Ofisi ya Rais – TAMISEMI Special Thread: Karibu tukuhudumie, tupe Maoni, Maswali, Mapendekezo na Malalamiko

Ofisi ya Rais – TAMISEMI Special Thread: Karibu tukuhudumie, tupe Maoni, Maswali, Mapendekezo na Malalamiko

OR TAMISEMI

Ministry
Joined
Jul 3, 2024
Posts
20
Reaction score
93
Ndugu wana JamiiForums,

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), kupitia thread hii, tutapokea Maoni, Ushauri, Malalamiko, Mapendekezo yako Mwananchi. Tunakuhakikishia kuchukua hatua stahiki kwa haraka zaidi kwa kile utakachokiwasilisha kwetu.

Ikumbukwe kuwa tangu Mwaka 1961 hadi sasa Ofisi ya Rais –TAMISEMI imekuwa ni Wizara inayojitegemea na madhumuni ya kuwepo kwa Serikali za Mitaa ni kupeleka Madaraka kwa Wananchi ambapo chimbuko lake ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 Sura ya 8, Ibara ya 145 na 146.

Hadi sasa Nchi ina Mikoa 26, Wilaya 139, Halmashauri 184, Tarafa 570, Kata 3,956, Vijiji 12,319, Vitongoji 64,361 pamoja na Mitaa 4,263.

Majukumu ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI
yanatekelezwa katika ngazi ya Makao Makuu, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia Hati ya Rais ya Mgawanyo wa Majukumu (Presidential Instrument) iliyotolewa na Rais Mei 2021, majukumu ya OR-TAMISEMI ni pamoja na:-

i) Kuratibu utekelezaji wa Sera ya Maendeleo Mijini na Vijijini na Upelekaji wa Madaraka kwa Umma (D by D);
ii) Kuratibu huduma mijini kama vile usafirishaji, maji na usafi wa mazingira;
iii) Kusimamia Tume ya Utumishi wa Walimu;
iv) Kuratibu na Kusimamia Tawala za Mikoa ili ziweze kuziwezesha Halmashauri kutekeleza wajibu wake;
v) Kuratibu Usimamizi na Uendeshaji wa Shule za Msingi na Sekondari nchini kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM);
vi) kusimamia na kuratibu shughuli za utolewaji wa huduma za Afya ya Msingi, Ustawi wa Jamii na Lishe
vii) Kuratibu na kusimamia mifumo na miundombinu ya TEHAMA katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi
viii) Kujenga uwezo wa watumishi wa OR-TAMISEMI ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi
ix) Kuratibu shughuli za wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo
x) Kusimamia utendaji wa Mashirika, Taasisi, Programu na miradi iliyo chini ya OR-TAMISEMI

Kupitia JamiiForums.com unaweza kuwasiliana nasi (OR-TAMISEMI) kwa kutuma ujumbe wako kwenye sehemu ya kuweka maoni hapo chini au tutumie kupitia Private Message (PM).

Pia, tunapatikana kupitia:

Instagram @ortamisemi
Twitter @ortamisemitz
Facebook Ofisi ya Rais-Tamisemi
Website www.tamisemi.go.tz
YouTube @ortamisemi
Watssap channel: Ofisi ya Rais - TAMISEMI

Anuani
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
S.l.P 1923 Dodoma - Tanzania,
Telephone: +255 262 321 234
Fax: +255 262 322 116
Email: ps@tamisemi.go.tz
Complain: ps@tamisemi.go.tz

Kituo cha Huduma kwa Mteja
+255 735 160 210 au +255 26 216 0210
Kuanzia saa 1:30 asubuhi mpaka saa 10:30 jioni
 
Malalamiko mfuko wa PSSSF

Kuna shida imejitokeza katika mfuko huu. Kuna watumishi wakidownlod SUMMARY CONTRIBUTION REPORT kupitia PSSSF Portal , kwa kule page ya mwisho kabisa chini unakutana na employer names zaidi ya moja

Kwa mfano, ameajiriwa halmashauri A lakini unakuta kuna halmashauri nyingine kama mbili hivi ambazo haujawahi hata kufanya kazi huko.

Majibu ya wahusika hayaridhishi kwani unaambiwa ni suala la tatizo la kimtandao lakini inaleta ukakasi sana kwani hakuna mabadiliko yoyote ya kuondoa huu utata.

Inawezekana vp employer names katika page ya CONTRIBUTION SUMMARY REPORT kuwe na employer names zaidi ya moja with employer ID ?

KAZI IENDELEE 🇹🇿
 
Wizara ya miradi ya upigaji.
Halafu watumishi wanaohangaika na majukumu huko vijijini ndio wanatumika tena kuisimika vizuri CCM kipindi cha kupiga kura.
Kuna tatizo kubwa sana nchi hii.

Anyway, karibuni.
 
Mimi niulize kitu kimoja kuhusu huu mradi wa DMDP phase 2. tuliona matangazo ya kusaini na fedha zikatoka kwa mkopo tukaambiwa utekelezaji utaanza rasmi mwezi jun 2024 katika wilaya ya ubungo na kibamba lakini hadi sasa ni July na hakuna dalili zozote za mradi huo kuendelea au kuanza je ndugu zangu wa Tamisemi hapa kuna mkwamo gani umetokea au ni vigogo wanataka kupiga hizo fedha zilizotolewa na wafadhili na serikali waje kuzilipa kwa kodi zetu au inakuaje? Ningefarijika sana kama mngenipatia haya majibu.

Nimeambatanisha na screen shot niliyoitoa Instagram mwezi march mwaka huu tarura walipokua wakijibu maswali ya wadau kuhusu mojawapo ya barabara kuanza ujenzi mwezi wa sita ila hadi sasa hakuna hizo dalili
 

Attachments

  • Screenshot_20240326-162256.jpg
    Screenshot_20240326-162256.jpg
    376.2 KB · Views: 54
Karibuni sana jf.....

Likizo za malipo kwa watumishi hivi hii kitu ni kweli ipo au ni kwa baadhi ya kada tu ndio hulipwa... Au ni baadhi ya halmashauri??

Kila mwaka ni kujaza jaza documents kibao, kuandika barua lakini mwaka wa kumi huu mie sijawahi kuona chochote, kama hakunaga haya malipo nashauri tusisumbuliwe.
 
Back
Top Bottom