KWELI Ofisi ya Msajili yawasihi CHADEMA kusitisha Mkutano uliopangwa kufanyika Julai 23, 2023 huko Bulyaga, Temeke

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Kwa hiyo ni Kanisa ndio adui wa serikali ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na sio Chadema?

Na kwa vile Kanisa ni waumini wake, una maanisha kuwa wakristu ndio wanaompinga Mheshimiwa Rais?

Na ili aweze kuwashinda unamshauri aelekeze nguvu zake kudhibiti Kanisa na wafuasi wake?

Seriously?

Amandla...
 

Kanisa gani limewakodi CHADEMA?
 
Hizo ni propaganda za CCM na machawa wa DP world.
Mkutano wa CHADEMA uko pale pale.

Toka lini msajiri akawa na mamlaka ya kuzuia mkutano wa chama cha siasa?
Msajiri amejuaje content za mkutano husika kabla ya kufanyika?
Msajiri=msajili
 
Acha kufananisha kanisa na vitu vya kipuuzi, mkutano wa watu kadhaa ugeneralize kanisa, timamu kweli?
 
Huyo Mutungi ni mtungi hasa.

Kiongozi wa dini kuhudhuria mkutano hakuna kosa lolote. Na ndiyo maana tumeshuhudia viongozi wa dini hata wakati wa mikutano ya kampeni ya vyama vya siasa wakisimama kwenye majukwaa ya mikutano.

Kisichoruhusiwa ni viongozi wa dini kutumia nyumba za ibada kufanya siasa za vyama.
 
Hatujawahi ona mkutano uliojaa mapdri na maasikofu Kama mkutano uliotarajia kufanyika leo, ulileta maswali mengi sana, tunashukru kwa kufutwa Tunaomba wahusika wahojiwe walikuwa na maana gani
 
Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi, amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kusitisha mkutano wake uliopangwa kufanyika kesho huko Buriaga, Temeke jijini.

Akizungumza leo, Jaji Mutungi amekikumbusha Chama hicho kuheshimu na kufuata sheria za nchi zinazosimamia usajili wa vyama huku akiwaita ofisini Jumatatu.

Aidha Wadau mbalimbali wameshangazwa kitendo cha chama hicho kuchanganya dini siasa na harakati.

Itakumbukwa baraza la Maaskofu lilitoa taarifa ya kusikitishwa na kitendo cha CHADEMA kusambaza uzushi kuwa Katibu wa TEC atakuwepo kwenye mkutano wao.

Chama chetu kina entaitain uongo halafu kinataka kishike dola?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…