Ofisi Ya Pinda Yakanusha

Ofisi Ya Pinda Yakanusha

Jukumu la kwanza ni kujua kinadharia; Waziri Mkuu hawezi kuzungumzia deployment ya majeshi yetu mahali popote with authority. Hivyo kusema Tanzania iko tayari kupeleka majeshi halafu unamnukuu Waziri Mkuu ni kuonesha hujui majukumu na nguvu za Waziri Mkuu.

Nilishasema tuna matatizo kutoka kwa waandishi wa habari wenyewe!!! Makanjanja wengi!!! haiwezekani gazeti kama lile lifanye oversight kama hiyo, kwa maana nyingine yapo mengine mengi yanayopotoshwa hapa Tanzania?

Issue tu ni kwamba wahusika hawajaleta tamko la kukanusha kama ofisi ya waziri mkuu ilivyofanya
 
Nilishasema tuna matatizo kutoka kwa waandishi wa habari wenyewe!!! Makanjanja wengi!!! haiwezekani gazeti kama lile lifanye oversight kama hiyo, kwa maana nyingine yapo mengine yanayopotoshwa Tanzania?

Mwanakijiji,

The presented notion is that Pinda is a very senior government official and even though he is not the commander in chief, he is above the minister of defence in the food chain, therefore very influential, in the know and can sway and should know our stand on the matter.

Tatizo kubwa zaidi kuliko Pinda ni suala zima la je, tuna a well formulated foreign policy? Au ndiyo mambo ya bendera kufuata upepo?

Maana kama tuna a well formulated foreign policy haijalishi kama ni Pinda, Waziri wa Ulinzi,Mkuu wa majeshi au Mwenyekiti wa chama tawala au hata mtu ambaye hana mamlaka over jeshi in the administration, watu watakuwa hawahitaji hata kuvutana mashati kabla ya kuonana na waandishi wa habari, kwa sababu Waziri Mkuu sio tu atajibu swali, bali atajibu swali na ku quote foreign policy ya Tanzania na ma charter tuliyo members na kwa nini tuko memberz nz objectives zake na ma clause yake anakupa jibu unaburudika.

Sio sasa viongozi wanakupa majibu unaona kama yanatoka vichwani mwao tu.Ndiyo maana mpaka leo hatufahamu kuwa Azimio la Zanzibar la CCM limekuwa amended au hapana, maana muungwana kasema msemo uliolipiga stop kwenye miiko ya uongozi essentially, lakini kalisema kwa kauli yake tu, hakuna kikao chochote kilichofanyika hivyo linakosa nguvu.

Kwa hiyo hii ni cancer kubwa kuliko Pinda.It is a systemic malady.
 
Hapana Pundit;

Hili liko wazi sana kwa wafuatiliaji wa utawala wa taifa letu... na hata hapa JF tulishawahi zungumzia....

Kwa taifa letu Waziri Mkuu anashughulikia zaidi mambo na day 2 day activities za serikali zaidi zikiwa za ndani ya nchi... ndio maana tawala za mikoa ziko kwake, ... wizara kama za habari, utangazaji, mifugo, ujenzi, utalii etc.

Rais wa nchi... huwa ana maamuzi makubwa kwenye mambo ya nje, uchumi, fedha na mipango, ulinzi na vyombo vya ulinzi (amir jeshi mkuu) etc....

Ukiangalia mfumo vizuri wa Serikali ni rahisi kung'amua hili mkuu!!! mgawanyo wa Mamlaka ya Rais na Waziri mkuu uko hivyo!!!

Ndio maana ni rahisi na makamu wake ndio wanaoenda nje ya nchi zaidi kuliko waziri mkuu... kumbukumbu ziko hata kwenye utawala wa awamu ya tatu... kumbukeni safari ile ya Mh. Sumaye aliyetumia fedha nyingi kule marekani baada ya kupata ka-trip ka-nje...

Akatumia almost bugdget yake yote ya safari za nje.

