Linguistic
JF-Expert Member
- Mar 16, 2021
- 3,669
- 8,268
DRC imeingia kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki. Imekuja na vitu vifuatavyo:-.
1. Imekuja na Population ya Watu Milioni 92. Idadi hii ya watu itaifanya Jumuiya yetu sasa kuwa na Population ya watu milioni 289. Congo pekee inachangia zaidi ya Robo ya Population yote ya EAC. Inaingiza Asilimia 31% ya population yote.
2. Congo imekuja na ukubwa wa Eneo KM za Mraba 2,345,000 na kuifanya Jumuiya kuwa na eneo la KM za Mraba 4,809,992. Congo pekee inaingiza asilimia 48% ya Eneo lote la EAC.
3. Imekuja na Deposit ya Madini ya Kutosha mengi kuliko ya nchi yoyote kwenye Jumuiya hii.
4. Imekuja na Ardhi yenye Rutuba ya kutosha na ambayo mvua hunyeesha kwa kiwango kikubwa kabisa.
Mambo makubwa yanayoitesa Congo ni mawili.
1. Haina Bandari hutegemea Mombasa na Daresalam kuingiza mizigo yao Congo.
2. Vita za hapa na Pale za kisiasa zimeathiri sana Shughuli za Kiuchumi DRC.
𝙺𝙴𝙽𝚈𝙰 𝚆𝙰𝙼𝙴𝚂𝙷𝙰𝙲𝙷𝚄𝙽𝙶𝚄𝙻𝙸𝙰 𝙳𝙸𝙻𝙸
Kwa Afrika Mashariki, Kenya ni mojawapo ya Taifa ambalo limewekeza kwenye Economic intelligence, tayari kikosi kazi cha Kenya kimeshafika Congo na Kuchambua Fursa zilizopo pale..
Kwenye ripoti yao wameonyesha mambo kadhaa mojawapo ni kwamba imebainika kuwa DRC asilimia 4% tu ya watu wote milion 92 ndio wenye bank account. Bank ya Kenya KCB wameweka mkazo mkubwa sana hapa na tayari wapo Congo kwa ajili ya Mission maalumu. KCB imeambatana na makampuni mengine mawili ya kibiashara ambayo ni Jubilee kampuni la bima na Jambo Net.
Ripoti hiyo pia imeonyesha kuwa Congo inatoa asilimia 70% ya madini yote ya Cobalt Duniani ambayo ndio msingi wa Utengenezaji wa mabetri ya Simu, laptop na kadhalika. Kwa kufahamu hilo tu Kenya wameanza Mpango wa kuja na kiwanda cha Magari yanayotumia Umeme kitakachojengwa DRC.
Ripoti hiyo pia inataja madini ya Copper kuwa Congo pekee inatoa asilimia 50 ya madini yote Duniani hivyo bado wanaendelea kuchakata ni kwa namna gani watatumia fursa hiyo ndani ya East Africa.
Ripoti hiyo pia inataja fursa za mazao ya Misitu, Kilimo, na Ufugaji ambayo Kenya wanazifanyia kazi ya kiuchambuzi zaidi kuona watanufaikaje.
𝙽𝙸𝙽𝙸 𝚃𝙰𝙽𝚉𝙰𝙽𝙸𝙰 𝙸𝙺𝙸𝙵𝙰𝙽𝚈𝙴.
Nimejiuliza sana ila hatupo aggressive sana kwenye mambo ya maana. Mijadala ya Watanzania wengi ni ya mambo rahisi sana kuanzia huku chini hadi juu.
Kwenye East Africa Tanzania ilikuwa giant kwenye mambo mawili. Moja tukikuwa na eneo kubwa kuliko nchi nyingine na tulikuwa na rasilimali nyingi kuliko nchi nyingine.
Nimeangalia Biashara kati ya Congo na Kenya, Uganda, Nikagundua Tanzania bado hatujawekeza sana huko Congo.
Dalili za Congo kuingia EAC zilishaonekana muda Mrefu. Kwa kufahamu hivyo Kenya Rais wake alikwenda Huko mapema mwaka huu kuweka kusaini mikataba kibao. Nitaileta hapa baadaye.
Ole Mushi
071702602