Bwana Mapesa
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 2,551
- 1,777
Taarifa nilizonyapianyapia na za motomoto ni kwamba mshambuliaji wa kimataifa Mganda Emmanuel Arnold Okwi ameomba radhi kwa kocha na viongozi wa simba pamoja na mashabiki huku akidhamiria kumaliza ukame wa magoli unaokumba klabu hiyo kwa sasa.
Okwi ambaye ameungana na kikosi hicho juzi akitokea nchini Uganda ambapo mara kadhaa kocha wa Simba Msoud Djuma amekuwa akimshutumu kwa kushindwa kusaidia klabu yake hasa katika michuano ya kombe la mapinduzi iliyofanyika visiwani Zanzibar.
Katika hatua nyingine kikosi cha Simba leo kinarejea jijini Dar Es salaam kutoka huko Morogoro tayari kwa pambano lake litakalofanyika hapo kesho tarehe 18/01/2018 kwenye uwanja wa Taifa.
Tumeshamsamehe mkuu