Oktoba 29 ni mashindano kati ya Reality vs Ahadi Hewa! Je, Watanzania Watachagua nini kati ya Visible, Tangible Deliverables vs Empty Promises?

Oktoba 29 ni mashindano kati ya Reality vs Ahadi Hewa! Je, Watanzania Watachagua nini kati ya Visible, Tangible Deliverables vs Empty Promises?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
59,804
Reaction score
134,593
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, hutoa zile makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa", Watanzania tunajiandaa kwa Uchaguzi Mkuu wa rais, wabunge na madiwani hapo Oktoba 29, Watanzania tunakwenda kuingia kwenye uchaguzi uchaguzi wa 2025 ambao ni uchaguzi wa mashindano kati ya tangible visible deliverables ambayo ni maendeleo ya kweli ya vitu vya ukweli vya kuonekanika ambavyo vimefanyika na kuwa ni tangible, visible deliverables vs ahadi hewa, empty promises kuwa ukinichagua mimi nitafanya hiki na kile!. Ahadi ikitolewa usually huwa ni empty promise, ikiisha tekelezwa ndio inakuwa ahadi ya ukweli, a firm commitment.

Hili ni bandiko la swali, hiyo October 29, Je Watanzania watachagua nini kati ya tangible visible deliverables za kuonekanika, na empty promises za kuahidiwa, with nothing to show?

Declaration of Interest
Kwa vile JF ni members generated forum, ukitokea kuna jambo unalijua, unalibandika humu ili kushare na wengine. Naomba ku declare interest kuwa mimi ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM, na humu tuna makada wengi wa vyama vyote. Enzi zile Prof. Kitila Mkumbo akiwa very active humu alikuwa ni kada wa Chadema. Zitto Kabwe akiwa Chadema alikuwa very active humu japo bado yuko yupo is sio very active kivile baada ya kuwa kada wa ACT, hivyo unaweza kuwa ni kada wa chama na bado ukawa ni mchambuzi mzuri, very objective bila kupendelea chama chako hivyo naomba ulisome bandiko hili kwa kusoma hoja zangu za ukweli na sio kuniangalia ukada wangu@

Kumhusu Samia na Uchaguzi wa 2025, Nilisema Zamani Kuwa
Tarehe 29/10/2015 kuna mengi nimeandika humu kuhusu utendaji wa serikali ya awamu ya 6.

Japo sikuunga mkono kile kilichofanyika Dodoma kwenye kupata wagombea wa CCM kwa hoja za msingi kabisa, mgombea akiisha pitishwa na chama chako, unakwenda nae.

Kuna kitu naomba nikiseme, Je wajua kuwa kupitishwa na vikao vya uteuzi vya CCM ni kazi ngumu kuliko hata uchaguzi wenyewe?. Je wajua kuwa jina lako likiishapitishwa na CCM, huo tayari ni ushindi tosha?. Ili CCM kupata ushindi wa kishindo, katika uchaguzi huu, hakuhitaji hata kupiga kampeni, kazi aliyoifanya Samia inaonekana wazi kabisa kwa naked eyes, wala huhitaji kuvaa miwani ya uchunguzi ndipo uone, wenye macho wanaona!

Tunakwenda Kuchagua Nini
Watanzania tunakwenda kuingia kwenye uchaguzi huku kuna chama kimoja kinaingia kikiwa na mtaji mkubwa wa vitu ilivyofanya katika utekelezaji wa ilani yake ya uchaguzi iliyokipatia ushindi ile 2020, kikiwa na mtaji wa vitu vya kuonekanika, a strong showcase, huku vyama vingine vikija with nothing to show case, ukitegemea Watanzania watachagua visible tangible deliverables or just empty promises?.

Ushauri wa Bure
Kwavile tunaingia kwenye mashindano kati ya mwenye kitu cha kuonyesha na asiye na kitu cha kuonyesha, ili kuwatendea haki Watanzania waweze kufanya an informed decision hiyo October 29 natoa wito kwa asiyenacho, ili aweze kuchaguliwa, asije tuu na ahadi bali aonyeshe hiki kilichopo sii lolote sii chochote, ningekuwa mimi ningefanya hiki na hiki na hiki.

Mfano mzuri ni kwenye elimu bure, inatolewa toka darasa la kwanza hadi kidato cha 6. Kwa vile wewe ulisema ungekuwa wewe ungetoa elimu bure toka chekechea hadi chuo kikuu, then unaeleza ungeitoaje kwa bajeti gani, ili Watanzania wakuchague wewe.

Uchaguzi Mkuu huu, tushindanishe sera na mikakati ya utekelezaji na sio kushindana kwa kutukana na kubeza kila kilichofanyika bali kueleza namna bora zaidi ya kufanya kuliko hiki kilichofanyika.

Mfano Samia amekamilisha daraja la Kigongo Busisi, then wewe ahidi kwamba utajenga daraja la Dar Zanzibar!.
Hapa naweka vitu 10 vya Samia
1. Kakamilisha Ikulu ya Dodoma na kuhamia rasmi makao makuu ya nchi kule Dodoma
2. Kukamilisha reli SGR
3. Kukamilisha Mwalimu Nyerere Hydro electric power project
4. Kukamilisha Daraja la Kigongo-Busisi
5. Kukamilisha daraja la Tanzanite
6. Kapanua barabara kutoka Ubungo kwenda Kibaha
7. Kaimarisha miundombinu ya jiji la Dar es Salaam
8. Kuongeza mi ndege na kuimarisha Shirika letu la ndege
9. Aliimarisha ugatuzi
10. Alifungua ofisi zaidi za ubalozi nje ya nchi
Mambo aliyoyafanya kwa nchi hii ni mengi.

Nikiweka yote Samia aliyoyafanya. Kiukweli kabisa kuna mtu wa kumshindanisha nae, au kuna chama cha kushindana na CCM?.

Tuwe Wakweli, Tuwe na Shukrani
It's good to appreciate kilichopo, kilichofanyika na kueleza wewe ungefanya namna bora zaidi ili Watanzania wakikuchagua, wajue wanakuchagua ili kupata kilicho bora.

Hitimisho
Namalizia kwa lile swali la msingi la bandiko hili hiyo October 29, Je Watanzania watachagua nini kati ya visible tangible deliverables za kuonekanika, au empty promises za kuahidiwa, with nothing to show?.

Nawatakia Jumapili Njema.

Jumatano tujitokeze kwa wingi kwenda kufanya kweli.

Paskali
 
Du! hili gazeti la P ndio lina Comment moja tu!

Anyways P mbona hata kauteuzi hukupata baada ya 29 pamoja na kuwa chawa
 
Back
Top Bottom