PostGE2025 Ofisi za CHADEMA Makao Makuu zimezingirwa na Polisi muda huu

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
52,828
Reaction score
165,667
Huu hapa chini ndio ujumbe alioutoa Hilder Newton kupitia Mtandao wa X:

Muda huu Jeshi la Polisi limezingira ofisi ya Makao Makuu ya CHADEMA Mikocheni, watu hawaruhusiwi kuingia wala kutoka.

Ikumbukwe asubuhi hii chama kilikuwa kinatarajia kuzungumza na Waandishi wa Habari.

Screenshot 2026-05-21 at 11-07-13 Hilda Newton (@HildaNewton21) _ X.png

CH1.jpg

CH2.jpg

CH3.jpg
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, Amani Golugwa amesema msaidizi wa Tundu Lissu, David Jumbe, ‘ametekwa’ na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Alhamisi, Mei 21, 2026 nyumbani kwake Mabwepande, Bunju jijini Dar es Salaam huku yeye mwenyewe akihojiwa na Jeshi la Polisi.

Akizungumza na Mwananchi leo Mei 21, 2026 kabla ya Jeshi la Polisi kuzingira ofisi za Chadema Mikocheni jijini Dar es Salaam kufanya mahojiano na Golugwa, amesema taarifa zinazosambaa mitandaoni ni za kweli.

“Hizi ni taarifa za kweli na tutaongea na waandishi wa habari muda si mrefu,” amesema Golugwa.

Mwananchi limefika Chadema asubuhi ya leo ambapo kumeitishwa mkutano na waandishi wa habari uliopangwa kufanyika saa 3:00 asubuhi kuzungumzia tukio la ‘kutekwa’ kwa David, lakini mkutano huo umechelewa kuanza.

Mkutano huo umeshindikana kuanza kwa wakati kutokana na kile kilichoelezwa na Mkuu wa Idara ya Habari wa Kurugenzi ya Habari na Uenezi ya Chadema, Gervas Lyenda kuwa Golugwa anahojiwa.

Lyenda amesema wamechelewa kuanza mkutano na waandishi wa habari kutokana na kiongozi wao huyo kuzuiliwa na Jeshi la Polisi, ambalo linaendelea kufanya mahojiano naye ndani ya ofisi za Chadema Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Mwananchi imeshuhudia magari manne ya askari wa Jeshi la Polisi yakiwa pembezoni mwa ofisi za Chadema huku baadhi wakifanya doria wakiwa na silaha za moto.
Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa mtandaoni kuanzia usiku wa kuamkia leo Mei 21, 2026, David anadaiwa kuchukuliwa nyumbani kwake Mabwepande, Bunju jijini Dar es Salaam.
 
Huu hapa chini ndio ujumbe alioutoa Hilder Newton kupitia Mtandao wa X:

Muda huu Jeshi la Polisi limezingira ofisi ya Makao Makuu ya CHADEMA Mikocheni, watu hawaruhusiwi kuingia wala kutoka.

Ikumbukwe asubuhi hii chama kilikuwa kinatarajia kuzungumza na Waandishi wa Habari.
Hiki chombo so called police tz needs reform au kifutwe kabisa
 
Ina maana jeshi la polisi linawazuia Chadema wasitoe taarifa kuhusu kutekwa kwa mlinzi wa Lissu nyumbani kwake.

Kwa hali hii tukisema wao ndio wahusika au wanawajua wahusika wa utekaji tutakuwa tumekosea?

Nyakati kama hizi ndio zakuitumia ile nyomi ya kwenye mikutano ya hadhara, heshima ingerudi haraka sana, hao polisi wangekumbuka wao ni walinzi wa watanganyika sio walinzi wa watawala.

Wanatuchezea makusudi kwasababu wanajua hatutawafanya chochote.
 
Kwa udikteta huu ni bora mara 100 kipindi cha Magufuli.
Rais Samia ameweka recoding ya muuwaji namba moja tangu nchi ipate uhuru

Record yake ni ya Afrika nzima. Hata hao mnaosikia walikuwa madikteta, hawakuwahi kufanya mauaji makubwa ya kiwango hicho! Huyu ni muuji wa kipekee ambaye amegeuza vyombo vilivyostahili kuwa vyombo vya usalama wa wananchi kuwa vyomba vya kuwaua wananchi!
Hii imethibitika kuwa mwanamke akiwezeshwa kuwa dikteta anaweza kuwazidi waliomwezesha.
 
Rudieni tena, naona kitima yuko kimya sasa hivi,kuna Kono lenye manyoya linamnyemelea nini?
 
Kwa udikteta huu ni bora mara 100 kipindi cha Magufuli.
Rais Samia ameweka recoding ya muuwaji namba moja tangu nchi ipate uhuru
BORA MAGUFULI ALIVYOFUNGA KABISA SHUGHULI ZA KISIASA KABISA UPO SAHIHI.
 
Huu hapa chini ndio ujumbe alioutoa Hilder Newton kupitia Mtandao wa X:

Muda huu Jeshi la Polisi limezingira ofisi ya Makao Makuu ya CHADEMA Mikocheni, watu hawaruhusiwi kuingia wala kutoka.

