Okra Magic ameondoka Simba akiwa wa Moto mno. Sema alipigwa Zengwe la Ulevi

Okra Magic ameondoka Simba akiwa wa Moto mno. Sema alipigwa Zengwe la Ulevi

Saido umri umeenda, sasa uchawi gani hapo kusema anarogwa? Yaani Boko awaroge wenzie halafu yeye asicheze mpira?
saido kaja juzi tu hilo swala la Bow cow ni la mda mreeefu..

Yeye na T.O pale langoni ndio zao hizo kubqli katqq
 
Mkuu kwa kiwango cha Chama, Chama hawezi kwenda kucheza mpira Yanga. Yanga ni timu inayotumia nguvu na kasi ktk uchezaji wake, kitu ambacho Chama hakiwezi kwa namna yoyote ile. Mbaya zaidi nafasi yake kuna mafundi wawili, Azizi Ki na Pacome, ni mwehu tu ndo anayeweza kuthubutu kumpa namba Chama Yanga mbele ya hawa mafundi, hapa kumbuka Maxi hatumzungumzii.

Mashabiki wa Simba embu kuna mda kubalini na kile ambacho watu na taaluma nao wanachokifanya. Si chini ya makocha 3 au 4 wa kigeni wakionesha nia ya kutofurahishwa na uchezaji wa Chama, Chama amekuwa overrated na ninyi mashabiki ila kiuhalisia kwa wabobezi wa Soka wanamuona ni average player.
Mpira kimbiza kimbiza ni wa kizamani. Haukupi uhakika wa matokeo. Ulichezwa sana na waarabu. Ila waalgeria mliwakimbizia wakawabutua 3-0. Al ahly pia mkaponea kwa uwezo binafsi wa pakome tena home. Mbiombio Leo unashinda tano kesho bila bahasha unagongwa. Angalia arsenal na unawachosha wachezaji sana.

Turudi huyo max anafanyaje kimataifa hapo yanga. Mpira unakimbiza kama ni shambulizi la kushitukiza tu.
Rudi kwa chama. Msimu jana tu ndie aliyefunga na kuasist zaidi pale Simba.
Msimu huu ametoa asist ya uhakika sana dhidi ya Al Ahly na ndio aliyeikoa Simba sana. Usijaribu sana kumfananisha pakome na aziz ki na chama. Wako na performance sababu wapinzani hawajawawekea mipango. Sawa na Onana tu. Chama anakuwa na perfomance nzuri kwa misimu 5 mfululizo kimataifa.

Sio makocha hawamtaki ila Viongozi tu.
 
Nje ya uwanja inaweza kuwa hivyo. Ila ndani ya uwanja sikuona kabisa mapungufu yake.

Wakati mwingine kumudu wachezaji kunaitaji management nzuri. Vip nabi Aliamua kumchukua morson kutoka simba Akiwa mkorofi. Na leo kaenda nae MOROCO.

Unaweza ukatumia ubora wake tu na udhaifu wake ukamwachia. Kama una wanasaikolojia wazuri matatizo mengi ya kitabia hutibika.
Ilikuaje Morison akaachwa akiwa kwenye kiwango Bora kabisa tena akifunga goal muhim zidi ya marumo gallants? Sometimes washabiki hatujui yaliyondani ya club,niheri kupunguza ujuwaji
 
Wanasemaga eti Bocco ndio anawapiga ndumba wenzie..

Umeniwahi Kaka…
Daaa Jangwani Hakuna Uchawi kaka ni juhudi zako tuu!
Ukisikika kwa wazee yaani wazee wakinusa kuwa kuna Mchezaji anawaloga wenzie amekwisha…
Watani wetu wa Jangwani wako Seriously mnoo na Soka[emoji91][emoji91]
 
Hivi ingetokea Simba wamemrudisha Okrah watu mngetafsiri vipi kitendo hicho?

Failure au success?

Jamaa ni talented ila Ishu kubwa ni nidhamu, msimu kama huu wa Mapinduzi Cup ndio msimu ambao Dejane alitimka.

Na sababu kubwa ilikuwa ni ugomvi kati yake na Okrah ambapo Okrah alikuwa ndiye mkorofi, na Dejane alitaka kuona management inamchukulia hatua.

Lakini alipoona management inataka kumaliza hilo jambo kwa mazungumzo kwa kuwapatanisha ndio hapo Dejane akaona Club haina misimamo bora asepe.

Okrah ana tuhuma za ulevi kupitiliza na akilewa anakuwa mgomvi na hata kama umefuatiia kwenye pages zake hivi karibuni amekuwa akipost wazi wazi akiwa anakula tungi

Okrah alishawahi kumpiga refa, hii level ya utukutu hata Morrison hajawahi kuifikia.

Akirudi Yanga atakutana na Mkude mlevi mwenzie ambaye ndio taita wa viwanja hapa mjini

Naamini Yanga imeona hayo yote na kujua namna ya kuweza kudili naye.

Ila binafsi siamini sana kwenye mabadiliko ya kitabia yatayo mfurahisha kocha pamoja na uongozi, labda kupunguza

Ok,
Kama nakuelewa…
Kama kweli ni Suala ka nidhamu na Sio Kulogwa na wachezaji wenzake Pale Msimbazi basi Hatofanikiwa huko alipoenda.
Ila Kama alikuwa anarogwa asifanyw vema,
Basi atafanikiwa sana.
 
Back
Top Bottom