Mbona aliwahi kutembela nchi hiyo zaidi a mara moja, safari ya kwanza alikwenda huko peke yake akiwa kijana, safari nyingine aliongozana na mchumba wake M. Lobinson. Mimi sioni kuna ulazima gani eti atembelee Kenya kwa kuwa kuna ndugu na makaburi ya ancestors wake, mbona hamsemi kwa nini asianzei safari yake kwa kutembelea kisiwa cha Ireland kwa kuwa mama yake mzazi, mababu na nyanya zake wana asili ya HUKO na bado kuna ndugu zake huko.
Now on a serious NOTE - Hivi unafikili OBAMA anaweza kuchangamkia mtoto wa Kenyatta kuwa RAIS wa Kenya, wakati akijua wazi wazi kwamba Kenyatta Senior ndiye alihusika moja kwa moja katika masahibu aliyo kumbana nayo Baba yake OBAMA alipo rudi kutoka masomoni Merikani na kufanya kazi kidogo katika Serikali ya Kenyatta Sr, baba yake OBAMA ambaye alikuwa ni Mchumi alikuja kutofautiana kidogo kwenye misimamo na Kenyatta hasa baada ya kuuwawa Tom Mboya, tofauti zao hizo zilikuwa ni mbaya sana OBAMA Sr alinusurika kifo zaidi ya mara moja na Kenyatta alihapa kwamba atahakikisha OBAMA Senior hapati kazi na atatembea mpaka kiatu kihishe sole - na kweli OBAMA Sr alipata wakati mgumu kimaisha!!! Ukatili wa kiwango gani huo, labda mtoto mwenye akili zenye uwalakini ndiye anaweza kumchangamkia Kenyatta Jr na 2 add salt 2 an injury Rais mwenyewe hata upigaji kura na matokeo yake yako highly questionable, Uhuru na wapambe wake wanaendeleza ubabe wa baba yake (Kenyatta) wa kujaribu ku-contain makabila fulani ili yasipewe Uongozi nchini Kenya hata kama wameshinda kwenye kura - binadamu gani mwenye akili timamu anayeweza ku-entertain genge lililo kaa kimafia mafia!!
Juzi juzi hapa niliona Balozi na Kenya na Rwanda UN wanataka kujaribu ku-derail mashtaka ya Rais na makamu wake, mama wa Kinigeria akawatolea nje na kuwapa vidonge vyao - baadae Uhuru kaongezewa shitaka lingine la kuwapatia wafuasi wake bunduki za G3 na AK-47 na visu ili wawadhulu wafuasi wa wapinzani wake - sioni hata kama kuna kitu amejifunza kwamba ICC wana uwezo wa kufungua a pandola box mpaka mwenyewe akasalimu amri na hawako peke yao alipo tembelea Uingereza Administraion ya Cameroon ali-act au ku-react kivipi ujio wake huko - siona kama anasoma harama za nyakati.
Nataka nieleweke kwamba binafsi sina tatizo na Uhuru au RUTTO kama binadamu lakini wakumbuke matendo yao ndio Dunia haipendi, wasifikili akili kuchaguliwa kwao kuwa Rais/Makamu basi hilo tu linaweza kuwafutia mashitaka ya ukatili against humanity i.e International community hifumbe macho kwa kuwa Uhuru sasa ni Rais! Kwa maoni yangu sababu nilizo taja kwenye paragraph ya pili mpaka ya mwisho ndizo zilizo mfanya Rais OBAMA hasiweze kuwa na hamu ya kutembelea Serikali ya design za Uhuru na Rutto, hata Uhuru na RUTTO hilo wanalijua sana; ndio maana wamekaa kimya - uchakachua wa kura utawafikisha mahali pabaya sana kadiri muda unavyo kwenda, waswahili usema akufukuzaye akwambii nenda, matendo yake tu yanakuwa message SENT and delivered.