Ofisi ya Rais – TAMISEMI Special Thread: Karibu tukuhudumie, tupe Maoni, Maswali, Mapendekezo na Malalamiko

Ofisi ya Rais – TAMISEMI Special Thread: Karibu tukuhudumie, tupe Maoni, Maswali, Mapendekezo na Malalamiko

Ndugu wana JamiiForums,

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), kupitia thread hii, tutapokea Maoni, Ushauri, Malalamiko, Mapendekezo yako Mwananchi. Tunakuhakikishia kuchukua hatua stahiki kwa haraka zaidi kwa kile utakachokiwasilisha kwetu.

Ikumbukwe kuwa tangu Mwaka 1961 hadi sasa Ofisi ya Rais –TAMISEMI imekuwa ni Wizara inayojitegemea na madhumuni ya kuwepo kwa Serikali za Mitaa ni kupeleka Madaraka kwa Wananchi ambapo chimbuko lake ni Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 Sura ya 8, Ibara ya 145 na 146.

Hadi sasa Nchi ina Mikoa 26, Wilaya 139, Halmashauri 184, Tarafa 570, Kata 3,956, Vijiji 12,319, Vitongoji 64,361 pamoja na Mitaa 4,263.

Majukumu ya Ofisi ya Rais - TAMISEMI
yanatekelezwa katika ngazi ya Makao Makuu, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia Hati ya Rais ya Mgawanyo wa Majukumu (Presidential Instrument) iliyotolewa na Rais Mei 2021, majukumu ya OR-TAMISEMI ni pamoja na:-

i) Kuratibu utekelezaji wa Sera ya Maendeleo Mijini na Vijijini na Upelekaji wa Madaraka kwa Umma (D by D);
ii) Kuratibu huduma mijini kama vile usafirishaji, maji na usafi wa mazingira;
iii) Kusimamia Tume ya Utumishi wa Walimu;
iv) Kuratibu na Kusimamia Tawala za Mikoa ili ziweze kuziwezesha Halmashauri kutekeleza wajibu wake;
v) Kuratibu Usimamizi na Uendeshaji wa Shule za Msingi na Sekondari nchini kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa (MSM);
vi) kusimamia na kuratibu shughuli za utolewaji wa huduma za Afya ya Msingi, Ustawi wa Jamii na Lishe
vii) Kuratibu na kusimamia mifumo na miundombinu ya TEHAMA katika Ofisi za Wakuu wa Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa na Taasisi
viii) Kujenga uwezo wa watumishi wa OR-TAMISEMI ili watekeleze majukumu yao kwa ufanisi
ix) Kuratibu shughuli za wajasiriamali na wafanyabiashara wadogo
x) Kusimamia utendaji wa Mashirika, Taasisi, Programu na miradi iliyo chini ya OR-TAMISEMI

Kupitia JamiiForums.com unaweza kuwasiliana nasi (OR-TAMISEMI) kwa kutuma ujumbe wako kwenye sehemu ya kuweka maoni hapo chini au tutumie kupitia Private Message (PM).

Pia, tunapatikana kupitia:

Instagram @ortamisemi
Twitter @ortamisemitz
Facebook Ofisi ya Rais-Tamisemi
Website www.tamisemi.go.tz
YouTube @ortamisemi
Watssap channel: Ofisi ya Rais - TAMISEMI

Anuani
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
S.l.P 1923 Dodoma - Tanzania,
Telephone: +255 262 321 234
Fax: +255 262 322 116
Email: ps@tamisemi.go.tz
Complain: ps@tamisemi.go.tz

Kituo cha Huduma kwa Mteja
+255 735 160 210 au +255 26 216 0210
Kuanzia saa 1:30 asubuhi mpaka saa 10:30 jioni
Mradi wa bonde la mto msimbazi unaanza lini!?
 
OR- TAMISEMI mfumo wenu wa TAUSI haupo na uhalisia malalamiko ni mengi lakini hakuna muitikio wowote.Changamoto zilizopo kwenye mfumo wa TAUSI PORTAL;

1.Mfumo wa ufunguaji wa account mpya haufanyi kazi.

