Wandugu,
Sehemu ingine hatari sana kupigwa panga ni Makuti- Iko Stend Mabasi Msamvu Morogoro. Kwa vile wengi wanaoend apale ni wasafiri basi wahudumu hupiga panga la nguvu na hata management wanafahamu. Nilienda Moro- tulikuwa tunarudi Dar- basi tulikuwa watu wanne- tukapitia asb kupata supu. Bili tuliyoambiwa na kijana mmoja wa Kichaga.. Supu ya Mbuzi 3000, Redbull 3000, Maji 500, Mtori 2000.. nk. Basi tukalipa kama 24,000 jumla na kuondoka.
Bahati nzuri\mbaya nikapata dharura kuwepo tena Moro siku ile- nikaahirisha safari. Nikarudi kwa lunch Makuti. Nakaagiza mchemsho wa samaki nikaambiwa na kijana yule yule samaki wameadimika hivyo ni 7,000. Wakaleta samaki nikalipa. Bahati mbaya samaki hakuwa mzuri... nikamrudisha.
Basi meneja akaja kuniuliza kulikoni nimerurisha samaki? na nimeshalipa? Nikasema 7,000 nimelipa tayari. Basi akasema samaki 5,000!
Nikauliza bei zingine.. mtori 1000, Supu 1500, Redbull 2000.
Nikapiga mahesabu nikagundua yule muhudumu alikata panga la 8,000 kwetu tu tangu asb!
Nikacharuka.. basi meneja akanirudishia 8,000 ananiomba yaishe kwa kuwa yule kijana alishakimbia! Basi nilikuwa na haraka ya kazi sikuweza kufuatilia zaidi.
Ukweli ni kuwa wizi\ufisadi upo katika kila nyanja...na wengi wetu tunaibiwa bila kufahamu!
High time kuwa makina zaidi- ila Makuti-Msamvu Stend ya Moro mabasi kwa kupigwa panga hapa ni hatari zaidi!
Kuna wateja wengine wanne nao walilalamikia huu wizi!