Ofisa wa Afya Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe afukuzwa kazi kwa madai kughushi cheti

Ofisa wa Afya Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe afukuzwa kazi kwa madai kughushi cheti

- Halmashauri ina Mkuu wa Wilaya, ambaye yup kisiasa kumuwakilisha Rais na kazi yake ni kusimamia ulinzi na usalama wilayani

- Mkurugenzi Mtendaji ambaye yupo incharge na Idara zote katika Halmashauri

- Halafu kuna DAS,

-Bado huyu Mwenyekiti wa Halmashauri kazi yake ni ipi sasa?

Huu ni utumiaji wa pesa za serikali vibaya
Kwanini upate tabu,soma Katiba ujue serikali za Mitaa ni nini na ina hadhi gani ki nchi,then utakuwa umejipata kwa habari ya swali lako. Asante
 
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe lililojigeuza kamati ya Uamuzi, limemfukuza kazi aliyekuwa Ofisa wa Afya wa Wilaya, Winston Nongwa, kutokana na kughushi cheti cha kidato cha nne kinyume cha sheria na kanuni za nchi.

Sambamba na azimio hilo, baraza hilo limetoa onyo kali kwa Ofisa Utumishi wa Wilaya hiyo, Singo Bakari, na Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kamasi, Deus Magesa, kwa kuwakata mshahara wao kwa asilimia 15 kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kufanya uzembe katika kazi zao na kuiingizia serikali hasara.

Akisoma maazimio hayo katika Baraza la Madiwani la Robo ya Nne ya Mwaka wa fedha 2023/24, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Joshua Manumbu, alisema baraza limefikia uamuzi huo kutokana na makosa waliyo nayo kila mmoja.

“Ofisa Afya Nongwa anakabiliwa na kosa la kugushi cheti cha kidato cha nne wakati akifahamu kufanya hivyo ni kukiuka matakwa ya sheria, hivyo uamuzi huu ni moja ya majukumu yetu katika halmashauri ikiwa ni pamoja na kusimamia nidhamu na utendaji kazi wa watumishi wote,” alisema.

Kwa upande wa Singo, alisema atakatwa mshahara wake kwa asilimia 15 kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo kwa kosa la kutokutekeleza maelekezo ya mwajiri wake na kumsabishia hasara ya Sh. 800,000.

Kadhalika, alisema Magesa naye anakabiliwa na adhabu hiyo hiyo kwa kosa la utoro kazini na kwamba adhabu hizo zimetolewa ili iwe fundisho kwa watumishi wa umma.

Aidha, baraza hilo lilitoa onyo kwa Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Selema, Rwegana Matala, kwa wizi wa Sh. milioni 1.5 ambazo ni michango aliyokusanya kutoka kwa wananchi kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika Shule ya Msingi Selema na ameamriwa kuzirudisha.

Katika hatua nyingine, Baraza hilo lilipokea taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na mradi wa BOOST unaoendelea kufanyika katika Kata ya Bukanda kwa kipindi cha robo ya nne 2022/23.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Emmanuel Shelembi, alisema serikali ilielekeza Sh. milioni 100.6 za BOOST kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa na matundu matatu ya vyoo. Mradi huo umekamilika kwa asilimia mia moja.

Shelembi alisema pamoja na ujenzi huo, serikali ilipeleka Sh. Milioni 76.6 katika zahanati ya Busunda kwa ajili ya ujenzi wa choo, kichomea taka, mnara wa tangi la maji, upanuzi wa chumba cha kujifungulia wajawazito na sehemu ya kuvalia nguo kwa wanawake wanaojifungua na ujenzi huo uko katika hatua za ukamilishaji.

Chanzo: Nipashe
Rwegana Matala anayetuhumiwa kwa kosa la kuiba shs. Mil 15 amepewa onyo kwa sababu alizila na madiwani, vinginevyo angeishia mahakamani.
 
1000122281.png
 
Alipwe nssf yake aendelee na maisha yake kwa sababu ndio utaratibu mliouunga mkono.
 
Utofauti wa majina na mwaka wa kuhitimu/kuajiriwa si vinaweza kufanya tatizo liwe palepale
Wengine walivyoambia kujiendeleza walitaka short cut, ndo kushindwa kwenda qt na kufoji vyeti.
 
Mwenyekiti wa Halmashauri/ mayor ni speaker wa Council Kama ilivyo speaker na bunge.

Inapokaa Full council (Mkutano mkuu wa Halmashauri, speaker ni Mwenyekiti wa Halmashauri/mayor na Katibu wake ni DEDb na Wajumbe ni madiwani akiwemo Mbunge wa eneo husika).

Ukiingia mgogoro wa kiutumishi fuata utaratibu, achana na masuala ya kusuluhishana kwa DC utapoteza muda
Hii kazi angeweza kufanya Mkurugenzi tu
 
Back
Top Bottom