KWELI Ofisi ya Msajili yawasihi CHADEMA kusitisha Mkutano uliopangwa kufanyika Julai 23, 2023 huko Bulyaga, Temeke

KWELI Ofisi ya Msajili yawasihi CHADEMA kusitisha Mkutano uliopangwa kufanyika Julai 23, 2023 huko Bulyaga, Temeke

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
IMG_8100.jpeg


Inadaiwa kuwa Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi, amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kusitisha mkutano wake uliopangwa kufanyika kesho Julai 23,huko Buriaga, Temeke jijini Dar es Salaam.

IMG-20230723-WA0019.jpg
IMG-20230723-WA0020.jpg

Barua inayodaiwa kuandikwa na Sisty Nyahoza, Naibu Msajili wa vyama.
 
Tunachokijua
Mamlaka ya Ofisi ya Msajili ni kama yalivyoainishwa na taarifa iliyochapishwa tarehe 22/04/2016 kwenye Gazeti la Serikali No 143 & 144 hufanya majukumu ya uratibu wa uhusiano katika vyama vya siasa na Serikali.

Ofisi hii imejikita katika usimamizi wa Sheria ya Vyama vya Siasa Na 5 ya mwaka 1992 na Sheria ya Gharama za uchaguzi ya mwaka 2010 ili kuhakikisha uwepo na ukuaji wa demokrasia ya vyama vingi nchini.

Madai ya Kuzuiwa kwa Mkutano wa CHADEMA
Yakiwa yamebaki masaa machache kabla ya kuanza kwa Mkutano un anaohusu masuala ya Uwekezaji Bandarini unaoihusu Serikali ya Tanzania na Kampuni ya DP World ya Dubani, taarifa zinazodai kuzuiwa kwa mkutano huu zimeanza kusambaa mtandaoni.

Julai 22, 2023, saa 5:17 usiku, Kurasa za Mitandao ya kijamii inayomilikiwa na Maulid Kitenge ilichapisha habari hiyo ikisema:

Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi, amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kusitisha mkutano wake uliopangwa kufanyika kesho huko Buriaga, Temeke jijini.

Akizungumza leo, Jaji Mutungi amekikumbusha Chama hicho kuheshimu na kufuata sheria za nchi zinazosimamia usajili wa vyama huku akiwaita ofisini Jumatatu.


Baadae, Barua inayotajwa kuandikwa na Naibu Msajili wa vyama, Sisty L. Nyahoza yenye wito huo huo wa kusitisha mkutano ilianza pia kuonekana mtandaoni.

Barua hiyo ilienza mbali zaidi kwa kuwaita viongozi wakuu wa CHADEMA walifike kwenye ofisi yake, Julai 24 kwa ajili ya mazungumzo.
Sehemu ya barua hiyo inasema:

“Hivyo, Msajili wa Vyama vya Siasa akiwa ndiye mwenye jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa yenye masharti ya yanayokataza masuala hayo na akiwa ni mlezi wa vyama vya siasa, anawasihi CHADEMA msitishe mkutano huo a viongozi wen waku kufika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa tarehe 24 Julai 2023 saa nne asubuhi kuonana naye, ili kuongea kuhusu suala hilo a masuala mengine ya utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa.”

Ukweli wa taarifa hii
JamiiForums imebaini kuwa taarifa hizi ni sahihi, zimetolewa na mamlaka husika.

Ukweli wa taarifa hii umethibitishwa pia na Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika, jioni ya Julai 23, 2023 wakati mkutano huo unaendelea. Amesema:

“Jana jioni nilipokea barua ya msajili wa vyama vya siasa, kama mtendaji mkuu wa chama akinieleza kwamba tuahirishe, tuufute huu mkutano wa leo. Sasa kwa sababu nilipokea nje ya muda wa ofisi, na chama chetu kinafanya kazi kitaasisi, kwa vikao, nikabaki nayo. Na busara zikanielekeza kwamba tuendelee na mkutano huu.”

Awali, Julai 22, 2023, Jeshi la Polisi lilikiri kupata taarifa ya uwepo wa Mkutano huo na kusisitiza ufanyike kwa kuzingatia sheria zilizowekwa.