Mwisho: Ni Amir Jeshi mkuu tu ndiye mwenye mamlaka ya kuongelea military deployment yoyote, waziri mkuu, waziri wa mambo ya nje wanaweza tu kuelezea zaidi pale ambapo amir jeshi mkuu ameshaongelea au kuamua kwenye jambo fulani la kiusalama!!! Huhitaji kwenda TSJ kujua hili, Wizara ya Ulinzi ina mawasiliano madogo sana na Ofisi ya Waziri mkuu. Kama ilivyo Wizara ya Utawala Bora, Utumishi etc... etc...
 
Mwanakijiji,

The presented notion is that Pinda is a very senior government official and even though he is not the commander in chief, he is above the minister of defence in the food chain, therefore very influential, in the know and can sway and should know our stand on the matter.

Tatizo kubwa zaidi kuliko Pinda ni suala zima la je, tuna a well formulated foreign policy? Au ndiyo mambo ya bendera kufuata upepo?

Maana kama tuna a well formulated foreign policy haijalishi kama ni Pinda, Waziri wa Ulinzi,Mkuu wa majeshi au Mwenyekiti wa chama tawala au hata mtu ambaye hana mamlaka over jeshi in the administration, watu watakuwa hawahitaji hata kuvutana mashati kabla ya kuonana na waandishi wa habari, kwa sababu Waziri Mkuu sio tu atajibu swali, bali atajibu swali na ku quote foreign policy ya Tanzania na ma charter tuliyo members na kwa nini tuko memberz nz objectives zake na ma clause yake anakupa jibu unaburudika.

Sio sasa viongozi wanakupa majibu unaona kama yanatoka vichwani mwao tu.Ndiyo maana mpaka leo hatufahamu kuwa Azimio la Zanzibar la CCM limekuwa amended au hapana, maana muungwana kasema msemo uliolipiga stop kwenye miiko ya uongozi essentially, lakini kalisema kwa kauli yake tu, hakuna kikao chochote kilichofanyika hivyo linakosa nguvu.

Kwa hiyo hii ni cancer kubwa kuliko Pinda.It is a systemic malady.

Kweli kabisa, na matatizo hayo ya system, ndio yamewafanya pinda na waandishi wote wajiingize kwenye matatizo kama haya. Ukiangalia kwa makini alichokisema Pinda alikuwa anajichanganya kwa kukosa basis ya what he was saying (hiyo well formulated foreign policy), Waandishi nao kwa haraka haraka zao, na kwa kukosa basis ykama reference ya statement ya mukulu, wakaibuka na yao
 
Mpitanjia,

Sidhani kama waandishi wana makosa kama mwenye kutoa maelezo anajichanganya mwenyewe. Yale yale ya Membe alipokuwa anaulizwa misheni ya jeshi letu kule ngazija..... Wako so disorganized hadi inatisha...

Cheche za Rweyemamu sijui zimeishia wapi!?
 
Hapana Pundit;

Hili liko wazi sana kwa wafuatiliaji wa utawala wa taifa letu... na hata hapa JF tulishawahi zungumzia....

Kwa taifa letu Waziri Mkuu anashughulikia zaidi mambo na day 2 day activities za serikali zaidi zikiwa za ndani ya nchi... ndio maana tawala za mikoa ziko kwake, ... wizara kama za habari, utangazaji etc.

Rais wa nchi... huwa ana maamuzi makubwa kwenye mambo ya nje, uchumi, fedha na mipango, ulinzi na vyombo vya ulinzi (amir jeshi mkuu) etc....

Ukiangalia mfumo vizuri wa Serikali ni rahisi kung'amua hili mkuu!!! mgawanyo wa Mamlaka ya Rais na Waziri mkuu uko hivyo!!!

Ndio maana ni rahisi na makamu wake ndio wanaoenda nje ya nchi zaidi kuliko waziri mkuu... kumbukumbu ziko hata kwenye utawala wa awamu ya tatu... kumbukeni safari ile ya Mh. Sumaye aliyetumia fedha nyingi kule marekani baada ya kupata ka-trip ka-nje...

Akatumia almost bugdget yake yote ya safari za nje.

