Ofisa usalama 'feki' anaswa

Ofisa usalama 'feki' anaswa

Siku hizi kila mtu ni Usalama wa Taifa, hata mimi sasa ngoja nijitangaze rasmi, mimi ni Usalama wa Taifa. Mpo hapo, Kova njoo huku upesi unikamate.

Tiba
 
Nooma aisee weka ndani

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
kila mtu ni usalama wa taifa,usipolinda usalama wa taifa lako nani atalinda? Ndio maana kuna ulinzi shirikishi,sungusungu na polisi jamii wote hao ni kulinda usalama wa taifa.

kwaiyo mkuu unakubaliana na mimi huyu mh ni usalama wa taifa ?? Jamaa hakuonyesha hofu yoyote ,,kesho au keshokutwa tutakuwa nae mtaani akiendelea kula bata,,,atakayeweza kufuatilia hii kesi kwa ukaribu tunaomba atujuze kwakila atua tafadhali.
 
Mtuhumiwa anajiyefanya Afisa wa Usalama wa Taifa Alquine Michael Masubo (42) mkazi wa Yombo Buza, ambaye alikamatwa na bastola mbili BROWNING namba A. 956188-CZ83 ikiwa na risasi 12 na MAKNOV namba BA 4799 ikiwa na risasi 19 na kitabu mmiliki wa bastola chenye namba CAR 00071678 chenye jina la P.1827 LT COL Mohammedi H. Ambari

attachment.php
 

Attachments

  • a feki.jpg
    a feki.jpg
    17.9 KB · Views: 2,167
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemkamata Alquine Claud (42) mkazi wa Yombo Buza wilayani Temeke kwa tuhuma za kujifanya ofisa Usalama wa Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova alisema kuwa baada ya mtuhumiwa kuhojiwa alikiri kuwa hakuwa mfanyakazi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kova alisema kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alikamatwa na vielelezo mbalimbali ikiwemo bastola aina browning yenye namba A.956188-CZ83 ikiwa na risasi 12 ndani ya magazine.

Kwamba alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na bastola nyingine aina ya Maknov yenye namba BA4799 ikiwa na risasi 19 pamoja na kitabu cha mmiliki silaha hiyo chenye namba CAR 0007168 na jina la P.1827 LT COL Mohamedi Ambari, kitambulisho cha JWTZ No.7001-E. 1075.

Mbali na vielelezo hivyo, mtuhumiwa alikutwa na nyaraka mbalimbali zikiwemo za Ikulu pamoja na mihuri ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na vyeti bandia vya shule.

Tanzania Daima


inji hii bana.....tutafika tu
 
Ipo siku tutakuja kamata msaidizi wa "mkulu wa kaya feki", nyie subirini tu coz hizi product za UVCCM ni shida xana.
 
Daa jamaa kala shavu la ukweli.. Hiyo ni ajali tu kazini ..

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Hivi polisi wanaanzaje kumkamata myu eti kisa kajiita Usalama wa Taifa? Kwani Usalama wa Taifa huwa ni visible?

Utajuaje kwamba kajiita Usalama wa taifa na siyo au ndiyo?

Hizi sanaa tu, wanataka kutuambia kuwa wale Askari kuanzia tigo, Trafic, Askari wa kawaida etc wanaodaigi rushwa eti ni askari feki, kwamba ndo hawa wanaokamatwa sasa.
 
Mtuhumiwa anajiyefanya Afisa wa Usalama wa Taifa Alquine Michael Masubo (42) mkazi wa Yombo Buza, ambaye alikamatwa na bastola mbili BROWNING namba A. 956188-CZ83 ikiwa na risasi 12 na MAKNOV namba BA 4799 ikiwa na risasi 19 na kitabu mmiliki wa bastola chenye namba CAR 00071678 chenye jina la P.1827 LT COL Mohammedi H. Ambari

attachment.php

Huyo sio feki ndugu kwani kuna maafisa usalama hadi vichaa tunao mitaani hapo Kova amebugi meen ua kuna siri imejificha nyuma ya pazia. Isije ikawa ni mbinu ambapo huyu anaweza kutimika kuwadhuru mahabusu wa kisiasa hususani CDM watakapowekwa rumande na lengo lao la kuwauwa liwe limetimia kabla ya 2015
 
Back
Top Bottom