Okra Magic ameondoka Simba akiwa wa Moto mno. Sema alipigwa Zengwe la Ulevi

Mkuu kwa kiwango cha Chama, Chama hawezi kwenda kucheza mpira Yanga. Yanga ni timu inayotumia nguvu na kasi ktk uchezaji wake, kitu ambacho Chama hakiwezi kwa namna yoyote ile. Mbaya zaidi nafasi yake kuna mafundi wawili, Azizi Ki na Pacome, ni mwehu tu ndo anayeweza kuthubutu kumpa namba Chama Yanga mbele ya hawa mafundi, hapa kumbuka Maxi hatumzungumzii.

Mashabiki wa Simba embu kuna mda kubalini na kile ambacho watu na taaluma nao wanachokifanya. Si chini ya makocha 3 au 4 wa kigeni wakionesha nia ya kutofurahishwa na uchezaji wa Chama, Chama amekuwa overrated na ninyi mashabiki ila kiuhalisia kwa wabobezi wa Soka wanamuona ni average player.
 
Wanasemaga eti Bocco ndio anawapiga ndumba wenzie..
Saido umri umeenda, sasa uchawi gani hapo kusema anarogwa? Yaani Boko awaroge wenzie halafu yeye asicheze mpira?
 
Leo mkuu umezungumza bila mahaba, kwa kweli mashabiki wa Yanga tutegemee yoyote yale kutoka kwa Okrah, kubadili tabia ni kitu kigumu saana.
 
Yanga siyo chuo cha upadri,uchungaji au ushehe hadi kupangia namna ya wafanyakazi wake matumizi ya hela yao acha kijana aje afurahie maokoto yake
 
Hoja yako imeegemea kwenye hadithi za kusadikika, Hoja ya kusema mkude achezi sababu ya ulevi ni hoja dhaifu isipokuwa na mashiko, wachezaji wangapi awachezi pale yanga na wenyewe ni walevi?
Nimekupa option zaidi ya mbili kuonesha kwanini Mkude hachezi

Lakini nimekuuliza swali nini sababu ya nyie kumsajili Mkude?

Mlimsajili huku mkijua ana kipaji na hivyo ataisaidia timu au mlimsajili kwa lengo la kuikomoa Simba?

Kama lengo lilikuwa ni uwezo wake, kwanini hachezi? Na akicheza ni dakika chache?

Unaweza kuniambia mchezaji gani mwenye uwezo mzuri ambaye anacheza mechi chache na kwenye hizo mechi ni dakika chache anazotumia, bila ya kuwa na matatizo yeyote ya kinidhamu nje ya uwanja?

Yani mchezaji awe fit, awe na nidhamu, awe na kipaji halafu ukawa unaona hata kwenye sub hayupo, unaweza kunitajia mkoja wa mfano?
 
Umejibu vizuri, labda pombe za Ghana hazileweshi kama za Dar, na huyo Mkude wamemtumia weee, badala waachane nae kwa amani bado wanampakazia mabaya kwa mwajiri wake mpya. Hawa Makolo bwana.
Mkude kuwa na tabia mbaya haijifichi hata kidogo. Timu zinavumilia vipaji na kifunika Tabia ya mchezaji ila ikizidi wanakuondoa. EL-Haji Diof alikuwa na kipaji kikubwa tangu AFCON mpaka kuvhukuliwa na Liverpool. Lakini alipozidisha ukorofi hawakumvumilia.
 
Phiri kutocheza ni ili kumpisha Saidoo mwenye mkataba unaomnufaisha Jaribu Tena. Kuhusu tabia mbovu za Okrah akiwa Simba linajulikanà na hakusingiziwa sijui unataka uthibitisho gani. Ninachosisitiza ni kama Yanga wamepata mwarobaini wa Tabia zake basi kipaji chake kitawabeba. Lakini pia binadamu tunapokosea tunatakiwa kujirekebisha. Inawezekana amegundua madhaifu yake na kuyaacha.
 
Asomae na afahamu.
 
Kila mahali kunakua na siasa zake.


Kwenye michezo, dini, siasa, biashara n.k n.k.

Binadamu wana mambo mengi mno mahali popote penye kipato, hapajawahi kuwa na amani. Haijawahi tokea.
Umepiga kwenye mzinga.
 
Yanga bado inasumbuliwa na pengo la Mayele, huyu Okra ameonesha kiwango kizuri cha ufungaji nadhani target mojawapo ni kwenye Ligi ya mabingwa hizo mechi zinahitaji wafungaji.
 
Tatizo ni menejimenti ya mchongo tu.
Hata Morrison alikuwa na tabia mbovu zaidi akiwa Simba tu,ila alivyoenda yanga alidhibitiwa.Huyo Mkude tumekaa naye muda wote sasa ndio tunajua alikuwa mlevi? Huko yanga hakuna pombe?
 
Saido alikuwa na utovu mwingi wa nidhamu, achana na hata hayo ya kambini, kuna wakati alifunga goli afu anatoka uwanjani hata bila ya maelekezo ya kocha.

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Okra ni chambo cha kumleta yule mshambuliaji wa medeama.
 
Hapo juu umesema aliondoka kambini ila hakutoa sababu za kufanya hivyo, sasa hii sababu umeitoa wapi?

Sent from my SM-A6050 using JamiiForums mobile app
 
Wala sio bo
Wanasemaga eti Bocco ndio anawapiga ndumba wenzie..
[/QUOTE

Sio boko bana. Banda alikuwa hapangwi kabisa. Na kila akiingia anaonesha uwezo. Uwezo wa banda ni mkubwa mara nne ya msonda aumzize
 
Mfumo wa kocha sasa ni kuwa na strong first 11. Sio wachezaji wawili kila namba. Hivyo mfumo haumpi nafasi sio mkude tu. Ata akina Musonda, Kibwana, Nkane na wengi tu.
 
Kwani mkude simba
Tatizo nyie Simba Wanga sana, hapa tunazungumzia hizo kashfa mnazowatupia wakiondoka Simba. Na hapo tatizo wakija Yanga. Yanga hachezi kakutana na Maprofesa wa Mpira tofauti na alikotoka.
Kwan mkude simba alikuwa anacheza?..
 
Huo mfano wa DIOF wala sio sahihi,
Kwani mkude simba
Kwan mkude simba alikuwa anacheza?..
Alikuwa analewa
 
Mfumo wa kocha sasa ni kuwa na strong first 11. Sio wachezaji wawili kila namba. Hivyo mfumo haumpi nafasi sio mkude tu. Ata akina Musonda, Kibwana, Nkane na wengi tu.
Maana yake hapo lazima tukubaliane kuwa Mkude hana uwezo wa kuwa beat hao 11 ili awe miongoni mwa strong 11

Na ndio maana linapokuja swala la ubora katika namba yake, yeye hapati nafasi
 
Acha kutunga maneno fala we, lini Mayele alitoroka kambi. KmlaMMko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…