Mkutano huu unaungwa mkono na CHADEMA pamoja na Sauti ya Watanzania, klabu maarufu iliyoanzia kwenye mtandao wa Clubhouse ikiwa na mkusanyiko wa watu wengi ikiwemo watanzania waishio nchi za nje (Diaspora).

Baadhi ya sababu zilizopelekea Ofisi ya msajili kutoa wito wa kusitisha Mkutano huo ni CHADEMA kualika watu wasio wanachama wake kuhuduhuria mkutano huo.

Miongoni mwa watu hao ni viongozi wa dini na taasisi nyingine ikiwemo Rais wa Chama cha Wanasheria cha Tanzania Bara (TLS) pamoja na kutoa matangazo ya mkutano yenye picha za viongozi wa dini wakiwa na nguo rasmi za taasisi zao za dini.

Kwa mujibu wa msajili, jambo hili sio sawa, ni ukiukaji wa sheria za nchi zinazokataza vyama vya siasa kuwa na udini na kutumia dini kufikia malengo yake ya kisiasa.

Pia ni ukiukaji wa sheria zinazokataza taasisi za dini kufanya shughuli za kisiasa hivyo amewataka CHADEMA kufika ofisini kwake, Julai 24, 2023 kwa ajili ya mazungumzo yanayohusu utekelezaji wa Sheria ya vyama vya siasa.

Akijibu wito wa kufika Ofisi ya Msajili wa vyama, Mnyika amebainisha kuwa CHADEMA hakitakwenda kwa sababu ni chama kinachosikiliza maoni ya umma.
INFACT CHADEMA INATAKIWA KUFUTWA,IMESHAKIUKA KANUNI ZA MSINGI,NA MIIKO YA USAJILI,ZA KUTOCHANGANYA SIASA,DINI,NA KUCHOCHEA MGAWANYIKO,KATI YA UTANGANYIKA NA UZANZIBAR HUKU WAKIFAHAMU FIKA YA KWAMBA TUMEUNGANISHWA SOTE NA KUWA WATANZANIA.
Utafutwa wewe lakini siyo chama chochote kile cha siasa ambacho kipo kwa mujibu wa sheria za nchi. Hakuna mwenye uwezo wa kukifuta chama chochote cha siasa.

Kama tungekuwa makini, chama kilichotakiwa kufutwa ni CCM, ambacho kimekuwa chama dola badala ya chama cha siasa, kama sheria inavyotaka.
 
Yaani habari yenyewe ni kutoka Kitenge Tv? Sasa huyo mtu anatofauti gani na toilet paper?

Mkutano haisimishwi na hamna la kufanya, mkitaka futeni usajili wa cham, au nendeni mkaue watu kwenye mkutano; hatuwezi kukubali kuuzwa huku tunajiona

Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Utafutwa wewe lakini siyo chama chochote kile cha siasa ambacho kipo kwa mujibu wa sheria za nchi. Hakuna mwenye uwezo wa kukifuta chama chochote cha siasa.

Kama tungekuwa makini, chama kilichotakiwa kufutwa ni CCM, ambacho kimekuwa chama dola badala ya chama cha siasa, kama sheria inavyotaka.
Kuna kanuni zinazosimamia vyama hivi aidha kwa kukiuka kanuni hizi chama chochote mile kipewe adhabu Kali ,ikiwepo kutokujihusisha na masuala ya siasa kwa miaka miwili (2).
 
Hatujawahi ona mkutano uliojaa mapdri na maasikofu Kama mkutano uliotarajia kufanyika leo, ulileta maswali mengi sana, tunashukru kwa kufutwa Tunaomba wahusika wahojiwe walikuwa na maana gani
Mimi pia napendekeza viongozi wa kisiasa wasiwe wanaapa kutumia vitabu vya Dini wawe wanatumia Katiba ya inch. Kutumia vitabu vya Dini ni kuchanganya Dini na siasa kwasababu wanachoenda kukitumikia si kitabu cha dini ni katiba ya inch. Pia viongozi wa dini wasiwe wanashiliki kitika mikutano ya viongozi wa kisiasa
 
Hao maaskofu mmewalipa shilingi ngapi kuja kwenye huo mkutano wenu?
Walipwe wana nini cha zaidi? Kila mmoja anakwenda kwa mapenzi yake, au unadhani hao maaskofu wana njaa za hivyo? Vumilieni tu watu kuongea ukweli. Zama za kutawala makandoo zilishapita.
 
