DOKEZO OCS kituo cha Polisi Igogo Mwanza jitathimini wewe na askari wako

DOKEZO OCS kituo cha Polisi Igogo Mwanza jitathimini wewe na askari wako

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

The Certified

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2016
Posts
910
Reaction score
774
Ndugu wanajamvi Habari za muda huu,

Nilifungua kesi polisi Igogo Mwanza na hii ni wiki ya tatu mtuhumiwa wangu hajakamatwa, mtuhumiwa amezidi kunitesa na kuniwinda njiani usiku ninapotoka kazini.

Mtuhumiwa alinitishia kunidhuru ila RB Inasoma Kutoa Lugha chafu, Hii Imekaaje? Na kwanini hakamatwi? Naibu Waziri Wa Mambo Ya Ndani Waziri Bashungwa, Jeshi La Polisi Mbona Kila siku linapoteza Dira na kuaminiwa na wananchi?

Najua upo Mwanza na nimeomba nikuone ila nikaambiwa uko busy Sana, najua upo JF, nimeshalalamika karibu ngazi mbalimbali na still hakuna ushirikiano wowote ule napata.

Sasa nikichukua sheria mkononi nikamdhuru huyu muharifu na mimi mtachelewa kunikamata?

Naomba haki yangu itendeke mapema kabla sijachukua sheria mkononi.

Nawasilisha Wana Jamvi.
 
Yamenikuta kama hayo dakika km 40 zilizopita....nimeenda kuripoti kituon kushambuliwa.Mtuhumiwa kanimwagia maji machafu na kunitolea matusi makali.Nilichoambulia ni kwamba ilo sio swala la kuripoti usiku,niende ata kesho....nikafikiria ningechukua sheria mkononi ingekuwaje?maana mtuhumiwa ningeamua kumshugulikia,dkk 3 zilikuwa nyngi ila nilihofia kujaza watu.

Halafu nikusahahishe,waziri wa mambo ya ndani sio Bashungwa bali ni Masauni.
 
Daaaah Pole Mkuu, Asante kwa kunisahihisha
 
Binafsi navyoelewa kukamata mtu lazima ushirikiane na mapoti hao, kufungua RB pekee haitoshi, polisi hafanyi kazi ya kumuwinda mtu mtaani. Ni jukumu lako kumtrack huyo mtu wako na kuwatonya mapoti mahali alipo. Hawana kazi Moja tu kumtafuta mtu wako. Nb usisahau ya brush
 
Hivi Bashungwa ni waziri wa mambo ya ndani

Ova
 
Labda jwtz kidogo Wana weledi, Lakini hao sidhani kama Wana msaada wowote kwako directly, labda mpaka mtu aumizwe vibaya sana ndio wa take action, usisahau kutoa ya brush.
 
Police ni kazi ya watu hafifu kiutu na kifikra, ladha yao ya maisha ni rushwa. Kazi ya hovyo na Ina watu wa hovyo maadili sifuri. Wanaishi maisha ya dhuluma na kikekike tu wanapata pesa mithili ya Kodi za meza za wake za watu.
 
Mtu akutishie au akupige ukimbie kushitak
Na wewe pigana
Mambo yatajulikana mbele ya safari
 
Back
Top Bottom