Mwisho: Ni Amir Jeshi mkuu tu ndiye mwenye mamlaka ya kuongelea military deployment yoyote, waziri mkuu, waziri wa mambo ya nje wanaweza tu kuelezea zaidi pale ambapo amir jeshi mkuu ameshaongelea au kuamua kwenye jambo fulani la kiusalama!!! Huhitaji kwenda TSJ kujua hili, Wizara ya Ulinzi ina mawasiliano madogo sana na Ofisi ya Waziri mkuu. Kama ilivyo Wizara ya Utawala Bora etc...

Kasheshe,

Naelewa structure ilivyokaa ndiyo maana nimeigusia hapo juu.Tujue kuwa hapa kilichokuwa kinafanywa siyo kutoa maamuzi (Pinda alikuwa hatoi maamuzi kuhusu Tanzania kupeleka majeshi Zimbabwe) bali ilikuwa anajibu maswali, ambayo ni sehemu hiyo ya day to day jobs za kiserikali.Kwa hiyo hakuwa nje ya mipaka yake kuongelea hilo, kwa sababu inawezekana walishakaa na Amiri Jeshi Mkuu kwenye cabinet meetings huko, Amiri Jeshi akatoa maamuzi kwa mfano, Pinda anachofanya ni kuelezea msimamo wa Tanzania kuhusu hii issue.Kwa hiyo Waziri Mkuu hawi limited kuongelea haya maswala, especially kwa sababu rais hahusiki na kazi za bunge na Waziri Mkuu ndiye Mkuu wa shughuli za serikali bungeni.Hatoi maamuzi hapa, anatimiza wajibu wake wa shughuli za kila siku za serikali, kuwapasha habari wabunge na wananchi ni moja ya shughuli za kila siku za kiserikali.

Ndiyo maana foreign policy ni muhimu sana kwa sababu kama hatuna foreign policy anakuwa na kazi ngumu sana.Lakini kama tunayo foreign policy na waziri Mkuu smart utasikia anaongelea msimamo wa nchi kiujumla halafu ana quote matamko ya Rais, ambaye ni mtu mwenye mamlaka ya kuongelea mambo hayo, kwa hiyo anakuwa anafanya kazi ya kuelezea maamuzi ya rais na foreign policy yetu kwa wabunge na wananchi.Kuelezea kazi za serikali za kila siku ni moja ya sehemu ya kazi za Waziri Mkuu.

Kwa hiyo mimi bado nasema kama Pinda,Mwinyi,Membe na echelon yote haiko in synch na a well formulated foreign policy kama vile wanadini wanavyoweza kuongea kutoka sehemu tofauti lakini hawapingani kwa sababu wanatumia msahafu mmoja, tutakuta leo rais kasema kitu kimoja na waziri mkuu kasema kingine.

Hapo ndipo spin za sikusema hivi, kilipanda kikashuka itaanza, mie ntaenda kuchukua mkanda wa TV footage na kumwambia "Waziri Mkuu unataka kusema hii footage watu wamemtafuta actor anayefanana na wewe?"

Mpaka leo hatufahamu tunasimama wapi kuhusu Zimbabwe, Mkapa alimtetea vikali CHOGM 2000 Australia, lakini hatujui kama ile ilikuwa ni foreign policy ya Tanzania au Mkapa tu? Na kama foreign policy how far will it go kumkumbatia huyu tyrant?

Kikwete ndiyo kabisa, alipigwa mkwala na Mugabe Zambia alivyoingia tu kuwa rais mpaka leo hana hamu naye.Labda ndiyo maana Pinda ana usongo naye kwa sababu anajua muungwana hamfagilii.But where is the policy?
 
Nilishasema tuna matatizo kutoka kwa waandishi wa habari wenyewe!!! Makanjanja wengi!!! haiwezekani gazeti kama lile lifanye oversight kama hiyo, kwa maana nyingine yapo mengine mengi yanayopotoshwa hapa Tanzania?

Issue tu ni kwamba wahusika hawajaleta tamko la kukanusha kama ofisi ya waziri mkuu ilivyofanya

Kasheshe yale ya JK alikuwa anakanusha yeye pekee ama ofisi yake je ulisha wahi kuna mtu wa media anasema ? Wanaambiwa usibishane na mkubwa utaumia so unategemea nini ?
 
