Ogopa kupata nuksi au nyota yako kushuka

Ogopa kupata nuksi au nyota yako kushuka

mr Future

Member
Joined
Jan 26, 2019
Posts
69
Reaction score
84
Habari za muda huu wana JF! Leo nazungumzia jinsi navyopitia mapito,

Kwanza nianze kwa kusema mimi mr future naamini uchawi upo kwa 100%

Ilianza kama utani kila jambo jema lilianguka katika mzunguko wa maisha yangu, nilipoona mambo hayaendi niliamua kutumia chumvi ambapo nilijifunza matumizi yake humu humu kipitia threads za Mshana Jr , ilikuwa 2019 nilipata ahueni kidogo, lakini hivi sasa nahisi mambo magumi mikosi imeniandana, lakini nikawa nachukulia poa, lakin nikajikuta Nimeachika kwenye mahusiano yote, nikashangaa nikitembea nakutana na vichaa wanaanza kunipigia kelele bila woga dah, nikaanza kufatilia dailil nikagundua ni nuksi tu.

Siku hizi kila nalopanga linaanza vema likifikia kwenye touch line, linafel roho inakuwa inasonona kila mwanamke naye mfata anachomoa nikasema labda vigezo ila nizidi kuona mazigaz hata salamu sikumbukwi na ndugu hata marafiki, nikaanza kutumia kuna formula za madawa ya kutoa nuksi lakin hola

Moja ya formula alitoa bwana rakims lakin nikafatilia maelezo yake huwa hayako vzuri so nashindwa kuelewa vizuri, miez kadhaa ilopita nikatumia mafuta fulani ya kuondoa nuksi si haba yalinisaidia kdgo lakin nilpoacha tu gundu ikarudi,

Lengo la kuandika thread hii ni kutaka msaada najua wapo wengi humu kama mimi

Anayejua formula ya kuchanganya madawa ya kisheria au mafuta yaliyo somewa kusomo karibu tusaidiane

NB: Hata simu nimeazima nispojib comment mtanisamehe,

Wafatao nimefatilia thread zao wana jua haya mambo
cc:
Mshana Jr
Rakims
MZIZI MKAVU
Pasco mayalla


Karibu
 
Nakumbuka ilikuwa ni siku ya kuadhimisha misa ya marehemu wote(all souls day, 2 November), padri aliyesalisha siku hiyo alitupatia neno.

Wakati fulani akiwa paroko parokia moja aliwahi kufuatwa na kijana ambaye alikuwa anajiona ana mikosi na nuksi zote.
Kijana huyo alimwambia baba padri kuwa alikuwa akifanya kila jambo halifanikiwi. Hata alikuwa akipata kazi baada ya muda mfupi tu atafukuzwa au ataacha tu yeye mwenyewe kwa uzembe wake.

Basi baba padri katika kumuhoji akagundua kuwa kijana yule katika malezi yake alilewa na mama yake mzazi pekee lakini alikuwa ameshatangulia mbele ya haki.

Basi baba padri akamshauri kijana akaombe misa kwa ajili ya marehemu mama yake mzazi na pia afunge na kusali novena ya siku 9.

Basi yule kijana alikuja kumtafuta baba padri miaka ya baadae na kutoa shukrani zake. Kwa ufupi ni kuwa apokea baraka zake.
 
nikwel hayo yapo, na omba yasikukute ukiwa hujawai kupamban na changamoto za kimaisha ama hujakomaab ktk kupambana na hayo mambo.

..unafika wakati ndugu wanakusahau,
..marafik wanakuwa hawaelewek(hawakuelew)
..mahusiano kuyumba, kila unaempata hamdumu, na mkidumu basi migogoro kila kukicha
..maisha kuyumba, ugumu kuongozeka, kazin kukosa mvuto ama kuchukiwa bila sabbu
..watoto& baazi ya wanyama kukuogopa bila sabbu
...kuota ndoto za aina moja ama zinazojirudia rudia mfano , kuota ndoto za kurudi shule, kukimbizwa, kupanda vilima/miinuko, kupambana na nyoka ama wanyama

haya ni baazi ya mambo yanaweza kuonesha maisha yako hayapo vzr spiritual, na sabbu zake zipo nying
[emoji117]kulogwa
[emoji117]kudhurumu mali za watu, ambapo vilio vyao na vinyongo vyao hukuletea nuksi
[emoji117]ushawai kwenda kwa mganga na ukapewa dawa ya mvuto, na huenda dawa iyo ikawa outdated(kuisha nguvu)
[emoji117]kufanya uzinifu na wanawake tofaut tofaut hasa wenye vifungo
[emoji117]mahal unapoishi(nje ya eneo la kipawa chako&mvuto wako), jina unalotumia(urithi wa mtu), watu unaoshirikiana nao(wana vifungo&wana husda&hamuendan kiutafutaji), mahala unapolala(kuna vifungo vya kishirikina), kaz unayoifanya(nje ya kipawa chako)

sasa ili kujua unajitibuje jarbu kusolve haya mambo niliyoandika, achana na waganga aisee watakupotezea muda wako, japo wapo wanaosaidia kwel ama kukupoteza kweli kweli, dawa ya matatizo yako ni kuchunguza asili ya tatizo lako kwanza, acha kubeti maisha yako kwa kutumia kila dawa kisa umesikia inaponya, tafuta dawa ya tatizo lako[emoji117] chunguza muenendo na matukio ya ndoto uotazo na znazokunyima usingiz(kujirudia) then fanya maamuzi
 
1
 
2

 
3
 
4
 
Back
Top Bottom