Ole Ngurumwa: Wilaya ya Ngorongoro ni kubwa sana; nchi ya Zanzibar inaingia mara 7 na DSM inaingia mara 10. Wamasai waachwe wilayani humo

Ole Ngurumwa: Wilaya ya Ngorongoro ni kubwa sana; nchi ya Zanzibar inaingia mara 7 na DSM inaingia mara 10. Wamasai waachwe wilayani humo

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mwanaharakati na Wakili msomi Ole Nguruma amesema hata kama itakuwa ni lazima kuwahamisha wamasai kutoka hifadhini basi wasipelekwe nje ya wilaya ya Ngorongoro.

Ole Nguruma amesema Ngorongoro ina eneo la mita za mraba za kutosha kabisa kuishi wamasai wote kwani nchi ya Zanzibar inaingia mara 7 ndani ya wilaya hiyo kadhalika mkoa wa Dar es salaam unaingia mara 10

Chanzo: Star TV!
 
Hata ingekuwa na ukubwa wa Morogoro kwa nini mng'ang'ane huko?...Mbona mpo Kenya, Arusha,Tanga, Morogoro aliyewaambia ni lazima kukaa Ngorongoro ni nani?.
 
Pia Ole akumbuke kuwa kuna maeneo makubwa nje ya hifadhi na nje ya mkoa wa Arusha ambayo hayana watu Wala wanyama. Kwa Nini anakariri Ngorongoro Kuna maslahi gani?
Sasa unadhani tunang'ang'ania bila maslahi. Maslahi ya Wamaasai pale Ngorongoro sio ya kuficha na hakuna anayeficha. Anayetaka Wamaasai waondolewe Ngorongoro ndio mwenye maslahi yaliyojificha.

Kwani sisi tuliwaambia mababu zao wakaishi kwenye jiolojia isiyovutia? Kwani sisi tuliwaambia mababu zao wale wanyamapori hadi ndege? Kwani sisi tuliwaambia mababu zao walime kila sehemu katika makazi yao?

Sisi tuna maslahi nayo. Ni eneo ambalo mababu zetu waliona inatufaa. Na kweli tumeona inatufaa kwa shughuli zetu za ufugaji.

Mababu zenu walichagua ardhi inayotosha bustani ya mboga mboga tu. Mababu zetu walichagua inayotosha ufugaji na wanyamapori pia.
 
Wakiondoka wewe utanufaika na nini na sasa unapata hasara gani wakiwepo?
Wakiondoka Taifa la Tanzania litafaidika kwa sababu wanyama wataendelea kuwepo na kuongezeka hivyo kuhakikisha nchi kuendelea kupata mapato makubwa kupitia utalii. wakibaki wataendelea kuongezeka na kupelekea wanyama kukimbilia kwenu Kenya hivyo Tanzania itakosa mapato ya utalii ambayo ndo sekta inayochangia kuzidi sekta zone kwenye pato la taifa
 
We mpuuzi haya mapato yanakunufaisha na nini? Akina Kigwangala walikuwa wanatumia pesa kwenda kula raha na mademu Ulaya, baada ya miaka 20 hakuna mtu atatoka Ulaya kuja kuangalia fisi watu wanahama huko utalii sasahivi ni wa sayari ya Mars watu wanaenda huko na siyo kuja kuona fisi anakimbiza nyumbu.
 
Zanzibar kuna idadi kiasi gani cha wanyamapori? Simba wakizagaa Zanzibar tutawaondoa, Hata tukisema tupeleke myama wetu pendwa Twiga ila wakizaana wakawa wengi hadi kuwa kero kwenye shughuli za wananchi unadhani wananchi ndio wataama na kuwaacha hao twiga mijini au watawapeleka Zoo?
 
Back
Top Bottom