Okwi aomba radhi Msimbazi, aapa kufa na Singida United

Okwi aomba radhi Msimbazi, aapa kufa na Singida United

Taarifa nilizonyapianyapia na za motomoto ni kwamba mshambuliaji wa kimataifa Mganda Emmanuel Arnold Okwi ameomba radhi kwa kocha na viongozi wa simba pamoja na mashabiki huku akidhamiria kumaliza ukame wa magoli unaokumba klabu hiyo kwa sasa.

Okwi ambaye ameungana na kikosi hicho juzi akitokea nchini Uganda ambapo mara kadhaa kocha wa Simba Msoud Djuma amekuwa akimshutumu kwa kushindwa kusaidia klabu yake hasa katika michuano ya kombe la mapinduzi iliyofanyika visiwani Zanzibar.

Katika hatua nyingine kikosi cha Simba leo kinarejea jijini Dar Es salaam kutoka huko Morogoro tayari kwa pambano lake litakalofanyika hapo kesho tarehe 18/01/2018 kwenye uwanja wa Taifa.



Tumeshamsamehe mkuu
 
Bwigane hunifurahisha sana akitangaza bao la Okwi.....Okwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii baada ya dakika 2 ndio anasema gooooooooooooooool
 
Back
Top Bottom