Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watu wanaojiita Usalama ni wengi sana na hilo ni kosa, idara yenyewe ya Usalama imeshindwa kudhibiti hii hali, manake kweli kujiita usalama ni kosa kisheria lakini la pili ni kwamba unajiita ili iweje, sasa hilo kosa la pili manake sasa ukijiita usalama unatapeli au unajipatia favour flani, nachojua huu ulikua ugomvi wa kiwanja na ndio sababu huyu jamaa akakamatwa sasa kusema ni au sio usalama ni kazi ya polisi kudhibitisha, je kama amekua usalama kwann wao hawakumjua siku zote mpaka juzi kiwanja kilipoleta gogoro na kwamba hicho kiwanja kinahusisha ndugu wa mkuu wa polisi ilala, kumbe walikua wanajua ila sasa ni mchezo wa kutegeshana ukiingia anga zao wanakuliza wakati hujaingia anga wanajua ww ni mharfu ila wanakaa kimya maajabu ya Tanganyika hii!!
nimjuavyo huyu jamaa si mtu wa usalama namfahamu vizur sana, tushaingia nae ofisi nyingi kwa hicho cheo, kama humjui acha usitee, ila sita sema kwani alishanitishia maisha yangu
Watu kama hawa ni wengi sana, na baadhi yao huwa wanapeleka taarifa za uongo kwenye chama fulani hivi cha siasa, halafu viongozi wa chama hicho huitisha mkutano na waandishi wa habari na kuueleza uma kwamba wamepewa taarifa kutoka ndani ya TISS, hahahahahaaaaa! Shame. Wanaokoteza vitaarifa vya uongo halafu wana exaggerate ili kufanikisha lengo lao! Endeleeni kuwatumia matapeli wanaojifanya TISS. Kuvuja kwa pakacha.....
mkuu nitafunguka, subiri nitafute vifaa vya kuzuia maumivu wakati wa kung'olewa MENO, KUCHA na KOPE kwasababu hayo mambo mtu hafanyi peke yake ni mtandao mkubwa tena kibaya zaidi hata TISS wanashiriki kwasababu unakuta TISS feki anakuwa rafiki mkubwa wa TISS wa kweli, hii humpa ujasiri wa kutapeli watu kwani hujua baadhi ya mbinu za tiss kupitia kwa marafiki zake, tofauti yao kubwa ni kuwa hawa TISS wa kweli hawasemi cheo chao mara nyingi ila hawa feki hujitambulisha kwa cheo ili uingie mkenge, hata kova alipomtambulisha hadharani alikuwa sahihi, ili watu wamjue wasitapeliwe tena, lakini pia wapo waliotapeliwa bila kujua wametapeliwa
Hivi hii movie iliishia episode ya ngapi????
steling nadhan alikufa,lakn h n bongo yaja nyingne stay tuned
huyu jamaa yuko nje kwa ile mikwara ya Kova na jamaa kuwa nje ndani ya muda mfupi inaacha maswali mengi
Ngoja tukusaidie ingawa ni nje ya thread,miaka ya 90 I mean 1990's hivi kulikuwa na tatizo sana na uwindaji wa ndovu kule tarangire/manyara!jamaa aliyekuwa anapiga biashara hii alikuwa mwarabu mmoja maeneo ya Galapo Babati,sasa kumpata nyendo zake na ushaidi ilikuwa kazi kweli!akatumwa TISS mmoja ambaye alipofika galapo akawa anajifanya ni kichaa,anabeba makopo mauchafu uchafu nk!yule mwarabu alikuwa na matrekta na mgahawa,basi jamaa akajijengea mazoea ya kwenda kuomba omba chakula pale,kwa sababu hakuwa akipiga mtu wala kuwa na neno na mtu ikawa rahisi kuzoeleka,taratibu jamaa akawa hata mwarabu akiwa na waarabu wenzie friends yeye anaenda na kuzunguka zunguka..hakuna aliyekuwa akimtiliia maanan as wote walijua ni kichaa!mshkaj alikusanya ushaid wa kutosha,audio as alikuwa akiwarecord,alipokuwa na uhakika na kujua huwa wanaficha wap pembe jamaa aka-organise police wakaja na defender,jamaa akamkamata mwarabu baada ya kumtolea na vitambulisho!watu wote hawakuamin kuwa yule kichaa ndo alikuwa TISS na kufanikiwa kumtia mikonon na ushahid juu wa uhakika mwarabu!to cut the story shot,go find anyone aliyetoka maeneo ya galapo huko babati ambaye ana miaka 30 plus/au alikuwa galapo miaka ya 90 hivi ,uulizie hii taarifa kama hujathibitishiwa.
Hivi hii movie iliishia episode ya ngapi????
Sasa hapa tuseme Kova alikuwa msanii au?? Mbona jamaa akula bata tu au ni nini kinaendelea wanajamvi???
jamaa mbona yupo uraiani