"Offside trap" mbinu inayotumiwa na Barcelona Fc kudhibiti wachezaji tishio duniani, mpaka sasa hakuna kocha mwenye mwarobaini wa kuizuia

Umechukua matukio machache, kuna baadhi ya matukio, kina mbappe na vinicius wenyewe walizinguwa.

Katika thread yako, picha ya pili nadhani inaonesha barca wameweka mtego wa offside vinicius kauvunja na valverde kaweka pasi moja mbele.
 
Ni vile tu hii mbinu Ancellot hakuifanyia assignment ila watu wakikaa wakaifanyia assignment hiyo mbinu hawezi fanya KAZI tena! For me it was a surprise to madrid
 
Hiyo trap haitofautiani sana na offside trick iliyokuwepo siku zote. Nadhani wameiboresha katika eneo moja. Kuwa na perfect timing ya kujua na kureact kabla tu ya mpira unapopigwa, tena ukichukulia siku hizi kuna faida ya V.A.R hautegemei tu macho ya mwamuzi.
 
Inachekesha sana🤣🤣
 
Ni vile tu hii mbinu Ancellot hakuifanyia assignment ila watu wakikaa wakaifanyia assignment hiyo mbinu hawezi fanya KAZI tena! For me it was a surprise to madrid
Hans Flick amekuwa akiitumia hii densive approach tangu Yuko FC Bayern na ndio aliyochukua nayo vikombe 6 ndani ya mwaka mmoja....

Na tangu amefika Barcelona imekuwa ndio mbinu yao kuu ya kiulinzi na imewasaidia sana mpaka hapa walipofika ni mara chache sana imewafelisha.

Yaani kabisa wewe unaamini eti Ancellot hakujua kwamba Barcelona wataingia na high line defensive approach kwenye game ya El classico??? alijua sana na aliifanyia kazi na ndio maana kipindi Cha kwanza Real Madrid waliwa outsmart sana mabeki wa Barcelona wakatengeneza nafasi nyingi sana za kufunga ila wakashindwa kuzitumia.

Kipindi cha pili Wachezaji wa Barcelona wakaja wameifanyia maboresho tayari hasa kwenye timing na wakafanikiwa, kwa upande mwingine niseme kipindi Cha pili mabeki wa Barcelona waliwa outsmart akina Mbappe.

High line defensive approach ni risk sana lakini mpaka ukutane na washambuliaji wanaotumia akili nyingi mno.
 
Hiyo mbinu kwa huko majuu sawa ila timu itakayoiga hiyo mbinu kwa hapa bongo imeisha na hawa marefa wetu mmmh
Hii Ina thrive kwenye mazingira yenye technology ya Hali ya juu na marefe wa kiwango Cha duniani ambao hawafanyi makosa ya kibinadamu kiholela holela.
 

sio rahisi kama unavyosema, ingekuwa vyepesi hivyo Real Madrid wangefanya hivyo ile juzi.
 
hii ipo kiufundi zaidi. hakika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…