2.Kwenye eneo la LAND SALES.Ukiingia kuna muda mfumo unaonyesha viwanja vipo wazi vinarangi ya kijani na kuna muda viwanja hivyo hivyo unakuta vimewekwa rangi nyekundu kuashiri vimeshanuunuliwa.

3.Utaratibu wa kulipia 30% upfront sio rafiki kwakua watu wengi wangependa kuona kwanza sehemu wanayonunua ili kuridhia.Huu utaratibu wa kulipia 30% ya bei ya kiwanja ndio mtu aende halmashauri husika akakione kiwanja unapunguza wateja na kuweka ugumu ikiwa viwanja vitaisha na mtu angependa abadilishiwe eneo.

Mnaweza mkabadili utaratibu kwa kuweka siku za kwenda kutembelea maeneo.Kwa mfano mara mbili kwa mwezi labda Jumamosi mbili kila mwezi katika muda wenu wa GROSS PERIOD.

Njia hii itavuatia watu wengi ambao watafika na kuonana na wataalamu na maafisa ardhi kwa maelezo zaidi na maelekezo ya umiliki wa ardhi katika halmashauri husika.Pia wale wenye changamoto mfano wameshindwa kufungua account na changamoto nyinginezo wangepata usaidizi wa haraka na uhakika kutoka watu husika.

Wahusika mtusaidie maana nimepiga simu mpaka halmashauri husika ila sikupata msaada wa kuridhisha na wakati mwingine simu hazipokelewi.

Mfumo huu ni mzuri kama utakuwa na ufanisi na utasaidia kuondoa vishoka na kuwa na mipango miji mizuri na kupunguza migogoro ya ardhi kwakuwa watu watanunua ardhi sehemu sahihi hivyo ni msaada kwa watu wa hali ya chini.

Pia niwaase muutangaze mfumo ili usiwe unajulikana tu kwa watu wachache.
 
3.Utaratibu wa kulipia 30% upfront sio rafiki kwakua watu wengi wangependa kuona kwanza sehemu wanayonunua ili kuridhia.Huu utaratibu wa kulipia 30% ya bei ya kiwanja ndio mtu aende halmashauri husika akakione kiwanja unapunguza wateja na kuweka ugumu ikiwa viwanja vitaisha na mtu angependa abadilishiwe eneo.
Huo ni utapeli wa kitaasisi uliohalalishwa na serikali.
 
Mfumo huu ni mzuri kama utakuwa na ufanisi na utasaidia kuondoa vishoka
Vishoka wako ndani ya taasisi husika kwa kushirikiana na wataalamu wa mfumo ili kuuchezesha wanapotaka kutekeleza jambo lao.
 
Nilisoma moja ya shule kubwa ya sekondari (yenye form 1 - VI) madasa A,B,C, D kwa kidato
Mwalimu wa phy 1, biology, 1, Chem 2, Hesabu 0 na baadae 1 (wanafundisha hadi wanapata kizunguzungu)
Huku waalimu wa English na Kiswahili wanagombea ili mwalimu asije akasahaulika na kuachwa bila kipindi
LAKINI zikitangazwa ajira utashangaa walio ajiriwa wengi ni wale wale wanaogombea wasikose kipindi.......
Sijui kama na hili linahitaji msaada wa watu wa Marekani ili watusaidie kufikiri ?
 
Nilisoma moja ya shule kubwa ya sekondari (yenye form 1 - vi) madasa A,B,C D kwa kidato
Mwalimu wa phy 1, biology, 1, Chem 2, Hesabu 0 na baadae 1 (wanafundisha hadi wanapata kizunguzungu)
Huku waalimu wa English na Kiswahili wanagombea ili mwalimu asije akasahaulika na kuchwa bila kipindi
LAKINI ikitangazwa ajira utashangaa walio ajiriwa wengi ni wale wale wanaogombea wasikose kipindi.......
Sijui kama na hili linahitaji msaada wa watu wa Marekani ili watusaidie kufikiri ?
🙏🙏🙏
 
Ila tamisemi mnazingua Sana, mna mifumo mingiii ila ufanisi wake niwamashaka, mfano ni ESS, mnachangia mazingira magumu Kwa watumishi walio chini yenu
 
Back
Top Bottom