Ole Mushi: Watanzania tumejipangaje kuipokea Congo kwenye EAC?

Haa haaa umekataa wakenya hawaweki kiwanda!
 
Tanzania imewekeza kwa kumpokea Kinana kwenye chama
 
Wazo zuri sana, viongozi wetu wanatakiwa kuliona hili na kuwahamasisha wananchi,. Unatakiwa mpango wa kitaifa na sio kuachia kila mwanchi kupambana kivyake.
tumepanga kuupiga mewing kwenye maria space
 

tanzania tunapeleka ccm watu wapate kadi za chama kirahisi zaidi
 
Ndio
 
Na huko Congo DRC [emoji1078] kwenyewe kunayo barabara ya kuendeshea hayo magari ya Umeme?

Achilia mbali changamoto ya Umeme wenyewe?

Tukkija kwenye suala la usalama. Wa mwekezaji Congo [emoji1078], bado ni changamoto pia.

Labda Lubumbashi na Kinshasa ndio hilo linawezekana.
Lakini sehemu zingine kama Goma,Kalemie,Kisangani,
Uvira nk bado usalama ni changamoto.

Fursa zipo ila unahitaji Bunduki zaidi kuliko Akili na hapo ujuwe ni unapambana na USA [emoji631], Rwanda [emoji1206].China [emoji630].

Na viongozi wakubwa wakubwa wa serikali yao wenyewe akiwemo Mstaafu Kabila anayemiliki kampuni mojawapo ya ndege.
Kagame anayemiliki mtandao wa simu za mkononi na wanyarwanda wengineo lukuki waliojichimbia kwenye uwekezaji mkubwa ndani ya DRC.
 
Economic intelligence ni muhimu sana kwenye maendeleo ya nchi
Vitendo vinatushitaki, hivi ni economic intelligence inayoshindwa kukuarifu namna bora ya kuendesha sera zako za uchumi na kuishia kujiwekea target la kusanyo la Tril 28.7 kwa mwaka kupitia kubuni tozo tu. Tax base imeishia kwenye kutozana tu?
 
Kabisa ni porojo as usual, sana sana watakaondelea kufaidi ni wenye malori ya mizigo na viwanda. Hawa walikuwa wanafaidi bila hata huu umoja wa EAC. Hii jumuiya ilikuwa na makubaliano ya kuwa ma sarafu ya pamoja, lakini hadi leo ni hadithi tu. Ni umoja ceremonial zaidi kuliko kunachohubiriwa.
 
sisi vyombo vya habari na magazeti,redio, social media wako busy wanajadili sijui membe, Kinana ,simba wa yuda na pumba zingine.
Hizi mada za msingi kuzingumzia sasa.
Na app.ya mange kimambi,lakini kuelimisha jamii kwa mambo ya msingi sifuri
 
Ahsante kwa taarifa, na ngoja tuone...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…