Nikatize huu mjadala niseme tu jambo muhimu sana....jamii ya kimataifa wanafanya
mambo haya ya kutumia uhasama wa zamani kwa kugonganisha baadhi ya viongozi
barani kwa busara sana na kwa manufaa yao wenyewe japokuwa kiuchumi na kihali
waafrika tunazidi kuzorota...tunajua pia wakenya walipoteza maisha yao kabla mkoloni
kuondoka madarakani... (kwenye mkoa wa kati, bonde la ufa na sehemu za magharibi
ya kenya, na pwani)...cha kustaajabisha ni mambo haya yanatekelezwa na
muingereza na marekani.
Hivi OBAMA yuko ziarani, lakini ni wachache sana katika mataifa anayoyazuru
wanatambua umuhimu wa safari yake kwao. Tena usisahau shughuli za mchina
zinamnyima mmarekani usingizi na itachukua mmarekani kila awezalo kukatiza
mchina analotekeleza barani EAC...mzungu kwa kawaida hapendi mwafrika
kupata maendeleo kwenye viwanja mbalimbali....
....miundo mbinu, upanuzi wa viwanda nk..kwa sababu angependa awe muuzaji
wa rasilimali tu.
Safari za rais wa marekani...mbona tusijiulize kwa nini haipatani na pingamizi
kama afrika ambapo vyombo vya dola vinapeperusha pingamizi. Ziara yake ina uhusiano sana na
STRATEGIC INTERESTS ZA MAREKANI AFRIKA MASHARIKI inayofichwa
ndani ya matamshi kama 'bilateral trade patnerships'.. Kwa kifupi mambo haya yana uhusiano....
Mahali ambapo rais wa marekani OBAMA kuzaliwa kwake na kulelewa kwake ina mvuta
nikuvute. Wengi husema ni indonesia au hawaii...na kule hakukutana wala kuelewa
misingi ya kikabila ya kenya...Hata lugha yenyewe ya asili yake haielewi. kwa mkenya wa
kawaida ziara ya OBAMA haina mashiko kwao ...Inasemekana Afisi ya wizara Obama Snr
alipokuwa akifanya kazi ilipata ugumu kutoka kwa utawala wa kenyatta Snr, na pia
inasemekana Obama Snr alikuwa na matatizo ya kibinafsi mojawapo kulewa chakari..
ambayo yalimwandama mpaka alipoelekea kupata afueni kule marekani..Je OBAMA jnr
anatambua haya yote. Yazidi kutuonyesha kuna uhusiano kati ya familia ambazo zina
historia ya kushika madarakani na kungangania madaraka kati ya baadhi ya hizo familia...
...na tena migogoro ya kihistoria yamedhihirisha wazi haishirikishi baadhi ya wananchi
wakenya wa kawaida licha yao kuwa ndio wanaoathiriwa pakubwa inapotekelezwa na
wanasiasa.....msukumo wa wabunge kenya kudai nyongesa zaidi inaturudisha nyuma kama taifa..
wakoloni walilazimisha haki miliki zote za rasilimali mikononi mwao kupitia mauaji
ya jinai, vitendo vya ughaidi, ukiukaji wa haki za binadamu...cha kusikitisha ni
tayari miaka hamsini baadaye mambo haya yanasahaulika huku waafrika
wakiendelea kuuana ka misingi ya siasa. Itakuaje leo hii watumie ICC na
UN kufikia malengo yao kutunyanganya rasilimali. Ni nani anayewakubalia
hawa na faida gani wanapata???...wananchi wana njia ya kufaidika kutokana
na hizi rasilimali au zinasaidia nani???...haya ndio maswali ya kuulizwa...
utapata mjinga akiniuliza maswali haya yameulizwa miongo kadha bila
majibu.... bila kujua uchumi wa dunia unaporomoshwa na mataifa
kama marekani....Badala ya kujificha chini ya bango la taifa eti kenya Tz
au Ug tutafute rukhusa kuthibitisha kwa nini sasa africa tunazidi pitia janga
kubwa uongozini......na EAC na mataifa yana taaluma.
lazima tujiulize mkoloni alitaka kuCONTAIN waafrika kwenye kambi za wakimbizi
kwa malengo gani??...enzi hizo walikufa hawakuwa watu...?? au kuna jamaa
amelipwa mahali kusahau au kutupa ushahidi??... Tusisahau mambo haya hivi karibuni..