Odinga ataka uchaguzi mwingine tena Agosti mwaka huu

Odinga ataka uchaguzi mwingine tena Agosti mwaka huu

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Kiongozi wa upinzani nchini Kenya kupitia NASA, Raila Amollo Odinga, ametaka kufanyika kwa uchaguzi mkuu mpya tena mwezi Agosti mwaka huu 2018.

Akizungumza na BBC Raila Odinga amesema hamtambui Uhuru Kenyatta kama Rais wa nchi hiyo kwani hana kibali cha watu, ingawa hana lengo lolote la kupambana na serikali ya Kenyatta.


"Hatutamtoa Uhuru Kenyatta Ikulu anaweza kuendelea kukaa kwa amani, lakini hatuutambui Urais wake kwa sababu uko kinyume, tunataka uchaguzi mwingine na kwa mujibu wa ratiba yetu utakuwa Agosti mwaka huu”, amesema Raila Odinga.


Hivi karibuni kiongozi huyo wa upinzani nchini Kenya alijiapisha na kuwa Rais wa watu, akisema yeye ndio chaguo la watu kuwaongoza na sio Uhuru Kenyatta.


Chanzo: EATV

raila-odinga.jpg.size-custom-crop.1086x0.jpg
 
Hehehehe!! Mzee Odinga..baaabaa mbona unatuyumbisha hivi, juzi umekula kiapo na kuwa rais wa nchi na kusema umetufikisha Kanani, sasa mbona hujiamini unatetereka na kujitwika majukumu ya tume ya uchaguzi ya kutangaza lini tufanye uchaguzi. Wanaokufuata kwa kweli wana shughuli sio haba.

Tatizo serikali nayo inamfuata huyu mzee, imepanic na kuanza kamata kamata zisizoeleweka, yaani hii nchi inazidi kuwa tamu, full vituko.
 
Ukicheza na jinga litakutoboa jicho na kukuacha kilema!
Watch out!
Majanga haya
 
That photo tells you the story of desperation in some quotas to present Odinga as more popular
 

Anapo fanya mkutano Uhuru Park, Kibera hubaki bila watu. Waliojaza huo uwanja ni wajaluo wote wa Kibera.
About 100,000 of them.
Alafu propaganda uwache. Kama una haja ya kucompare apples with apples, tafuta picha za inauguration ya Uhuru. Wachana na picha za kitambo.
 
Anapo fanya mkutano Uhuru Park, Kibera hubaki bila watu. Waliojaza huo uwanja ni wajaluo wote wa Kibera.
About 100,000 of them.
Alafu propaganda uwache. Kama una haja ya kucompare apples with apples, tafuta picha za inauguration ya Uhuru. Wachana na picha za kitambo.
Propaganda my foot
Hiyo si mliposti wenyewe
Dadeki!
 
Back
Top Bottom