Ofisi ya CAG ifutwe kama hatutaki kupambana na ufisadi

Ngoja kwanza niwape maarifa,kwani afisi Iko chini ya nani,Sasa kwa nini ifutwe wakati haina madhara? Mi napendekeza afisi tuwape jeshi.
Ni Bora, jeshi linataka kazi kazi na linaogopwa. Shida ni halina wataalamu wa kutosha.
 
Wanyamazishwe? Mbona tayari wawili wameishanyamazishwa others to follow aisee! Be very very extra careful braza K! 😭
 
Ripoti inasema pesa zilizoibiwa ni zaidi ya bajeti ya nchi ambayo hata utekelezaji wake ni almost 40 % ni mwehu tuu anayeweza iamini hyo ripoti

Naweza kuiamini maana kuna sehemu sektaz kuna watu wanaifyonza hii nchi dah! [emoji2367][emoji2367]
 
Mama hana nia ya kufuta ubadhilifu hapa nchini kwani kazungukwa na wezi ambao pia wanamsaidia katika shughuli zake za kifisadi, Mama hana tofauti na mshauri wake mkuu, Kikwete.
 
Wanyamazishwe? Mbona tayari wawili wameishanyamazishwa others to follow aisee! Be very very extra careful braza K! 😭
That's my point. Tunaanzisha ofisi halafu ufisadi ukiwekwa wazi tunaanza kupoteza watu. Unaanzisha ofisi ya ukaguzi sasa ukaguzi ukifunua ufisadi tuanaanza kuwinda watu Tena.
 
Mama hana nia ya kufuta ubadhilifu hapa nchini kwani kazungukwa na wezi ambao pia wanamsaidia katika shughuli zake za kifisadi, Mama hana tofauti na mshauri wake mkuu, Kikwete.
Kweli kabisa mkuu hakuna nia ya dhati ya kupambana na ufisadi kutoka kwa mkuu wa nchi. Wezi ndio wenye sauti kwa Sasa.
 
Ofisi ya CAG ni muhimu Kwa nchi iliyostaarabika! Nchi yetu bado haijastaarabika, kwahiyo ofisi hii ni takataka! Huwezi kuanzisha ofisi ya CAG ambayo uchunguzi wake hutaki kuusikia!
 
Kawashika makalio wao wenyewe wamekuja kwa hamaki kwamba ripoti imekosewa. Walikuwa wamezoea kukenua meno kumshambulia JPM sasa ni zamu yao na bado mwakani mambo ni mabaya sana kwa upigaji serikalini
 
Kweli kabisa mkuu hakuna nia ya dhati ya kupambana na ufisadi kutoka kwa mkuu wa nchi. Wezi ndio wenye sauti kwa Sasa.
Kumbe unajuwa, Mama mwenyewe ni mbadhilifu na ndiyo maana anawanyamazia vijana wake wezi. Ni kitu kilicho wazi kabisa, aipitie tu ile ripoti ya CAG yeye mwenyewe.
 
Nilipoiona Ile report nilifurahi Sana, maana niliona jirani yangu hapa Kimara kwisha habari yake maana huyu bwana utadhani ndani kwake Kuna mashine ya hela.
Lakini ndio kwanza mkewe na mtoto ndito ya kuolewa wako Dubai tangu jumamosi iliyopita.
 
Ukiona hivi basi juwa Mama mwenyewe anahusika na ndiyo maana hakemei kitu. Nchi imeharibika sana chini ya Mama akishauriwa na Kikwete na Mze Makamba.
 
Yote majizi tu iwepo, isiwepo hamna tofauti yanaiba mfuko huu yanaweka mfuko huu mwingine na tushaambiwa report imekosewa tufanyeje🤷‍♂️
 
Naunga mkono hoja hiii 💯💯💯💯

Let aside the unprecedented deaths of the CAG officials....
DAMN this country😒
 
Shida sio katiba mpya utashi wa kisiasa wa hawa Viongozi wa bunge na serikali.
Unajua utashi wa watu wanaotafuta vyeo vya kisiasa? Kikubw ni mamlaka na mali. Bila kupigania katiba bora utasubiri huo utashi hadi mbingu zishuke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…