Ole Ngurumwa: Wilaya ya Ngorongoro ni kubwa sana; nchi ya Zanzibar inaingia mara 7 na DSM inaingia mara 10. Wamasai waachwe wilayani humo

Ole Ngurumwa: Wilaya ya Ngorongoro ni kubwa sana; nchi ya Zanzibar inaingia mara 7 na DSM inaingia mara 10. Wamasai waachwe wilayani humo

We mpuuzi haya mapato yanakunufaisha na nini? Akina Kigwangala walikuwa wanatumia pesa kwenda kula raha na mademu Ulaya, baada ya miaka 20 hakuna mtu atatoka Ulaya kuja kuangalia fisi watu wanahama huko utalii sasahivi ni wa sayari ya Mars watu wanaenda huko na siyo kuja kuona fisi anakimbiza nyumbu.
Hayo maneno kawaambie wenzako Kenya mnaotaka Ngorongoro ife ili Tanzania ife kiutalii na ifaidike nchi yako Kenya
 
Mwanaharakati na Wakili msomi Ole Nguruma amesema hata kama itakuwa ni lazima kuwahamisha wamasai kutoka hifadhini basi wasipelekwe nje ya wilaya ya Ngorongoro.

Ole Nguruma amesema Ngirongoro ina eneo la mita za mraba za kutosha kabisa kuishi wamasai wote kwani nchi ya Zanzibar inaingia mara 7 ndani ya wilaya hiyo kadhalika mkoa wa Dar es salaam unaingia mara 10

Source: Star tv!
Hawataki waondoke wilaya ya Ngorongoro. Watoke ndani ya hifadhi wawaachie wanyama wajitanue kwa nafasi. Wana siasa washaanza longolongo zao kama kawaida. Nakujiita wasomi juu
 
Hata ingekuwa na ukubwa wa Morogoro kwa nini mng'ang'ane huko?...mbona mpo Kenya, Arusha,Tanga, Morogoro aliyewaambia ni lazima kukaa Ngorongoro ni nani?.
Tuna maslahi nayo. Wamasai wa Ngorongoro tumezoea hali ya hewa ya Ngorongoro. Hali ya hewa ya Moro, Chalinze, Tanga ni tofauti sana na ya hali ya hewa ya Ngorongoro.
Kama vipi NCA wapewe eneo katika maeneo ya wazi mikoa mingine halafu waje wahamishe wanyama.
Wakifanya promotion ya nguvu, watalii wataenda na huko.
Watuachie Caldera yetu. Wanyama wachache watakaobaki, tutaishi nao.
 
Huyu hana tofauti na ACT wazalendo, alikuwa wapi kusema mapema mpaka jana PM alipotoa msimamo wa serikali na yeye ndiyo anaamka leo? hongereni CHADEMA mpo mbele ya wakati sn
Huyo ni mwanaCCM alichukua form ya kugombea ubunge Jimbo la Serengeti kupitia CCM usifananishe CHADEMA na huyo mfugo.
 
Pia Ole akumbuke kuwa kuna maeneo makubwa nje ya hifadhi na nje ya mkoa wa Arusha ambayo hayana watu Wala wanyama. Kwa Nini anakariri Ngorongoro, kuna maslahi gani?
Eni jioo marupurupu! huwezi amini kuna Mpaka ya utafiti wa inzi
 
Fact Check:

Ngorongoro Area: 8,292km
Zanzibar Area: 2,561km
Dar-es-Salaam: 1,590km
 
Kilimanjaro kuna Hifadhi ya KINAPA na pembezoni kuna makazi. Huo Mkoa sheria za mazingira ni kali kila kona iwe kwenye makazi hadi kwenye hifadhi.

Cha msingi, mifano iliyopo Kilimanjaro na mikoa mingine itumike pia Ngorongoro kwamba watu waishi na hifadhi ishamiri na isiharibiwe
 
Mwanaharakati na Wakili msomi Ole Nguruma amesema hata kama itakuwa ni lazima kuwahamisha wamasai kutoka hifadhini basi wasipelekwe nje ya wilaya ya Ngorongoro.

Ole Nguruma amesema Ngorongoro ina eneo la mita za mraba za kutosha kabisa kuishi wamasai wote kwani nchi ya Zanzibar inaingia mara 7 ndani ya wilaya hiyo kadhalika mkoa wa Dar es salaam unaingia mara 10

Chanzo: Star TV!

bahati mbaya it will be complicated ili watu wapige pesa
 
Mwanaharakati na Wakili msomi Ole Nguruma amesema hata kama itakuwa ni lazima kuwahamisha wamasai kutoka hifadhini basi wasipelekwe nje ya wilaya ya Ngorongoro.

Ole Nguruma amesema Ngorongoro ina eneo la mita za mraba za kutosha kabisa kuishi wamasai wote kwani nchi ya Zanzibar inaingia mara 7 ndani ya wilaya hiyo kadhalika mkoa wa Dar es salaam unaingia mara 10

Chanzo: Star TV!
Wliya ni Loliondo na sio Ngorongoro
 
Moja: Hivi kwani kuna mawakili ambao sio wasomi? Kwa nini huyu apewe title msomi?
Mbili: Hivi kuna uhusiano gani baina ya ngorongoro na nchi ya zanzibar au mji wa dar es salaam?
Tatu: Hivi ni mimi tu ambae nimeshindwa kuona anachosema huyu anaeitwa msomi? Sasa kama Zanzibar
inaingia mara 7 ndio iwe nini?
 
Back
Top Bottom