewa! soma kasome tena bandiko, kwa kifupi issue sio "utajiri" kama ni utajiri angezungumzia SA, Botswana, Nigeria etc.Kibaya zaidi issue pia sio yeye kazaliwa wapi!

Yaani huwezi kuchangia bila kuonyesha rangi yako.You are prejudicative really you are!
 
"alisema jana kuwa kila atakakopita ataziambia nchi hizo za Afrika ziige mfano wa Tanzania."
Kama habari hii ni ya kweli kabisa na si kwamba anatupiga changa la macho, naanza kudoubt credibility ya Obama. Hivi kweli Marekani inaye balozi hapa nchini, ina mashushushu kibao na vifaa vya kuangalia matukio yote duniani Rais wake anaweza asiwe makini kiasi hiki?
Eti nchi zingine ziige mfano wa TZ ; kwa yafatayo!:
-Viongozi walio madarakani kutokubali kushindwa? (angalia uchaguzi wa Biharamulo, Zanzibar) nk.
-Kuacha sumu ikawaua wananchi wake kwa kuthamini mno wawekezaji?(Angalia North Mara -au naye ana hisa humo?)
-Kufisadi hela za wananchi na kuwaacha mafukara wa kutisha?
Kufisadi hela za wafadhili? (angalia zile za maliasili)
-Kubwa zaidi ni kuitumbukiza nchi katika vita na migogoro ya kidini. Ebu asubiri islamic courts kama za Somalia zianzishwe Tz ndipo atajua kuwa kauli yake ilikuwa ya kipuuzi.

Nawasihi viongozi makini wa Africa, msiige Tanzania. Hata hiyo inayoitwa amani haipo bali ni ujinga tu. Msiige TZ kwa kuwafanya wananchi wenu wajinga na makondoo kama TZ.
 
Kuna yule balozi wa marekani yule mchungaji alikuwa hapa nchini baada ya mabomu alikuwa africa ya kusini akihojiwa na SABC alikuwa anaiisifu kweli Tanzania anasema atazunguka dunia nzima kuitangaza anasema ni nchi ya mfano hajapata kuona Africa .
nadhani ni kutokana na mchango wa nchi kwa nchi zingine za magomvi ikiwemo Kenya
Halafu hakujawa na mgogoro mkubwa na ukitokea tunatatua wenyewe kama ilivyokuwa kwa Zanzibar
Sasa inabidi JK awaambie CCM waache wizi wa kura na kusimamia demokrasia kama mwenyekiti wa chama vinginevyo sifa anazozipata zitatyeyuka akiachia mambo ya busanda na biharamuro kuendelea hawatamfumbia macho siku zote
lakini na uranium ya huko kusini na mchuchuma inageuza viswahili vya akina obama
 
Kuna watu hapa hawataki kusikia jambo lolote zuri kuhusu Tanzania. Ndio tuna matatizo lakini huenda tu nafuu kuliko wenzetu wa nchi zingine za Afrika ambao wana hali kama ya kwetu.

Je hayo maneno yatufanye tukae na kushangilia? Hapana, ni changamoto kwamba tukiamua tunaweza kufanya yaliyo bora. Tanzania bado tuko nyuma na wananchi wetu wengi bado wanaishi kwa shida kubwa. Ila pia sio kweli kwamba serikali ya JK haijafanya chochote.

Tumuunge mkono JK badala ya kila siku kulalamika tu. Sisi wenyewe ndio tunaongoza kufisadi nchi badala ya kutumia muda wetu na resources zetu kujenga nchi yetu.

Mkuu
Tatizo la sisi ni wivu hilo ni tatizo kuu,watanzania wachache sana wenye tabia ya kusifia mema na kukandya mabaya ,Ni wivu tuu unasubuwa watu wala sio upinzani.
 
Back
Top Bottom