Kwa Tanzania hata Katiba iwe nzuri kiasi gani bila utashi wa kisiasa hakuna litakalofanikiwa. Katiba inampa mamlaka CAG kuwa huru, lakini Kuna kipindi alihojiwa ikulu Kama Ni kweli Trilioni 1.5 zilipotea.
Ni kwa sababu tume "politicized" kila kitu ikiwemo ufisadi na jinai nyingine. Siasa tupu hata paspo hitajika siasa na "utashi".
Nikupe mifano kuonyesha ubovu na udhaifu wa Katiba na mfumo wetu wa sasa - na kwa nini "maadui" Rushwa, Ufisadi, Umaskini na Ujinga vimetushinda tangu uhuru.
1. Rais wetu - mwenye mamlaka ya kifalme/emperor anamteua CAG, Director of PCCB, DPP, DCI, IGP, RPC, RC Mawaziri na ma DED (wote hao ni mhimili wa Dola - Utawala). Wanakula kiapo cha utii kwake. Pamoja na wenzao hapo chini #2.
2. Halafu Rais anawateua Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi na majaji (Mhimili Mwingine wa Pili wa Dola uitwao Mahakama)
3. Tena Rais wetu ni mwenyekiti wa chama chake na anamteua Spika na Naibu wake kuongoza Mhimili wa Tatu wa Dola uitwao Bunge.
Na 2020 Rais Magufuli aliteua Wabunge wote i.e. Bunge lote la sasa!
NB: Duniani hakuna mwanadamu yeyote chini ya jua mwenye uwezo au ni genius wa kutenda kwa ufanisi, weledi wala haki hayo majukumu yote. Na ni kawaida kabisa Rais yeyote atazidiwa na/au kuwa influenced na wanaomzungaka!
Watu hutoa utetezi 'dhaifu' kuwa Rais ni taasisi na sio mtu mmoja, lakini hakuna mantiki, uhalali wala ukweli kwenye hilo. Hayati Magufuli aliwahi kusema hataki kushauriwa wala "kuingiliwa"!
Ona maigizo na vichekesho sasa:-
CAG anakagua mahesabu, anamaliza na kutoa ripoti kwa Mamlaka ya Uteuzi - Rais.
Ripoti yake inakabidhiwa kwa Bunge ili kubaini na kutolewa "Mazimio ya Bunge" ili Serikali i.e Mamlaka ya Uteuzi ichukue hatua. (Usisahau sifa za kuwa mbunge ni kujua kusoma na kuandika). Eti hao wakae kama Mahakama ya Kangaroo inayoitwa 'Kamati' kupitia na kuamua mambo ya kitaalam na kiweledi ya kijinai ya ripoti ya CAG!
Halafu kuna wanaotaka kumlaumu Rais ki rejareja wakati sheria zetu zinatamka hivyo.
Worst still, hata Azimio la Bunge likesema fulani ashtakiwe, PCCB, Police na DCI watachunguza na kuandaa mashtaka, lakini ni DPP atakayeamua kesi iende mbele au la, na pia iendeje! Huo nao ni mhimili wa kiaina ktk mfumo wa sasa. Plea bargains za hayati Magufuli na Biswalo ni mfano mzuri.
Si utaona wazi tu shida iko wapi.
Jamani hatujawahi kuwa serious kupambana na rushwa wala ufisadi-ni siasa tu.
Tumejidanganya na kudanganywa kuna mihimili mitatu, ukweli ni kwamba uko mmoja tu "uliojichimbia chini" unaoamua na kufanya kila kitu nchini. "Check and Balance" ni hadithi ya kusadika tu. Ndugai alipotofautiana na huo, alikaa pembeni fasta! CAG Assad alitupwa bench alipotofautiana nao. Hamuoni?? Hamsikii??
Inatosha! Tupeni Katiba Mpya sasa.
::Katiba ni utaratibu tutakaojiwekea wa kujitawala; kupambana na changamoto za sasa na mazingira na mahitaji ya sasa na ya baadaye. Pia ni uti wa mgongo wa Sheria zote za nchi na pia chimbuko la MAMLAKA na Power.
Tutapunguza madaraka na influence ya Rais. Tutaunda mfumo tofauti na huu, tutangeneza Taasisi huru na zenye nguvu na mamlaka kiutendaji na kimamlaka zitakazoshughulikia mambo yale kwa ufanisi na kwa haki - kwa haraka.