Ogende ogaruke na Shuntama

Ogende ogaruke na Shuntama

Nasikia wabongo walioko Bongo na hata majuu wanasafiri hadi Nigeria eti kutafuta dawa ya mapenzi!! maana wanaona penzi limepungua!
Tena kuna Kabila fulani kule Congo (Zaire) kuna jamaa yangu wa Congo alikuwa ananiambia eti akienda kule akipewa chakula hawezi kula (akiamini kwamba akila chakula tu anaweza kulishwa kitu na kujikuta anasahau kwao)...
 
Kama huamini nenda Kenya kwa Wakamba wakuonyeshe "KAMUTEE" inavyofanyakazi
Ningependa kuamini sababu Elimu haina Mwisho ndio maana naomba mwanajamii mmoja anieleweshe vizuri na kama uwezekano upo tuweze kupata ingredient ili tuwape wanandoa ambao hawajatulia lakini shida ya hii kitu utawezaje kuhakikisha kwamba kweli ndio imefanya kazi..?
 
Ningependa kuamini sababu Elimu haina Mwisho ndio maana naomba mwanajamii mmoja anieleweshe vizuri na kama uwezekano upo tuweze kupata ingredient ili tuwape wanandoa ambao hawajatulia lakini shida ya hii kitu utawezaje kuhakikisha kwamba kweli ndio imefanya kazi..?
Kha! Wewe unataka kuwapa wanandoa? Huwa unatoa ushauri kwao na unaona hawaelewi? Kamutee inafanyakazi nimeshuhudia
 
Kha! Wewe unataka kuwapa wanandoa? Huwa unatoa ushauri kwao na unaona hawaelewi? Kamutee inafanyakazi nimeshuhudia
Vipi unaweza ukaniongezea Data kidogo kwa sisi kina Tomaso..., na unajua Ingredients zake..., Kama ni kweli kwanini nisiwape wanandoa au hata mimi mwenyewe kujaribu na mwenza wangu pia..., huoni kwamba hii itasaidia matatizo mengi.? Je ina madhara yoyote?
 
Mie siamini kabisa kama kuna dawa ya mapenzi. Ila naamini kwamba unaweza kumpenda mtu kupitiliza na hii inasababishwa na vitu mbali mbali kama vile jinsi anavyokujali, kukuheshimu, kukuonyesha mapenzi ya hali ya juu kila siku iendayo kwa Mungu n.k. Wale wasiaomini kwamba unaweza kumpenda mtu kupitiliza hadi uwe umerogwa sijui tuwaite vipi labda ndio wale wanaosema nampenda fulani kwa 55% au 60% sijui asilimia nyingine wanamuachia nani. Nasikia wabongo walioko Bongo na hata majuu wanasafiri hadi Nigeria eti kutafuta dawa ya mapenzi!! maana wanaona penzi limepungua!



Why not using part of that money to revive the love!
 
Kama huamini nenda kwa wahaya ulizia shuntama au mnyoshe utapewa lkn madhara yake utajuta kwa nini ulimpa, mi binafsi siwezi kumpa mme wangu kwani nitakuwa na raha gani kumfanya mwenzagu zezeta na je ndugu zake watanionaje
 
kama huamini nenda kwa wahaya ulizia shuntama au mnyoshe utapewa lkn madhara yake utajuta kwa nini ulimpa, mi binafsi siwezi kumpa mme wangu kwani nitakuwa na raha gani kumfanya mwenzagu zezeta na je ndugu zake watanionaje
Kwahiyo hii haina kiwango..., ukimpa tu mtu anakuwa zezeta??, basi hii sio dawa ya mapenzi ni dawa ya kuwa kichaa 🙂
 
Wote wanaopenda kupita kiasi ni asilimia ndogo sana wamepewa dawa,wengi wana maradhi ya utegemezi wa hisia,watu wengi wana njaa ya kupendwa halafu wao wenyewe hawajui kupenda nini!
 
Wote wanaopenda kupita kiasi ni asilimia ndogo sana wamepewa dawa,wengi wana maradhi ya utegemezi wa hisia,watu wengi wana njaa ya kupendwa halafu wao wenyewe hawajui kupenda nini!
Kwahiyo hii dawa ipo? Wewe umeshashuhudia?
 
