Ole Gunnar Solskjær afukuzwa, Manchester United watoa tamko rasmi

Cannabis

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2014
Posts
11,557
Reaction score
33,535

Inasemekana bodi ya klabu ya Manchester United imeridhia maamuzi ya kumfukuza kazi Ole Gunnar Solskjær. Maamuzi hayo yanakuja kutokana na muenendo usioridhisha katika msimu wa mwaka 2021/22. Hatua hiyo imechukuliwa baada ya klabu hiyo kupokea kichapo cha magoli 4 kwa 1 dhidi ya Watford. Inasemekana ndani ya muda wowote klabu hiyo itatoa tamko rasmi na kuwataja Michael Carrick na Darren Fletcher kama makocha wa muda mpaka klabu itakapotangaza kocha mpya.

====
Imethibitishwa, Manchester United yamfukuza Ole Gunnar Solskjær.


RASMI: MAN. UTD YAMFUKUZA SOLSKJAER

Baada ya Mkutano wa dharura wa Bodi ya timu hiyo kukaa jana kutokana na mlolongo wa matokeo mabovu, klabu imeachana na Ole Gunnar Solskjaer

Solskjaer alichaguliwa kuinoa timu hiyo Desemba 2018 baada ya Jose Mourinho kufutwa kazi
 
Endelea kuota
 
Ila sasa hata hao wanaobaki kama Caretaker Coaches pia ni wale wale wao ndio wamechangia msiba huu wa sasa.

Ni sawa tu na Magufuli kufa kisha anarithiwa na (Chief Hangaya) halafu inaonekana mabadiliko yamefanyika kumbe ni kutoa gongo kwenye chupa na kumimina kwenye glasi.
 
Wamlete Leonaldo jardim huenda ikawa suluhisho!
 
Tangu mchana kumekiwaa na tetesi za kitimuliwa Kwa Kocha wa Man U.
Hivi kina ukweli wowote!
Ila Uncle Ole aana bahati sana!
 
Hajafukuzwa Bali wamefikia makubaliano ya yeye kutokuendelea kuifundisha team

Tetesi zilizopo Ni carrick au fletcher kuendelea kuifundisha team

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tangu mchana kumekiwaa na tetesi za kitimuliwa Kwa Kocha wa Man U.
Hivi kina ukweli wowote!
Ila Uncle Ole aana bahati sana!
Kafukuzwa tangu saa 8:14 leo mchana 21/11/2021.

Na Michael Carrick ambaye ni Kocha msaidizi ndiye atayebakia hapo OT akiendelea kuifundisha Man Utd ikiwa bado Bodi kuu ya usajili inatafuta Kocha wa kazi ya kudumu kuajiriwa upya kuchukua nafasi ya Ole Guna Sosha Super Sub.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…