Mama Samia achana hii kitu, ni ushauri wa bure tu warudishie watanganyika Bandari yao ili uwe na amani rohoni, vinginevyo kazi kwako itakuwa pevu mno.

Wenye mali yao wanasema hawamtaki mwarabu, sasa tatizo lipo wapi kumwambia mwarabu aondoke zake? hapa ndipo tunapopata wasiwasi kwamba kuna kitu kinazunguka zunguka chini ya kapeti.
 
Matusi ya nini? Wananchi hawawaamini tena chama chenye kuwagawa kwa misingi ya dini.
Uzuri kwenye kipimo cha Imani ya wananchi ni kwenye box la kura, huko imedhihirika pasi na shaka kuwa CCM haiheshimu kipimo hicho. Ni bahati mbaya CCM imeng'ang'ania kubaki madarakani kwa shuruti hadi kizazi kimebadilika, huku yenyewe ikilizimisha kutawala kizazi kisichoikibali. Ndio hapo unaona inatawala kwa hila, mabavu, wizi wa kura, vitisho, rushwa na upuuzi mwingine kama huo. Fahamuni wakati ni ukuta.
 
Huyu mutungi ameanza tena uhuni wake wa miaka yote!
Hivi majaji mnaona namna huyu mtu alivyoharibu heshima ya Ujaji na anaendelea kuiharibu!
Huyu mtu anatumika na ccm na hizi vurugu zilipangwa na ccm ili kufanikisha kuzuia huu mkutano ili wananchi wasijue ukweli wa utapeli wa makataba wa DPW
 
Mama Samia achana hii kitu, ni ushauri wa bure tu warudishie watanganyika Bandari yao ili uwe na amani rohoni, vinginevyo kazi kwako itakuwa pevu mno.

Wenye mali yao wanasema hawamtaki mwarabu, sasa tatizo lipo wapi kumwambia mwarabu aondoke zake? hapa ndipo tunapopata wasiwasi kwamba kuna kitu kinazunguka zunguka chini ya kapeti.
Tatizo ni namana ya kutapika ule mlungula kwani tunaambiwa wengine wameshanunua appartments Mikocheni
 
Mama Samia achana hii kitu, ni ushauri wa bure tu warudishie watanganyika Bandari yao ili uwe na amani rohoni, vinginevyo kazi kwako itakuwa pevu mno.

Wenye mali yao wanasema hawamtaki mwarabu, sasa tatizo lipo wapi kumwambia mwarabu aondoke zake? hapa ndipo tunapopata wasiwasi kwamba kuna kitu kinazunguka zunguka chini ya kapeti.
Alishachukua hela ya mwarabu maana hazina ilikuwa haina kitu ili kuendesha mambo ya serikali. Ule uongo kuwa tulikuwa tunajenga miradi ya kimikakati kwa fedha zetu ulifikia mwisho.

Wanachoficha kama serikali ni kuweka ukweli huo hadharani maana na nyingine wamezichota wao. Hizo ndio huitwa siri za serikali. Unapoona serikali imeamua kushikilia huo uwekezaji mbali ya hizi kelele ni kwakuwa tayari walishabeba mzigo wa watu kwa kificho. Wanajua bunge ni lao, vyombo vya dola ni vyao hivyo watapata ulinzi wa huo mkataba.
 
View attachment 2696502

Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi, amekitaka Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema kusitisha mkutano wake uliopangwa kufanyika kesho huko Buriaga, Temeke jijini.

Akizungumza leo, Jaji Mutungi amekikumbusha Chama hicho kuheshimu na kufuata sheria za nchi zinazosimamia usajili wa vyama huku akiwaita ofisini Jumatatu.

Aidha Wadau mbalimbali wameshangazwa kitendo cha chama hicho kuchanganya dini siasa na harakati.

Itakumbukwa baraza la Maaskofu lilitoa taarifa ya kusikitishwa na kitendo cha CHADEMA kusambaza uzushi kuwa Katibu wa TEC atakuwepo kwenye mkutano wao.

Chanzo: Kitenge Updates
Chawa kazini
 
ulikuwa ni mkutano wa Injili Jaji Francis yupo sahihi kuzuia
 
Back
Top Bottom