MJINI CHAI
JF-Expert Member
- Dec 12, 2010
- 2,202
- 1,228
Napita.........
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ishu ya ponda inapotezewa
kila mtu ni usalama wa taifa,usipolinda usalama wa taifa lako nani atalinda? Ndio maana kuna ulinzi shirikishi,sungusungu na polisi jamii wote hao ni kulinda usalama wa taifa.
Duu! hii nchi ni rahisi sana kuishi.
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemkamata Alquine Claud (42) mkazi wa Yombo Buza wilayani Temeke kwa tuhuma za kujifanya ofisa Usalama wa Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova alisema kuwa baada ya mtuhumiwa kuhojiwa alikiri kuwa hakuwa mfanyakazi wa Idara ya Usalama wa Taifa.
Kova alisema kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alikamatwa na vielelezo mbalimbali ikiwemo bastola aina browning yenye namba A.956188-CZ83 ikiwa na risasi 12 ndani ya magazine.
Kwamba alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na bastola nyingine aina ya Maknov yenye namba BA4799 ikiwa na risasi 19 pamoja na kitabu cha mmiliki silaha hiyo chenye namba CAR 0007168 na jina la P.1827 LT COL Mohamedi Ambari, kitambulisho cha JWTZ No.7001-E. 1075.
Mbali na vielelezo hivyo, mtuhumiwa alikutwa na nyaraka mbalimbali zikiwemo za Ikulu pamoja na mihuri ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na vyeti bandia vya shule.
Tanzania Daima
Mtuhumiwa anajiyefanya Afisa wa Usalama wa Taifa Alquine Michael Masubo (42) mkazi wa Yombo Buza, ambaye alikamatwa na bastola mbili BROWNING namba A. 956188-CZ83 ikiwa na risasi 12 na MAKNOV namba BA 4799 ikiwa na risasi 19 na kitabu mmiliki wa bastola chenye namba CAR 00071678 chenye jina la P.1827 LT COL Mohammedi H. Ambari
![]()