Ogopa Teknolojia: Nimeweka mkataba wa bandari kwenye Chat-GPT, Imejibu kwamba bandari zitakuwa za DP World Milele!

R-K-O

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2023
Posts
482
Reaction score
2,178
Kwa wale ambao hamuijui Chat GPT, hii ni teknolojia ya Artificial Intelligence (Akili Bandia),

Kumekuwa na vuta nikuvute ya huu mkataba, wapo wanaosema mkataba huu ni halali wakiongozwa na spika wa bunge Tulia Ackson na msemaji Gerson Msigwa... Upande wa pili ndio hawa wanaofanya ishu itrend kila kona ya nchi kwamba mkataba huu unapiga nchi mnada.

Nikaona nipandishe mkataba huu kwenye mtambo wa chat gpt.

Nikaiuliza swali - makubalioano haya yanaweza kuzipora bandari za Tanzania milele.

Jibu ndilo hilo kama lilivyo kwenye picha,

Huu mkataba unamwezesha mwarabu kuichukua bandari milele, Tukitaka kuuvunja hatuwezi upande moja, DP World akiamua anaweza kuiendesha bandari milele!!



Nikaiuliza, kuna kifungu kinavunja mkataba 23(1) kukiwa na "permanent cessation" hii ina maana gani, ikanijibu kwamba ni mpaka pale DP world atakapoamua kuacha shughuli zake, Ni mpaka yeye atakapoamua.

Nikauliza kama inaweza kuwa baada ya miaka elf 1, ikajibu kwamba inaweza kuwa milele "indefinetely"




Inasikitisha sana kuona mpaka robots wanaukataa huu mkataba ulivyo wa hovyo, lakini ajabu viongozi wetu baadhi maprofesa wanajiaibisha kwamba kila kitu kiko sawa, Aibu tupu!

Ushauri wangu: mkataba uwe na kikomo cha muda, Mfano majirani wetu Zanzibar bandari yao hivi karibuni wamesaini mkataba wa miaka mitano na kampuni ya "The Africa Global Logistics - AGL", Sisi huku kwetu Tanzania Bara kwanini mkataba wetu hauna kikomo cha muda ? nachopendekeza mkataba uwe na muda wa kikomo, kwa sasa hao hao DP world wanaweza kuonekana waaminifu lakini hakuna aijuae kesho, wanaweza kuja kutukomoa huko mbele na hatuna cha kuwafanya, hii sio sawa kwa watoto na wajukuu zetu kuja kuumia kwenye jambo ambalo linaweza kurekebishwa ndani ya siku 1 tu bungeni.

kampuni iliyopita ya TICTS iliyosimamia bandari kwa miaka 22 ilikuwa na uwezo mdogo na madudu mengi haifai hata kidogo, suluhisho imebidi ije kampuni yenye ufanisi zaidi lakini hakuna sababu hata moja ya kujishusha kiasi hiki, Ni sawa na kwenda kwa mganga ukiwa na hali ya kawaida kiuchumi unataka pesa zaidi unapuuzia masharti lakini ukipata pesa unaanza kuona masharti ni magumu, unatamani kurudi hali ya zamani uwe huru lakini ndio hivyo tena huwezi.
 
CCM tunawambia mkataba niwakitapeli niwabishi
 
Sijui kwa nini madamu spika na usomi wake kwa sasa namuona kama kiazi. Yaani potato na I can't help it .nikimuona akili inachora potato
 
Sijui kwa nini madamu spika na usomi wake kwa sasa namuona kama kiazi. Yaani potato na I can't help it .nikimuona akili inachora potato
Herding behavior is an occurrence of thoughtful people suspending their individual reasoning because of fear, (amygdala), in this case fearing leaders or in favor of group objective, (CCM)
 
Safi sana hiyo, kwani wewe utakuwepo milele?


Bandari za babu yako ziko wapi?
 
Mbona hujamwekea chatgpt article 5:4?
 
Uvivu ht kusoma.
Nna uhakiki hakuna jipya.
Endeleeni tu vithread vyenu keyboard worriers
 
Nilikuwa nakuona mtu wa maana sasa vp utaamini akili bandia wakati akili zetu original tunazo.
 
Wacha uongo wewe kifungu cha 5:4 mbona hakipo hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…