Ikumbukwe asubuhi hii chama kilikuwa kinatarajia kuzungumza na Waandishi wa Habari.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Bara, Amani Golugwa amesema msaidizi wa Tundu Lissu, David Jumbe, ‘ametekwa’ na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo Alhamisi, Mei 21, 2026 nyumbani kwake Mabwepande, Bunju jijini Dar es Salaam huku yeye mwenyewe akihojiwa na Jeshi la Polisi.

Akizungumza na Mwananchi leo Mei 21, 2026 kabla ya Jeshi la Polisi kuzingira ofisi za Chadema Mikocheni jijini Dar es Salaam kufanya mahojiano na Golugwa, amesema taarifa zinazosambaa mitandaoni ni za kweli.

“Hizi ni taarifa za kweli na tutaongea na waandishi wa habari muda si mrefu,” amesema Golugwa.

Mwananchi limefika Chadema asubuhi ya leo ambapo kumeitishwa mkutano na waandishi wa habari uliopangwa kufanyika saa 3:00 asubuhi kuzungumzia tukio la ‘kutekwa’ kwa David, lakini mkutano huo umechelewa kuanza.

Mkutano huo umeshindikana kuanza kwa wakati kutokana na kile kilichoelezwa na Mkuu wa Idara ya Habari wa Kurugenzi ya Habari na Uenezi ya Chadema, Gervas Lyenda kuwa Golugwa anahojiwa.

Lyenda amesema wamechelewa kuanza mkutano na waandishi wa habari kutokana na kiongozi wao huyo kuzuiliwa na Jeshi la Polisi, ambalo linaendelea kufanya mahojiano naye ndani ya ofisi za Chadema Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Mwananchi imeshuhudia magari manne ya askari wa Jeshi la Polisi yakiwa pembezoni mwa ofisi za Chadema huku baadhi wakifanya doria wakiwa na silaha za moto.
Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa mtandaoni kuanzia usiku wa kuamkia leo Mei 21, 2026, David anadaiwa kuchukuliwa nyumbani kwake Mabwepande, Bunju jijini Dar es Salaam.
Kikwete ni bora sasa amashauri Samia kuwa hizi njia hazifai kwa Tanzania.Tanzania ilikuwa nchi ya mfano sisi wote wapenda haki na Amani hata kama sio wafuasi wa Chadema hayatufurahishi haiwezekani nchi moja wengine waishi kama waarikwa hilo linaondoa furaha,linaleta chuki na Sura yetu inachafuka duniani
 
Lakini mda mwingne hata wabongo ntasema sisi ni wajinga wa mwisho kweli hali tunaijua ilivyo wanakuja askari hata hawafiki kumi wanamchukua mtu na watu wapo wanaangalia badala waanzishe timbwili kieleweke inabaki ni kulalamika mitandaoni. Wakenya mungu awabariki maana wanapigania haki yao wao wenyewe.
Kuna msimu wa dagaa zilikosa kenya tukawa tunasafirisha tukifka miji ilizo mpakani tunafaulisha na pkpk za kenya unapewa chako unaenda. Siku moja maaskari wakenya na bongo wakaungana kuja kukamata hao dagaa mbona waliona cha mtema kuni. Afande alikuwa anapgwa hadi bunduki inakuwa nzito wakaitisha back up hiyo backup hata haikufika sehemu ya tukio coz walirudishwa na wananchi wabongo wakarudisha mapolis wa bongo na wakenya wakarudisha wao siku nzima wanaulizwa mboga mnazikamata za nini na aliyedai kaibiwa hao dagaa ajitokeze. Siku hyo maafande walijifungia kwa majirani ikawa pona pona yao coz mtu au mnyama akiingia kwa mji wa mtu sababu ya usalama huyo anaachwa. Sasa na sisi tukishkana tutawashida hao watu.
 
Kitu cha kwanza kufanywa na Chadema baada ya kutwaa Nchi kwa njia Yeyote ni kulivunja jeshi la polisi n.a. kukamata viongozi
wake haraka sana
 
Kwa udikteta huu ni bora mara 100 kipindi cha Magufuli.
Rais Samia ameweka recoding ya muuwaji namba moja tangu nchi ipate uhuru
Haya ni matokeo ya idictetor wa magufuli. Mpumbavu wewe
 
Mtaani kwetu huwezi kuja na gari upaki sehemu hata kama unasubiria demu wako maeneo hayo shusha vioo ka utoke ndan ya gari na usipak zaid ya dk 10 my friend juz wabeba magendo wamepak sehem wakawa ni kutoka wanaleki ilibdi watu wawazibie na matrekta wakajieleza ikawa pona yao. Wanaokuja kuteka mtu kwanza lazma wawahi seiem husika wasome mazingira. Shituken mkiona magari au watu wageni mtaani kwenu na wataogopa. Zamani mtu kukamatwa ilikuwa lazma wapitie kwa mjumbe au mwenyekiti ndo waende kwa mtuhumiwa wajieleze ndo watoke na wewe. Lakin siku hizi ambush and hijack. Tanzania tuamkeni.
Tulindane sisi kwa sisi.
Tujuane sisi kwa sisi.
Tujaliane sisi kwa sisi.
Tanzania amkeni,amkeni kumekucha.
 
Wakiitwa jeshi la polisi la ccm wanakasirika wakati matendo yao yana mwelekeo huo.
 
Back
Top Bottom