econonist
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 20,189
- 29,663
Kwa maoni yangu yanayotokana na mashambulizi dhidi ya ofisis ya CAG, ni bora tuifute ofisi hiyo maana ni Kama inadharaulika.
Naomba nijadili matukio mawili ambayo yamesabaisha nifikie hitimisho hilo. Nikiondoa tukio la CAG Assad kuitwa mbele ya kamati ya bunge kujieleza kipindi Cha ndugai.
Kwanza, bunge limeonesha kupambana na ofisi ya CAG. Kwa Sasa bunge haliipi ripoti ya CAG uzito wowote. Ni Bora bunge lijadili azimio la kumpongeza Rais au maadili, lakini kutenga siku tatu kujadili mambo mazito Kwenye ripoti inaonekana ngumu mpaka kurushwa mwezi wa kumi na moja amabpo ushahidi utakuwa umeondolewa na maofisa wa CAG kunyamazishwa.
Pili, serikali kupitia msemaji wake imeishambulia ofisi ya CAG kwa kudai kuwa wafanyakazi wa ofisi hiyo ndio wenye kasoro. Moja kwa moja inaoenekana serikali haiamini ripoti za CAG na kuwashuku maafisa wa CAG kupika takwimu.
Sasa Kama bunge na serikali haiiamini ofisi ya CAG basi ni bora tuifute hiyo ofisis ili ufisadi uendelee bila ufuatiliaji, Kuliko kuizodoa na kuikashifu ofisi ya CAG kisa imetoa ripoti yenye kuonesha ufisadi mkubwa.
Ni unafiki wa kuendelea kulipa mabilioni ya shilingi Kwenye ofisi ya CAG wakati ripoti yake tunaidharau na kuishamblia na wala haitekelezwi.