Ofisa usalama 'feki' anaswa

Ofisa usalama 'feki' anaswa

Kenyan

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2012
Posts
414
Reaction score
314
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemkamata Alquine Claud (42) mkazi wa Yombo Buza wilayani Temeke kwa tuhuma za kujifanya ofisa Usalama wa Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova alisema kuwa baada ya mtuhumiwa kuhojiwa alikiri kuwa hakuwa mfanyakazi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kova alisema kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alikamatwa na vielelezo mbalimbali ikiwemo bastola aina browning yenye namba A.956188-CZ83 ikiwa na risasi 12 ndani ya magazine.

Kwamba alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na bastola nyingine aina ya Maknov yenye namba BA4799 ikiwa na risasi 19 pamoja na kitabu cha mmiliki silaha hiyo chenye namba CAR 0007168 na jina la P.1827 LT COL Mohamedi Ambari, kitambulisho cha JWTZ No.7001-E. 1075.

Mbali na vielelezo hivyo, mtuhumiwa alikutwa na nyaraka mbalimbali zikiwemo za Ikulu pamoja na mihuri ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na vyeti bandia vya shule.

Tanzania Daima
 
Mbona hao ni wengi sana, tena mitaa ya Lumumba, kule chini Posta mpya/zamani wamejaa sana.

Zamani walikuwa na kijiwe chao pale mitaa ya Bills, ila siku hizi wanaopendelea kukaa mitaa ile ni TISS wenyewe.
 
Tumeshawazoe mbona akina yahaya ni wengi sana mnashituka leo!!

"Nchi ngumu hii"
 
ukiona hivyo wameshaona huko kwenye usalama wa taifa kuna maslahi zaidi na nirahisi kuingia bila kujulikana
 
Yule jamaa aliyeibiwa moro smg ambayo ni ya kivita mbona hawatuambii kilichojiri? huyo bastola 2 tu na mihuri
 
Hii ni tamthiliya ya kuchonga. Juzi juzi alishikwa yule traffic feki tabata na serikali ikaahidi kula nao sahani moja halafu ghafla wanakamatwa wengi kishenzi. Halafu inakuzwa kuwa bonge la news. Hakuna kitu hapa.
 
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limemkamata Alquine Claud (42) mkazi wa Yombo Buza wilayani Temeke kwa tuhuma za kujifanya ofisa Usalama wa Taifa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamanda wa Kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova alisema kuwa baada ya mtuhumiwa kuhojiwa alikiri kuwa hakuwa mfanyakazi wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Kova alisema kuwa siku ya tukio mtuhumiwa alikamatwa na vielelezo mbalimbali ikiwemo bastola aina browning yenye namba A.956188-CZ83 ikiwa na risasi 12 ndani ya magazine.

Kwamba alipopekuliwa nyumbani kwake alikutwa na bastola nyingine aina ya Maknov yenye namba BA4799 ikiwa na risasi 19 pamoja na kitabu cha mmiliki silaha hiyo chenye namba CAR 0007168 na jina la P.1827 LT COL Mohamedi Ambari, kitambulisho cha JWTZ No.7001-E. 1075.

Mbali na vielelezo hivyo, mtuhumiwa alikutwa na nyaraka mbalimbali zikiwemo za Ikulu pamoja na mihuri ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na vyeti bandia vya shule.

Tanzania Daima
huyu atakuwa usalama au wanataka kumrahisishia utendaji wake wa kazi,,ili watu wasijue ni usalama
 
mbona wako wengi hvo?? Watu wanajtambulisha baa wanaposhndwa kulipa na hata kwenye daladala akigombana na konda tu utamskia. Mi wala sshangai.
 
Kila mtu ni usalama wa taifa,usipolinda usalama wa taifa lako nani atalinda? Ndio maana kuna ulinzi shirikishi,sungusungu na polisi jamii wote hao ni kulinda usalama wa taifa.
 
Bongo Movies
Story by;S.Kova
Directed by;S.kova
Na mengine yote ni S.kova
Mpaka Driver,dressed by
Yaani mpaka Movie inakosa muelekeo
 
Bongo Movies
Story by;S.Kova
Directed by;S.kova
Na mengine yote ni S.kova
Mpaka Driver,dressed by
Yaani mpaka Movie inakosa muelekeo

Dressed by Kova???? Hahahahahaha!!!! Inawezekana kaka manaake kaivalia njuga sana
 
Kila mtu ni usalama wa taifa,usipolinda usalama wa taifa lako nani atalinda? Ndio maana kuna ulinzi shirikishi,sungusungu na polisi jamii wote hao ni kulinda usalama wa taifa.

Kwa Mtizamo wangu Ningeliomba jina la Usalama wa Taifa libadilike wawe na Jina Lao Maalum Kama ilivyo kule USA UK Urusi nk na itungwe Sheria Kali sana ili Mtu akijifanya usalama fake ahukumiwe jela Miaka 30 angalau watapungua Usalama fake wanaotamba kwenye mabaa na mitaani .
 
huyo ni tapeli mzuri kwenye jiji hili kabla hajahamia huko buza amekaa sana tabata relini, tena anafahamiana na wakubwa kuliko kawaida, nilicho shangaa ni kukutwa na silaha naanza kufikiri ata ujam,,,baz anashiriki
 
huyu atakuwa usalama au wanataka kumrahisishia utendaji wake wa kazi,,ili watu wasijue ni usalama
Naungana na wewe mkuu kwani kilichonishangaza wakati akuonyeshwa na Kova kwenye TV alikuwa ni mtu mwenye furaha hasiye na wasiwasi wowote huku akicheka na kwa nini Kova aliamua kumtambulisha hadharani tofauti na waharifu wengine?
 
Lisemwaloo.........
 
Back
Top Bottom