OCTOBER: Mwezi wa malkia wa rozari takatifu

OCTOBER: Mwezi wa malkia wa rozari takatifu

temoin

JF-Expert Member
Joined
Apr 25, 2025
Posts
311
Reaction score
708
Tumsifu yesu kristu.

Tupo ndani ya octoba (mwezi wa kumi), ni mwezi ambao kanisa katoliki liliuchagua kuwa mwezi maalumu wa rozari takatifu kwa ajili ya kumuenzi mama bikira aliye mama wa mkombozi na mwombezi wetu.

Ingawa rozari husaliwa na wakristo kila siku ila kanisa liliona ni vyema kukawa na mwezi maalumu wa kanisa kwa ajili ya rozari takatifu.

Rozari ya bikira Maria ambayo ilipata sura hatua kwa hatua katika karne ya pili chini ya maongozi ya roho wa Mungu, ni sala iliyopendwa na watakatifu wasio na idadi na kuhamasishwa na mafundisho ya kanisa.

Ni sala rahisi lakini yenye kina , na inabakia hata mwanzoni mwa milenia hii ya tatu kuwa sala ya maana kubwa iliyokusudiwa kuzaa matunda ya utakatifu . Inaoana vizuri na safari ya kiroho ya maisha ya kikristu ambayo baada ya miaka 2000 hayajapoteza hata chembe ya upya wake wa asili.

"Ee Rozari yenye baraka ya Maria, mnyororo mtamu unaotuunganisha na Mungu, kifungo cha upendo kinachotuunganisha na malaika, mnara wa wokovu dhidi ya mashambulizi ya motoni, bandari ya salama katika uangamizi wa chombo chetu cha ulimwengu huu hatutakaa tukuache . Utakuwa kitulizo chetu katika saa ya kufa: kutupatia busu lako la mwisho maisha yatakapotoweka .Na neno la mwisho kutoka midomoni mwetu litakuwa jina lako tamu , Ee mama wa mama wa takatifu, Ee mama mpenzi ,Ee kimbilio la wakosefu ,Ee kitulizo kikuu cha wenye kuteswa. Uheshimiwe pote leo na siku zote duniani na mbinguni ewe bikira Maria mtukufu na mwenye baraka , Amina"

Bikira Maria malkia wa rozari takatifu utuombee
 
Back
Top Bottom