Pundit, kwenye hili tatizo siyo kile ambacho Pinda alisema kwani alisema something within his domain (very vague to be honest) lakini gazeti la the Citizen lilimnukuu vibaya kabisa na kimsingi kumfanya aonekane very irresponsible kitu ambacho kilisababisha ofisi ya Waziri Mkuu itaoe maelezo.

Nyani, nadhani mtu anaruhusiwa kula kuona tu... mtu unajua moyo wako ulipo vingine ni vya kusafishia macho tu..
 
Huyo ndie Waziri Wetu Mkuu mpya tuliemtarajia kuonyesha njia esp kwenye hiki kikao cha 11 cha Bunge.
 
Attachments

  • kp_232pinda.jpg
    kp_232pinda.jpg
    14 KB · Views: 55
Pinda: Ikilazimu JWTZ itakwenda Zimbabwe

na Salehe Mohamed na Rachel Chizoza, Dodoma

KITENDAWILI cha hali ya usalama nchini Zimbabwe kinaweza kuilazimisha Tanzania kupeleka nchini humo vikosi vya majeshi yake ya kulinda amani iwapo itaombwa kufanya hivyo na Umoja wa Afrika (AU) au Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).
Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipokuwa akijibu maswali ya papo kwa hapo aliyokuwa akiulizwa na wabunge katika utaratibu mpya ambao ulianza kufanyika jana. Hilo litakuwa likifanyika kila Alhamisi.

Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), ndiye aliyeuliza maswali kuhusu msimamo wa Tanzania kuhusu kusuasua kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi nchini Zimbambwe.

Mbali ya hilo, Zitto alitaka kujua iwapo Tanzania itakuwa tayari kupeleka majeshi ya kumuondoa kiongozi ambaye hatakubaliana na matokeo ya uchaguzi kama ilivyofanya Comoro.

“Chama kinachotawala nchini Zimbabwe ni rafiki mkubwa wa chama chako Mheshimiwa Waziri Mkuu. Je, serikali itakuwa tayari kupeleka majeshi huko kama mtu hatakubaliana na matokeo?” alihoji Zitto.

Katika majibu yake, Pinda alisema kwa hivi sasa wanasubiri kuona hali ya mambo inavyokwenda nchini Zimbabwe, kwani hadi sasa matokeo ya uchaguzi wa rais bado hayajatangazwa.

“Suala la Zimbabwe halipendezi hata kidogo na ni kitendawili kwa dunia nzima… lakini pia hatuwezi kujiingiza mahali ambapo hatujaombwa kufanya chochote, maana tukijiingiza tunaweza kuulizwa, nani kawaita,” alisema Pinda.

Alisema jambo la msingi ambalo Tanzania inapenda kuona ni matokeo ya uchaguzi yanatangazwa na mshindi anapatikana kulingana na kura alizopigiwa na wananchi. Alisema SADC inakutana kesho na ndiyo kiungo kikubwa cha jambo hilo, na kama itashindwa kulitolea maamuzi, linaweza likapelekwa AU, ambayo ndiyo chombo kikubwa barani Afrika kufanya maamuzi.

Zimbambwe ni miongoni mwa marafiki wakubwa wa Tanzania kihistoria na katika harakati za kudai uhuru, Tanzania iliisaidia sana Zimbabwe kama zilivyo nchi nyingine kusini mwa Afrika.

Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni, nchi hiyo imekabiliwa na matatizo makubwa ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, hasa baada ya Rais wake Robert Mugabe, kuingia katika mgogoro na mataifa makubwa kutokana na sera zake.

Taifa hilo lilifanya uchaguzi wake wiki mbili zilizopita na hadi sasa matokeo yake hayajatangazwa bila kutolewa sababu ya msingi, huku mpinzani mkuu wa rais wa sasa, Morgan Tsvangirai, wa Chama cha MDC, akidai kuwa hizo ni mbinu za kutaka kubadilisha matokeo ambayo yeye ameshajitangaza kuwa mshindi.

Aidha, katika kile kinachoonekana kumpigia debe Waziri Mkuu, muda mfupi baada ya kipindi hicho cha maswali kumalizika, Spika wa Bunge Samuel Sitta, alisema Tanzania imepata kiongozi anayefaa, ambaye ameonyesha kumudu vilivyo nafasi hiyo.

