Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
Ogopa mambo haya matatu!
Anaandika, Robert Heriel.
Yawezakana kuna mambo yanakuogopesha sana katika maisha yako. Lakini lazima uelewe kuwa yapo mambo makuu unayopaswa kuyaogopa Sana, tena Sana!
Mambo hayo ni:
1. Dhambi
2. Umasikini
3. Ujinga
1. Dhambi/Uovu/ uhalifu
Katika maisha yako ogopa kitu inaitwa dhambi/Uovu/ Uasi Kwa Mungu wako.
Unajua Kwa nini? Kwa sababu;
i. Dhambi inaaibisha.
Wakati unaifanya dhambi inakupofusha macho. Unakuwa Kama kipofu. Unaweza hata Kufanya Mapenzi vichakani, unaweza kubaka, unaweza kuwa mshirikina na mchawi ukavua nguo.
Unakuwa Shoga unapumuliwa unaaibika na kuabisha wazazi na watoto wako. Ila ukifumaniwa hapo ndipo utajua dhambi ni mbaya.
ii. Dhambi inaua.
Ogopa dhambi Kwa sababu ndio chanzo pekee cha uhakika cha kifo chako. Ili Binadamu afe kabla ya wakati wake basi itampasa afanye dhambi au mtu Fulani amtendee dhambi.
iii. Dhambi inakufanya utese wengine bila huruma.
Unaiba pesa za umma bila kujali huku raia wanakufa bila madawa. Unakuwa jambazi na kutoa roho za watu. Unazini unamtesa mkeo/mumeo.
Dhambi inakufanya usiwe na huruma na wengine.
iv. Dhambi inaleta umasikini.
v. Dhambi inaleta magonjwa, vita, na njaa.
2. Umasikini
Baada ya Dhambi ogopa umasikini. Sababu zinaingiliana.
Umasikini unaaibisha, unatesa, unaua, unadhalilisha, unashusha utu wako. Ogopa umasikini Kwa nguvu zote.
3. Ujinga
Hili ni jambo la mwisho. Ogopa ujinga, ujinga unadhuru, unaua, unakufanya ufanye dhambi, unakufanya uwe masikini, ujinga unakufanya uwe mtumwa.
Hivyo ogopa watu hawa na waepuke,
1. Waovu
2. Masikini
3. Wajinga
Hao kaa nao mbali, makundi hayo ukae nayo kwa tahadhari sana. Ni hatari kuliko hatari yenyewe.
Taikon leo sina mengi.
Robert Heriel,
Taikon wa Fasihi,
Kwa sasa Dar es salaam.