Binti wa zamani
Platinum Member
- Nov 19, 2011
- 15,052
- 36,866
Nina changamoto ya kiafya kwahiyo leo natulia zangu nyumbani siendi kokote. Kila la kheri kwa wote mtakaoshiriki na kutuwakilisha.
Kwa wenzangu mliobakia majumbani:
TAFADHALI: Ukiona kitu au habari ambayo sie tulio majumbani inabidi isitupite kuhusu yanayoendelea huko nje, tunaomba utushirikishe kupitia huu uzi.
Kwa wenzangu mliobakia majumbani:
- Nini kimesababisha ushindwe kutoka kwako au kwenu na kutumia haki yako ya kikatiba?
- Unafuatilia updates na yanayojiri kupitia akaunti au channels gani huko mtandaoni na wengine tuangalie?
- Leo hapo nyumbani mnapena raha na mpenzi au umepumzika mwenyewe au na familia?
- Swali la kizushi: ukiambiwa uchague kiongozi mmoja aliyepita aondolewe kwenye historia ya viongozi wa Tanzania, utamtoa nani?
- Kwa sababu leo tuna muda; una kitu au vitu ambavyo unavijua na unaweza kunifundisha mimi na wengine?
TAFADHALI: Ukiona kitu au habari ambayo sie tulio majumbani inabidi isitupite kuhusu yanayoendelea huko nje, tunaomba utushirikishe kupitia huu uzi.