Ofisi za Maprofesa na Madaktari wa UDSM zinathibitisha namna Taifa lilivyofeli. Je, hata majumbani kwao wanaishi kwa dhiki hivi?

Uprofesa siku hizi hauna maana yoyote. Maprofesa wengi ni wajinga na wapumbavu. Pia walishasema hapo ni jalalani so ni haki yake kuwa na ofisi ambazo ziko hivyo
 
Tume iundwe ya kuchunguza ubovu wa vyoo ikiongozwa na Profesa mwenzao Taletale na Dr Mwaka?
 

Acha kutusi nyumbani kwenu, huko ni kutojua mambo mengi kwanini hali iko hivyo, ww kwenu au ulikozaliwa kijijini au sehemu yoyote ya Tz kukoje? Huruma na busara za kuona hali mbaya mahali badala ya kuumia moyo au kusikitika kimya kimya, ww unawasimanga au kuwang'ong'a hivi, I hate to say this, you are such a freaking shithole.
 
Bado kama taifa hatujawa tayari kuliangalia kwa umakini unaohitajika suala la elimu, tunadonoa donoa tu. Huyu anaongelea ofisi za maprofesa, huyu anaongelea madawati, huyu anaongelea vishikwambi kwa walimu, huyu anaongelea ranking za shule. Tunarukaruka tu kama tumerukwa akili.
 
Inasikitisha sana nchi hii,
Nimekuwa nikipita kwenye geti kuu la kuingilia Mbuga ya Wanyama Nyerere upande wa Mloka, kusema kweli ni aibu,

Sielewi hata hao watalii huwa wanatufikilia nini sisi Watanzania, Reception ni hovyo, hakuna hata computer, wafanyakazi wana lugha mbaya na za kukera, hujafanya kiss lolote wenyewe ni kufoka foka tu, eneo ni chafu hakuna mvuto wowote,

Mpaka unajiuliza hawa watu hawajawahi hata kwenda mbuga za wenzetu kujifunza kitu.

Ni aibu
 
Pia tembelea parking ya Utawala uone V8 za maboss wao zilivyopark pale zinapumua utadhani ni mawakala wa TOYOTA.
 
Ni issue ya mentality wala siyo pesa.
 
Hawapelekwi kujifunza Kwa Wenzetu.
Zikitokea Safari wanakwenda Wapumbavu Kupiga picha na kutafuta like kwenye FB.
Hiyo Ipo kila Idara.
Wahifadhi wote wanepita JKT mafunzo ya Kijeshi . Na Je mafunzo ya Kijeshi kule JKT na kwingineko yanaendana na mahitaji za jamii na kimataifa ?

CCM imefikia mwisho Kwa uwezo wa Mungu pekee mana imeliharibu Taifa hili lililokuwa limeasisiwa na mwalimu Nyerere Kwa uzalendo mkubwa.

Enzi za mwalimu haiwezi kupata kazi kwenye hifadhi za wanyama kama hujasoma Chuo Cha Mweka International Wildlife College.
Chuo kilikua kinatoa wasomi wa kiwango Cha kimataifa.
Leo sijui JKT , sijui SUA , sijui wapi wanafundishwa kikatilikatili na mazingira ya kukwamishana TU Hali inayowafanya kuwa na roho mbaya na kuwaza pesa TU. Ndio maana siku hizi hata wakimwona kuku wa kienyeji kwenye hifadhi wanaweza wakampiga risasi na kumkamata mmiliki .
 
Kila mwaka bajeti za ukarabati wa majengo na ofisi .
Pesa zinatengwa.
Wapumbavu na wahuni wanagawana pale pale Chuoni ,jioni wanakaa kwenye baa na kulewa pombe na kama Kuna mwanafunzi wa Ke mwenze makalio makubwa lakini akili ndogo basi pesa inazobaki itatumika kulipia gest . Ukarabati utafanyika mwakani kwani fungu kimekwisha .

CAG akifika anawaonea aibu maprofesa na hata wakibainika kuwa wamechezea pesa za umma hatua haichukuliwi mana wasomi ni miungu watu waliwafundisha wezi wa Mali za umma ambao ni miungu kamili.

Kila sekta na Idara imejaa majizi yanayolindwa na waliopaswa kuwafukuza na kuajiri watanzania wenye wito halisi wa kuwatumikia na kuwapa Elimu Bora watanzania.

Ukitaka ujue Nini wasomi wanawaza basi fualitia mazungumzo yao wakikutana na kampani zao za starehe.
Mwafrika katika nchi zetu hizi Akishapata PhD na basi hashughulishi Tena Kichwa chake zaidi ya kutafuta madili yenye pesa za kula Bata.Angakau wale wa za amani kama akina Shivji na wengine wenye above 65 years.

Dubai imeendelea Kwa sababu ya kupata Kiongozi sahihi wa kusimamia mwelekeo wa nchi.
Serikali ya wahuni haiwezi kudhibiti uhuni na wahuni .
Sio kweli kuwa Chuo kikuu kinashindwa kukarabati ofisi za malecturer . Kuna shule za secondary private zenye maofisi mazuri kama ofisi ya meneja wa Benki.
Watumishi wengi hawajali kulinda hata fungu la usafi wa mazingira. Hawawezi vibarua wa usafi matokeo yake ni mazingira mabovu.
 

Mkuu umeandika kwa uchungu sana
 
Hivi udsm bado Wana WiFi??
Nashangaa Sana kuona chuo wanafunzi wanatumia bundle la kampuni za simu...tunatia aibu
Pale kuna V8 tu hayo mambo ya Wi-Fi waachie GRANO CAFFE (restaurant @ Mlimani City). AIBUUUU
 
Umeandika vizuri. Ni shida kuona mtu anashindwa kuyaweka mazingira yake ya kazi yawe mazuri. Wasomi wameshindwa katika hilo hapa nchini.
 
Hivi wewe umewahi kuingia ofisi za wakusanya ushuru huku wilayani, utadhani wao sio wakusanya ushuru hata pazia hawana.
Aisee nenda kwenye ofisi za watendaji wa vijiji ambao ndio wadau wakubwa wa kukusanya Kodi, achana na ofisi nenda vyooni wallah hata kichaa hawezi kujisaidia huko
 
pesa yenyewe ya R&D hamna unategemea serikali ndio iwaboreshee ofisi.
sasa apewe ofisi nzuri nawakati hata serikali yenyewe haijawekeza cha kutosha katika R&D
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…