Ofa ya kiwanja kwa atakayenisaidia kujiunga na Polisi

Ofa ya kiwanja kwa atakayenisaidia kujiunga na Polisi

Hapo mtaani kwenu kama Kuna mkubwa yoyote mtumie huyo kupata nafasi,utumishi wa umma wa nchi hii ni WA upendeleo na kujuana sana,Mimi nilikosa nafasi ya jeshi kutokana na upendeleo mwaka 2002,sasa kama Hari ilikuwa ngumu miaka 20 iliyopita,leo itakuwaje?
Tafuta watu,connections hao watakuweka sehemu nzuri
kuna mmoja nachat nae kwa meseji ila haingiliki kaka...nimemwambia anisaidie ananiambia vigezo tu ndio vitakavyo nibeba..nielekeze jinsi ya kumpanga labda mimi nakosea...
 
Ukianza kuomba na ukiwa na umri wa miaka 18 ndani ya miaka 12 inamaana una 30 sasa hivi
Polisi mwisho miaka 26 kama hujafika degree, kama una degree na masters ni 28

USHAURI: Uza kiwanja fungua kampuni ya ulinzi chukua wanamgambo waajiri. Wewe utakuwa mkurugenzi

MWISHO: unachokifanya ni RUSHWA mpaka hapo umejitoa ktk vigezo vya kuwa polisi
asante kwa ushauri nitaufanyia kazi
 
Umetafuta zaidi ya miaka kumi na mbili.18 +12=30 kule ni miaka 26 kwenda chini muraaaa kachonge cheti cha kuzariwaa kwanza.
ivi sasa nina miaka 26...ila kwenye sekta hizo mchawi ni refa tu.....yupo mtu namjua aliingia akiwa na miaka 32....wala hakubadirisha cheti....tena aliingia na elimu ya darasa la saba...enzi za marehe Matanga...dah....mwenyezi Mungu amlaze mahala pema pepo...siajabu hivi sasa na mimi ningekuwa askari...Matanga Mbushi ninaamini umepewa ukilanja huko peponi ulikuwa na roho nzuri sana BABA
 
Kaka upolisi umeutafuta miaka nane??
ndio na mara zote nimekosa...last time nilipata namba za aliekuwa mkuu wa chuo cha polisi enzi hizo..marehemu Matanga Mbushi...akaniambia mwanangu jiandae mwakani utaaingia...huo mwakani ukawa mwaka wa shetani 2015...na yeye akahamishwa...miaka 2 baadae nikasikia amefariki....iliniuma ndoto zangu zikawa zimefifia...
 
Kiwanja kiko wapi?
Viwanja vyote ni vizuri ila si kila kiwanja ni kizuri kwa kila mtu.
Kuna viwanja hata bure huwezi chukua
kitunda...dar es salaam....picha unayo iona hapo juu ndio muonekano harisi wa hicho kiwanja
 
Kwani lazima uwe polisi? Fanya mambo mengine
 
Mimi Kuna muda nilishinda mashindano ya Isha ya Polisi jamii... Nikatumiwa barua kutoka was IGP kwamba nikihitaji kujiunga na Polisi nitapewa kipaumbele.

Nilitoboa kirahisi saana hamna interview Wala nini. Naonyesha barua tu naambiwa nyie tuna maelekezo yenu mtakuja siku ya kuondoka tu.

Miaka 19 Sasa nshakuwa OC FFU. [emoji41]
nipiganishie na mimi mkuu....nimezihangaikia sana hizo nafasi bila mafanikio
 
Hicho kiwanja unachotaka kuhonga utakirudisha kwa miaka mingapi kwa kutegemea mshahara wa polisi? Hautegemei kuumiza wengine ili ufanikiwe haraka?

Uza hicho kiwanja ufanye uwekezaji wowote huku ukitafuta kazi nyingine ila sio upolisi. Tutakuombea mabaya mpaka ukome na hilo pepo lako la upolisi
asante kwa ushauri wako...nitaufanyia kazi
 
kwa mara nyingine nakuja kwenu ndugu zangu, ndugu yenu nimehangaika sana kutafuta nafasi kwenye majeshi yetu bila mafanikio, kiukweli nina nia ya dhati kabisa ya kulitumikia taifa letu, nimehangaika kutafuta nafasi jkt miaka 8 mfululizo bila mafanikio, nimehangaika kutafuta nafasi za polisi zaidi ya miaka 12 sijawahi kufanikiwa.

najua humu ndani kuna watu wa aina tofautu tofauti, lengo langu ni kujiunga na jeshi la polisi hivyo kama kuna mtu humu ndani anao uwezo wa kunisaidia nikasajiliwa ndani ya jeshi la polisi...nitampa zawadi ya kiwanja, kiwanja hicho ni mari yangu kabisa, ni kikubwa 70*35....ni matumaini yanu maombi yanu yatamfikia mlengwa...View attachment 1898297
Kiko wapi? Kesho asubuhi ukaapishwe kuwa IGP?
 
Inawezekana alikuwa anatafuta JKT na Unjagu kwa pamoja mkuu ila alianza kutafuta Unjagu alafu baada ya miaka 4 akaanza kutafuta na U-jkt so kwa miaka 8 ya mwisho ya utafutaji wake alikuwa anapiga parallel ..........

Turudi kwenye uwanja sasa, nakubaliana na hoja yako, atuambie huu uwanja uko wapi! Kama upo kawe beach karibu na Kikwete au Masaki itarahisisha sana watu kujitoa kumsaidia
bora umenielewa ndugu yangu...nilianza kuzifuatilia hizo nafasi tokea nimemaliza darasa la 7....kwa kifupi kiwanja kipo dar es salaam huko kitunda
 
Back
Top Bottom