Ofa ya kiwanja kwa atakayenisaidia kujiunga na Polisi

X_INTELLIGENCE

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2014
Posts
10,400
Reaction score
14,339
kwa mara nyingine nakuja kwenu ndugu zangu, ndugu yenu nimehangaika sana kutafuta nafasi kwenye majeshi yetu bila mafanikio, kiukweli nina nia ya dhati kabisa ya kulitumikia taifa letu, nimehangaika kutafuta nafasi jkt miaka 8 mfululizo bila mafanikio, nimehangaika kutafuta nafasi za polisi zaidi ya miaka 12 sijawahi kufanikiwa.

najua humu ndani kuna watu wa aina tofautu tofauti, lengo langu ni kujiunga na jeshi la polisi hivyo kama kuna mtu humu ndani anao uwezo wa kunisaidia nikasajiliwa ndani ya jeshi la polisi...nitampa zawadi ya kiwanja, kiwanja hicho ni mari yangu kabisa, ni kikubwa 70*35....ni matumaini yanu maombi yanu yatamfikia mlengwa.

18808792_114180709171063_3620998549715550208_n.jpg
 
Samahani mkuu, umesoma vigezo hata vitatu tu vya kujiunga na hilo jeshi?

12+8=20
Tuseme kuzaliwa mpaka kusoma kwako ulitumia miaka6.
20+6=26 umri huu tayari disqualified

Tuzungumzie huo uwanja sasa
Upo eneo gani.

Kila la kheri ktk maombi yako, lakini tahadhari tu nakupa, watu wanautamani huo uwanja kuliko hiyo kazi uipendayo. Ogopa matapeli km vipi mtafute Kamanda Sirro direct hukosi shavu. Una magamba yoyote ya ujuzi?
 
Alafu Ukishaipata, hasira zako za kuhonga kazi kwa kutoa kiwanja uje uwatolee bodaboda, wapinzani na wauza mkaa.

Omba kazi nyingine hii ya upolisi nakuombea ukose kabisa! Tena ukiendelea kubembeleza hii kazi nakuombea upate laana ya maisha yako yote.

Tena shindwa katika jina la Yesu Kristo
 
Samahani mkuu, umesoma vigezo hata vitatu tu vya kujiunga na hilo jeshi?

12+8=20
Tuseme kuzaliwa mpaka kusoma kwako ulitumia miaka6.
20+6=26 umri huu tayari disqualified

Tuzungumzie huo uwanja sasa
Upo eneo gani.
Inawezekana alikuwa anatafuta JKT na Unjagu kwa pamoja mkuu ila alianza kutafuta Unjagu alafu baada ya miaka 4 akaanza kutafuta na U-jkt so kwa miaka 8 ya mwisho ya utafutaji wake alikuwa anapiga parallel ..........

Turudi kwenye uwanja sasa, nakubaliana na hoja yako, atuambie huu uwanja uko wapi! Kama upo kawe beach karibu na Kikwete au Masaki itarahisisha sana watu kujitoa kumsaidia
 
Alafu Ukishaipata, hasira zako za kuhonga kazi kwa kutoa kiwanja uje uwatolee bodaboda, wapinzani na wauza mkaa.

Omba kazi nyingine hii ya upolisi nakuombea ukose kabisa! Tena ukiendelea kubembeleza hii kazi nakuombea upate laana ya maisha yako yote.

Tena shindwa katika jina la Yesu Kristo
Babu, tusameheane tusiombeane mabaya wala kutakiana laana.
Kila mtu ana ndoto ya kupata kile anachokipenda.
Ingawa unaweza kupenda kitu kumbe kina shari ndani yake na ukakichukia kitu kumbe kina heri ndani yake.
Si police wote wabaya na si madaktari wote ni wema.
 
Safi sana.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Babu, tusameheane tusiombeane mabaya wala kutakiana laana.
Kila mtu ana ndoto ya kupata kile anachokipenda.
Ingawa unaweza kupenda kitu kumbe kina shari ndani yake na ukakichukia kitu kumbe kina heri ndani yake.
Si police wote wabaya na si madaktari wote ni wema.
Hicho kiwanja unachotaka kuhonga utakirudisha kwa miaka mingapi kwa kutegemea mshahara wa polisi? Hautegemei kuumiza wengine ili ufanikiwe haraka?

Uza hicho kiwanja ufanye uwekezaji wowote huku ukitafuta kazi nyingine ila sio upolisi. Tutakuombea mabaya mpaka ukome na hilo pepo lako la upolisi
 
kwani mshahara wa polisi shingapi jaman!!!

maana story zimekuwa nyingi sana.
 
Hicho kiwanja unachotaka kuhonga utakirudisha kwa miaka mingapi kwa kutegemea mshahara wa polisi? Hautegemei kuumiza wengine ili ufanikiwe haraka?

Uza hicho kiwanja ufanye uwekezaji wowote huku ukitafuta kazi nyingine ila sio upolisi. Tutakuombea mabaya mpaka ukome na hilo pepo lako la upolisi
Mungu anapokea maombi yote ya waja wake lakini jukumu la kuchuja mashudu na mchele si jukumu la muombaji ila la muombwa hivyo yeye ndiye anaamua amkubalie mchawi akutese au neema na maombi ya waja wema vikumulikie.

All in all si mimi niliyeweka hilo bango lakini bado sijaona nafasi ya yeye kulaumiwa na kupewa maneno mabaya
 
Huyo anayeomba kazi ya upolisi bora aendelee kusota kitaa dawa imuingie kisawasawa
 
Umetafuta zaidi ya miaka kumi na mbili.18 +12=30 kule ni miaka 26 kwenda chini muraaaa kachonge cheti cha kuzariwaa kwanza.

Ukianza kuomba na ukiwa na umri wa miaka 18 ndani ya miaka 12 inamaana una 30 sasa hivi
Polisi mwisho miaka 26 kama hujafika degree, kama una degree na masters ni 28

USHAURI: Uza kiwanja fungua kampuni ya ulinzi chukua wanamgambo waajiri. Wewe utakuwa mkurugenzi

MWISHO: unachokifanya ni RUSHWA mpaka hapo umejitoa ktk vigezo vya kuwa polisi
 
kwa mara nyingine nakuja kwenu ndugu zangu, ndugu yenu nimehangaika sana kutafuta nafasi kwenye majeshi yetu bila mafanikio, kiukweli nina nia ya dhati kabisa ya kulitumikia taifa letu, nimehangaika kutafuta nafasi jkt miaka 8 mfululizo bila mafanikio, nimehangaika kutafuta nafasi za polisi zaidi ya miaka 12 sijawahi kufanikiwa.

najua humu ndani kuna watu wa aina tofautu tofauti, lengo langu ni kujiunga na jeshi la polisi hivyo kama kuna mtu humu ndani anao uwezo wa kunisaidia nikasajiliwa ndani ya jeshi la polisi...nitampa zawadi ya kiwanja, kiwanja hicho ni mari yangu kabisa, ni kikubwa 70*35....ni matumaini yanu maombi yanu yatamfikia mlengwa...View attachment 1898297
Hapo mtaani kwenu kama Kuna mkubwa yoyote mtumie huyo kupata nafasi,utumishi wa umma wa nchi hii ni WA upendeleo na kujuana sana,Mimi nilikosa nafasi ya jeshi kutokana na upendeleo mwaka 2002,sasa kama Hari ilikuwa ngumu miaka 20 iliyopita,leo itakuwaje?
Tafuta watu,connections hao watakuweka sehemu nzuri
 
Back
Top Bottom