Observation: Nyerere, Mkapa na Magufuli (RIP) wana mfanano wa ajabu

Observation: Nyerere, Mkapa na Magufuli (RIP) wana mfanano wa ajabu

Wote wamelaaniwa kwa kumwaga damu za watanzania. Ndio maana wote wameshakufa wakati wenzao wa dini ile nyingine wako hai na uzee wao.
 
Vipi Kuhusu Nadharia kwamba,Wakitangulizana kutokana na tofauti za kimtazamo katika masula fulani?Wa mwisho kazidiwa kete baada ya kujarbu tena kumtanguliza mwingine.Kuna ukweli katika hilo?
Wa mwisho alitaka kumtanguliza nani? Msoga company?
 
Hivi Nyerere na Mkapa ni wasomi kuliko Kikwete na Suluhu?
Hivi usomi ni nini, kuwa na vyeti?

Nionyeshe maandishi yoyote ya hao wawili wa mwisho, nami ntakuonyesha ya wawili wa mwanzo.

Hapana. Hata kama huna maandishi ya kuonyesha, taja fikra na mawazo waliyoyasimamia hao wawili wa mwisho, nami nitakuonyesha za wawili wa mwanzo.
 
Magufuli hakuwa msomi.

Wasomi wanaandika.

Nyerere kaandika vitabu kuhusu Ujamaa. Mkapa kaandika kitabu kuhusu maisha yake.

Magufuli kaandika nini?
 
Wote walitangaza vifo vya viongozi wakuu nchini.
1. Nyerere alitangaza kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu hayati Sokoine
2. Mkapa alitangaza kifo cha Nyerere
3. Magufuli alitangaza kifo cha Mkapa

Nadhani ni mgongano tu maana hata ambao hawakutangaza wenzao watakufa tu. Kwahiyo tusiwe na hofu kwa Samia kumtangaza Magufuli
 
Wallichangia pakubwa kuliko waliobakia
Walisomea shule za misheni
wawili walikuwa na vipara na walivaa miwani
Wawili walitoka kanda ya ziwa
Wote walitoka mpakani
Wote walikuwa wasafi kwa kiwango kikubwa
Wote walikuwa wanajiamini na kuamini katika kile walichokiamini
Wote walikuwa na mke mmoja mmoja
Wajane zao wote wapo
Wote hawakuacha watoto wao serikalini wala kwenye siasa
Wote walikufa ghafla
 
Back
Top Bottom