KERO Ofisi ya Afisa Elimu Jiji Dodoma haina utaratibu mzuri wa kusikiliza Wananchi wanaohitaji huduma za Afisa Elimu

KERO Ofisi ya Afisa Elimu Jiji Dodoma haina utaratibu mzuri wa kusikiliza Wananchi wanaohitaji huduma za Afisa Elimu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Ofisi ya Afisa Elimu Jiji Dodoma haiko na utaratibu mzuri wa kusikiliza Watu wanaohitaji huduma za Afisa Elimu.

Nimekuwa nikifuatilia barua ya ruhusa wiki mbili sasa lakini kila nikienda nakutana na PS naambiwa mpaka boss awepo.

Akija Afisa Elimu anakaa dakika tano ofisini kisha anatoka anasema anarudi muda mfupi ujao, baadaye anatuma ujumbe kwa PS kuwa hatarudi mpaka keshoyake, huo umekuwa ndio utaratibu tangu nifatilie hili suala langu.

Watu wengi wanakuja pale wanaishia kukalishwa tu kwenye mabenchi kisha saa tano wanaambiwa waje kesho na kesho inakua kesho tena.

Waangalie utaratibu mzuri wa kusikiliza shida za watu au awekwe msaidizi wake.
 
Back
Top Bottom