Alisema Mungu anajua kuchagua kiongozi anayefaa kwa taifa la Tanzania, na lazima ijivunie kwa kuwa na aina hiyo ya kiongozi ambaye amepata madaraka muda mfupi uliopita, lakini ameonyesha kuifanya kazi yake hiyo vizuri.

Sifa hizo alimmwagia alipokuwa akifunga kipindi hicho kipya cha maswali na majibu ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, kilichoanzishwa kwa lengo la kuwapa fursa wabunge kupata nafasi ya kuuliza na kujibiwa moja kwa moja kutoka kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

“Kweli Mungu huchagua viongozi wake, na kweli Tanzania tumepata PM (Waziri Mkuu) anayefaa, kwani tumemuona jinsi alivyojibu maswali vizuri katika awamu yake ya kwanza ya kujibu mambo hapo kwa hapo,” alisema Sitta.

Source: Tanzania Daima.
 
Pundit, kwenye hili tatizo siyo kile ambacho Pinda alisema kwani alisema something within his domain (very vague to be honest) lakini gazeti la the Citizen lilimnukuu vibaya kabisa na kimsingi kumfanya aonekane very irresponsible kitu ambacho kilisababisha ofisi ya Waziri Mkuu itaoe maelezo.

Sawa, tuachane na waliomnukuu. Tuangalie moja kwa moja alisema nini bila kupitia dalali wa habari.

... suala la Zimbabwe ni kitendawili si kwa Serikali ya Tanzania lakini ninaweza kusema kwa Afrika yote na ninaweza kusema hata kwa International Community yote, si jambo linalopendeza hata kidogo yaani halipendezi hata kidogo.

...Kwa hiyo, unalolisema ni concern kwa kila mtu sisi wote hapa we are very much concerned lakini aah! mimi nasema ngoja tungoje tuone litakalotokea ni nini.

...(Makofi)... sisi tume play role kubwa sana kwa uhuru wa Zimbabwe aah! sasa tungoje tuone litatokea nini maana mimi sina jibu la harakaharaka kwenye eneo hili hata kidogo. (Makofi)

...mimi nadhani tungoje International Pressure na mimi najua ipo kubwa, tutakapopata a breakthrough na kwa kweli kama ni lazima kupeleka jeshi nasema kama ni lazima AU nina hakika itakaa chini itatazama what to do na kama hapana budi watafanya hivyo. (Makofi)"

Haya, umesema kwamba tatizo sio alichosema Pinda. Halafu hapo hapo ukasema kwa kweli hakuwa baini. Kwa kuanzia, hilo tayari hapo tatizo.

Pili, katika lugha za ki diplomasia ukisema uko concerned manake hukupenda hata kidogo kilicho fanyika. Tayari hilo ni tamko rasmi la msimaomo wa nchi, hususan ukisema 'sisi wote hapa tuko concernced'. Sasa, huwezi kutoa tamko rasmi halafu hapo hapo ukasema tusubiri kwanza. Ndio maana ndugu Pundit akasema Pinda ilibidi aseme hawezi kuongelea jambo hilo, mwisho wa hadithi. Yeye Pundit alisema hii inajulikana katika lugha za kidiplomasia, lakini mimi nasema sio kwenye diplomasia peke yake. Muulize hata mcheza mpira wa shule katika nchi zilizoendelea, nchi zinazojua mambo ya mawasiliano ya hadhara. Muulize: mkiingia fainali mna mpango gani wa kushinda ubingwa? Anakujibu nini? 'Hatujafika - na hatujui kama tutafika - fainali; tunacheza mechi moja moja.' Hujibu vitu vya kufikirika!

Tatu, sijawahi kusikia kiongozi anasema 'tungoje international pressure'. Kwanza hujui kama zitakuja. Pili, yeye kama mmoja wa wasemaji wa Tanzania - nchi inayoongoza AU, iliyoko mbele katika kutatua migogoro Afrika Mashariki na kati- ni moja ya hizo nguvu za international pressure. Hawezi kusema anazingoja. Ni kama vile anafuata upepo. Yani hiki ni kituko!