Kwahiyo hii dawa ipo??, wewe umeshashuhudia?
Dawa zipo, ambacho hujakiona au kushuhudia haina maana hakipo! Nikikuuliza kwanini unaamini dunia ni duara wakati hujaiona kwa macho? Umeoneshwa picha tu na ukaamini!
 
Dawa zipo,ambacho hujakiona au kushuhudia haina maana hakipo!Nikikuuliza kwanini unaamini dunia ni duara wakati hujaiona kwa macho?Umeoneshwa picha tu na ukaamini!
Naamini dunia ni Duara sababu ya usiku na mchana; pia sababu ukitembea kuelekea mbele utajikuta umerudi ulipotoka pia kuna satellite images; Sasa kuhusu hizi dawa yaani kitu ukila au kupewa kikufanye umpende mtu usiyempenda ??

Anyway Mkuu hapa nimetoa mada ili tubadilishane mawazo kwahiyo chochote ambacho wenzangu mnakifahamu naomba tujuzane
 
Huu mtanange ni mkali zaidi ya shubiri...tupendane sisi kwa sisi na miili yenu iwe chakula chenu nyote,msinyimane maana kwa kufanya hivyo mtakuwa mmepunguza upendo wa Mungu kwenu (parable statement)

Tatizo hatutafakari maneno tuliyofundishwa kwa kina,hatutaki kuumiza vichwa kutafakari badala yake tunakuwa lax,tunapoteza mda mwingi kusikiliza miziki,kwenda baa,club,kufanya vitu ambavyo havihitaji kufikiria sana ila kama tungetulia tukatafakari statement kama hiyo hapo juu naamini tusingekuwa tunakosa upendo kati yetu...

Dunia imetuweka bize sana ili tukose mda wa kutosha kutafakari na finally the more you gain the more you loose,dawa zote ni belief na dawa zina kikomo ndo maana hata hospital watu wanaendelea kufa
 
Haya yote yanatokana na kutokumwamini Mungu Biblia inasema Bwana asipoijenga nyumba wajengao wafanya kazi bure na Bwana asipoilinda nyumba walindao wakesha bure.

So utaenda kutafuta dawa kumlinda mpenzi wako kwanza unaenda kwa binadamu mwenzako kumwomba msaada pili unapewa masharti ukikikuka tuu unaweza kujuliamu maisha yako yote.

Upendo natural from God ndio wa kweli huo wakutafuta kwa dawa kuna siku dawa hazitafanya kazi utalia kilio cha mbwa mwizi SO LETS PRAY TO GOD TO GIVE US TRUE LOVE.
 
Dawa ya mapenzi mganga anayetoa ni wewe mwenyewe.
Utakimbilia kwa waganga uambiwe upeleke ushuzi wa simba ushindwe.
True stor: kuna mdada alienda kwa mganga ili mumewe atulie, mganga akamwambia apeleke nyoya la simba. Dada wa watu akaanza vitrip vya dar zoo akalitafute nyoya. Kahangaika sana hadi kutoa hela ili wafanyakazi wa mule wamchomoe simba nyoya. Mwisho wa siku akafanikiwa. Akampelekea mganga mganga akamuuliza hili nyoya umelichomoa mwenyewe mdada akasema ndio,... Mganga akamwambia we dada ni jasiri sana, yaani simba na ukali wote huo umeweza kumtuliza hadi ukachomoa nyoya lake unashndwa kumtuliza mumeo?! Haya rudi nyumbani katumie mbinu kama ulizotumia kupata unyoya kumtuliza mumeo.
 
Kwetu Bukoba kuna kilainishi Cha nafsi kinaitwa shuntama, upewa Mtu anayetakiwa asichomoke Kwenye mahusiano. Sina uelewa WA Ndani sana kuhusu namna inavyofanya kazi ila hii chakula inasifika sana.

Katika jukwaa kama Ili tunaweza tumia shuntama kama kichokoza mada kufahamu mengi kuhusu asili ya limbwata na nnjia wanazotumia watu kuliswa na namna yakuzikwepa.

Vijana mkipata Shule hii mtakwepa kula vitu vichafu au kupenda kimizimu badala yakupenda Kwa hiari.

Tushuntame
 
Back
Top Bottom