Wengi wao wanajua ubunge hawawezi kupata ila target Yao Ni nafasi za uteuzi baada ya kukosa kuteuliwa kuwa mgombea. Watu wanaishi kwa historia maana takwimu zinaonyesha kuwa miaka ya nyuma Waliotia Nia Kisha wakakosa ubunge wamekuwa wakipewa nafasi za uteuzi. Na hii ndo point kubwa hivyo hayo mafuriko yasikupe tabu. Over to you.
Watakuwa wamekosea. Teuzi nyingi zilifanywa kimkakati ili kuondoa waliokuwa wa JK ili JPM aanze na timu yake. Teuzi hizo nyingi bado zimejazwa, labda waombee walio katika nafasi hizo waende kinyume na matakwa ya JPM hasa katika uchaguzi huu.
Kinachosikitisha ni idadi ya watia nia kuzidi hata idadi ya nafasi kwa ujumla wake. Ubunge imekuwa ni chanzo cha kipato. Professions zimekuwa nyuma!