Ofisi ya Waziri Mkuu yaomba Tsh. Trilioni 12.5 mwaka 2026/2027

Ofisi ya Waziri Mkuu yaomba Tsh. Trilioni 12.5 mwaka 2026/2027

Nchi haiwezi kupunguza umaskini hivi karibuni.

Yaani matumizi ni makubwa zaidi kuliko pesa ya maendeleo.

Kama Taifa kuna namna tunapaswa kufanya.Tatizo sio makusanyo ya kodi tatizo ni matumizi yetu pia.

Tuachane na matumizi ya anasa/yasiyo ya lazima.
 
Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zilizo chini yake imeliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha jumla ya shilingi trilioni 12.5 kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Hayo yameelezwa leo Aprili 1, 2026 na Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba wakati akiwasilisha hotuba ya bajeti ya ofisi yake bungeni jijini Dodoma.

Dkt. Mwigulu amesema kati ya fedha hizo, shilingi trilioni 8.7 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 3.7 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.

Hii nchi ina mambo ya kipumbavu sana. Ina maana hizo bilioni zote ni za kutumbua tu?
 
Back
Top Bottom