Nne, Pinda hatakiwi kusema Afrika nzima haijafurahia ya Zimbabwe. Kiufupi, hatakiwi kuongelea wengine.

Mwisho, ulivyosema Pinda 'alisema something within his domain' nadhani hata Pundit hakusema Pinda aliongea nje ya mipaka yake ya kazi. Tena zaidi ya hivyo alichosema Pundit na - nadhani yuko sahihi 100% - ni kwamba watu wengi sana wanaweza kuwa wasemaji wa Serikali (Waziri wa nje, wa Ulinzi, Waziri mkuu, Rais na wasemaji wao wote). Cha msingi ni kwamba mjue siasa yenu ni nini kuhusu jambo fulani ili muweze kushabihiana mnapotoa tamko. Kwa hiyo, hata kama gazeti limemnukuu vibaya , na yeye bado kachemka vibaya vibaya!

Bahati mbaya zaidi, yale makofi na vifijo alivyopewa na wenzake vinasema kitu fulani kuhusu hao wabunge - au nchi nzima - kuliko ubora wa alichosema Pinda!
 
tuko pamoja Mkuu Pundit na Kuhani Mkuu,

.....kuondoa hii migogoro, haw amapolicy makers wetu....mijdala kama hiyo inabidi wawe wana-quote policies husika nakama kuna any msimamo/directives kutoka kwa Mkuu wa nchi au makubaliano ya vikao vikuu...........na siku zote hapa nasema hawa viongozi wetu kama hawana uhakika na jambo wawe wanajifunza kusema....at least NO COMMENT......sio kuanza kubwabwaja
 
Ogah.... right on point.... Tatizo ni kwamba sisi waTanzania (nikiwemo mimi na viongozi) tunafuata le mentality/motto ya FFU, "Act first and reason latter".....ha ha haaa
 
Nilisema nini kuhusu matamko ya Pinda jamani? Angalia alichosema Pinda halafu, endorsement ya Mbeki kwa Mugabe:

... suala la Zimbabwe ni kitendawili si kwa Serikali ya Tanzania lakini ninaweza kusema kwa Afrika yote na ninaweza kusema hata kwa International Community yote, si jambo linalopendeza hata kidogo yaani halipendezi hata kidogo.

...mimi nadhani tungoje International Pressure na mimi najua ipo kubwa, tutakapopata a breakthrough na kwa kweli kama ni lazima kupeleka jeshi nasema kama ni lazima AU nina hakika itakaa chini itatazama what to do na kama hapana budi watafanya hivyo. (Makofi)"

Mbeki says 'no crisis in Zimbabwe' after Mugabe talks
LUSAKA (Agence France-Presse) Sat Apr 12, 7:40 AM ET

…But hopes that leaders might issue a hard-hitting statement and even put pressure on Mugabe to stand down were dealt a blow in the hours before the summit when South Africa's President Thabo Mbeki stopped over in Harare en route to Lusaka.

After his first face-to-face talks with Mugabe since the elections, Mbeki ignored pleas for outside pressure to be levied upon the veteran Zimbabwean leader and demanded that things be allowed to run their course.

"There is no crisis in Zimbabwe," he told journalists. "The body authorised to release the results is the Zimbabwe Electoral Commission, let's wait for them to announce the results."

Mugabe, alongside him, made no mention of the election, but denied he was snubbing the summit, saying, "We are very good friends and very good brothers. Sometimes you attend, sometimes you have other things holding you back."

Southern African leaders have been heavily criticised over their traditional reluctance to speak out against Mugabe, who has ruled Zimbabwe for 28 years and is the oldest leader in the region.
 
Hivi aliyoyasema Pinda yanatosheleza kuwa yalijibu swlai aliloulizwa? hayo aliyoyasema yalitosheleza kuonyesha msimamo wa tanzania, kama nchi iliyo na dhamana ya kuongoza bara la afrika, kuhusiana na zimbabwe?
Pinda anamaanisha nini anaposema tusubiri tuone? yaano wauane kwanza halafu ndio hatua zichukuliwe?
Sia ajabu kuwa amekuwa misquoted kwa sababu nadhani hata yeye mwenyewe amemiss present argument yake
 
Back
Top Bottom