DOKEZO Ofisi ya Rais Utumishi, TAMISEMI na Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga okoeni mtumishi huyu

DOKEZO Ofisi ya Rais Utumishi, TAMISEMI na Mkurugenzi wa Manispaa ya Sumbawanga okoeni mtumishi huyu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Aende kwa mkuu wa wilaya na amsaidie mara moja na alimalize hili tatizo haraka. Akishindwa kulimaliza ndani ya siku saba nendeni kwa mkuu wa mkoa.

Wakishindwa kulimaliza tatizo hili waambie wote ndani ya siku 30 waanze kutafuta kazi za kufanya.
 
Aende kwa mkuu wa wilaya na amsaidie mara moja na alimalize hili tatizo haraka. Akishindwa kulimaliza ndani ya siku saba nendeni kwa mkuu wa mkoa.

Wakishindwa kulimaliza tatizo hili waambie wote ndani ya siku 30 waanze kutafuta kazi za kufanya.
Tumeona Nyaraka zilizoenda hadi Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na bado hakusaidiwa kabisa. Nyaraka zote kapeleka na zimepokelewa kwa ushahidi wa wazi kabisa.
 
Mbona haujatuambia hiyo ofisi yenu aliyofika ni ipi (ina wadhifa gani).

Anyway, siyo wakurugenzi au maafisa utumishi tu, kwa ujumla Luna baadhi ya watu wanapopata nafasi ya uongozi hujiona miungu watu, na hawa ktk utumishi Tz ni wengi sana na ndiyo maan wengine hufa vifo vya ajabu.

Huyo atoke huko kijijini arudi Sumbawanga mjini apambanie haki yake, ikiwezekana aandike barua kwa waajiri wake ngazi za juu kuhusu sakata hili. Au atafute mwanasheria awapeleke mkurugenzi na huyo afisa utumishi aliyehama mahakamani ili aweze kupata haki yake na stahiki zake zote za nyuma atalipwa.

Au akamuone mwenyekiti wa halmashauri ili suala hilo mkurugenzi akalitolee ufafanuzi kwenye vikao vya madiwani. Nina hakika ataambiwa alishughulikie Mara Mona.
Naona mahakamani ndipo atapata haki yake kwa urahisi amtagute wakili msomi Mh Kibatala
 
Aandike barua kwa katibu mkuu utumishi au Aende pale ajieleze watamwandikia barua mkurugenzi fasta na atajibu ila asiwe na mazongi iwe kweli alifuata utaratibu hapo pana vita hiyo kama ya mama yangu mdogo na mkurugenzi mmoja walipambana mpaka anarudishwa amebakiza miaka 3 kustaafu na sasa tayari kastaafu. Yaan mkuu wa mkoa alishangaa namna mkurugenzi anavyokamaa naye mpaka anakata rufaa ofisi ya raisi asiruhusiwe kurudi.
 
Sishauri Sana akimbilie HQ Dodoma huko anaweza kuishia tu kwa masekretari mapokezi hata ktb Mkuu akamsikia kwenye radio tu. Nashauri yafuatayo: mtafuteni Afisa utumishi mbobezi wa miaka ya kutosha kazini mwenye roho nzuri(wapo japo wachache). Muelezeeni kila kitu halafu pamoja na kushauri cha kufanya amuunganishe na watu wenye utu pale utumishi wamsaidie. Lkn jambo la haraka hapa asifate hiyo njia anayoitumia kutaka kurudi kazini, atafute mwajiri mwingine serikalini aombe nafasi Kama ipo kurudi kazini kwa kueleza nini kilitokea. Itachukua zaidi ya mwaka lkn vyombo Vya usalama vitamshauri ktb Mkuu amrudishe kazini baada ya kujiridhisha kuwa alionewa. Sasa hili hawezi kusimama peke yake lazima awepo MTU wa kumuongoza, serikalini ni kugumu Sana yaani watu kutafsiri haraka nini kinatakiwa kufanyika. Kwa kifupi ni hv
 
Kizazi hiki cha karne ya 21 lazima tusolve problems guys sio kutengeneza matatizo. Mbona hivi lkn.
 
Back
Top Bottom