Ofisi ya CAG ifutwe

Ofisi ya CAG ifutwe

Unitman

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
511
Reaction score
671
Habari za kazi ndugu wadau.Napendekeza CAG aondolewe kwenye mfumo na nafasi yake ichukuliwe na wizara zenyewe ziwajibike kwa bunge.

Ofisi ya CAG kwa sasa imejiingiza kwenye ufisadi na hakuna masirahi kwa taifa.

Nasema hivyo kwa sababu kama CAG atakagua kihalali hakuna halimashauri au taasisi ya serikali itapata hati Safi.

Kila ofisi ya serikali ina matumizi yasiyokuwa na msingi ni poshoo tu na manunuzi mengi ni ya kifisadi hayazingatii thamani ya fedha yaani value for money.

Wao wanaangalia makaratasi bila kuangalia thamani ya fedha ni wahasibu wa kukariri na wa mchongo hawana msaada wowote kwa taifa.
 
Naunga mkono hoja..pia hao wakaguzi ndio wanaogoza kwa kula rushwa ili wafute hoja mbalimbali za wizi wa pesa kwenye halmashauri na taasisi mbalimbali za serikali.

#MaendeleoHayanaChama
 
Naunga mkono hoja , ni ofsi ya kuchafuana tuu na kujichukulia sifa , ndo mana Maghufuli alimfukuza Yule pimbi
 
Kinacho kera kwenye hii office ni kama gazeti tu wana andika ma report lakini hakuna action zozote ni kama pambo
 
Naunga mkono hoja, ni bora hiyo ofisi ikahamishwa kuwa kitengo kimojawapo cha TAKUKURU
 
Taja kiongozi ndani ya CCM ambae sio fisadi
 
Naunga mkono

Kuna jamaa zangu fulani Wafanyakazi wa hiyo ofisi kuna kipindi wakienda kukagua lazima warudi na pesa ya maana.
 
Back
Top Bottom