Ole Sabaya adaiwa kumshambulia Diwani wa Sombetini Arusha

Ole Sabaya adaiwa kumshambulia Diwani wa Sombetini Arusha

diwani tajiri

Senior Member
Joined
Oct 14, 2017
Posts
165
Reaction score
796
Sabaya matatani kwa kumshambulia Diwani wa Sombetini Arusha

Philip Kana - 23rd February 2021

MKUU wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya, ambaye amekuwa anatuhumiwa na kuhusishwa na matendo kadhaa ya kijambazi, sasa ametuhumiwa kumshambulia Diwani wa kata ya Sombetini, jiji Arusha, Bakari Msangi, Februari 9 mwaka huu. Katika tukio hilo, Sabaya aliambatana na walinzi wake binafsi sita wakiwa na bunduki moja na bastola mbili.

Kwa mujibu wa Msangi na watu walioshuhudia tukio hilo, diwani huyo alishambuliwa baada ya kupigiwa simu na mfanyabiashara mmoja mkoani humo, Ally Asaad Ajirin, anayemiliki duka la mapazia la Shaahidi Stores lililopo Barabara ya Nyamwezi jirani na Soko Kuu, jijini Arusha.

Mfanyabiashara huyo alimpigia Msangi simu akimuomba msaada baada ya vijana wake wa dukani kumtaarifu kuwa Sabaya na vijana wake wamewafungia dukani na wanawapiga.

Sabaya alikuwa anahitaji shilingi milioni 100 kutoka kwa mfanyabiashara huyo, Asaad, akimtuhumu kufanya biashara ya kuuza fedha za kigeni kwa magendo.

Sabaya alitaka apewe fedha hizo, vinginevyo angemfungulia Asaad kesi ya uhujumu uchumi.

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Salum Hamduni, Februari 16 mwaka huu alithibitisha kutokea kwa tukio hilo akasema wanaendelea na uchunguzi ingawa hakuwa tayari kulizungumzia kwa kina.

Kikao cha kamati ya ulinzi na usalama mkoa Arusha, ambacho mwenyekiti wake ni mkuu wa mkoa, Iddi Kimanta, kilichokaa Februari 12 mwaka huu, kilimwalika diwani Msangi na kupokea maelezo yake, kisha kikamwagiza RPC Hamduni kuhakikisha anaendelea na taratibu za kipolisi wakati wao wakiendelea na taratibu za kuwasiliana na mamlaka ya uteuzi wa DC Sabaya. Tangu siku hiyo, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.

Siku ya tukio, Sabaya alifika dukani kwa mfanyabiashara huyo majira ya saa 11 jioni akawataka wafanyakazi wake wamweleze alipo Asaad. Walimpigia simu akawa hapokei.

“Waliniambia mpigie simu mjomba wako mwambie tunataka pazia. Mimi nikampigia mjomba simu ikawa inaita tu. Wakatunyang’anya wafanyakazi wote simu tukawekwa chini ya ulinzi,” alisema mmojawao, Norman Jasin, na kuongeza:

“Nilikuwa mimi na mfanyakazi wangu mmoja, ikawa mtu yeyote akiingia dukani anawekwa chini ya ulinzi wanataka kujua ni nani. Machinga waliokuwa wanaona duka linafungwa wanakimbilia kuchukua mali wawapelekee wateja akiingia wanawekwa chini ya ulinzi na kipigo juu.”

“Walivuta mlango wakaanza kutupiga kwa kupokezana. Sabaya akawa analazimisha tusema mjomba Asaad alipo, sisi tukawa hatujui, tukipiga simu yake inaita tu. Sabaya akapanda juu akageuza kamera ili wasionekane, lakini ilikuwa imesharekodi.”

“Diwani Msangi alipofika dukani hapo akawa anaongea na Sabaya lakini tukashangaa na yeye anapigwa hata kuliko sisi.

Baada ya kuwapiga sana majira ya saa tatu usiku aliwachukua vijana wawili akawaepeleka kwenye kituo cha polisi cha kati na kuagiza wafunguliwe mashitaka ya uhujumu uchumi huku akiondoka na diwani Msangi ambaye walikuwa wamemfunga pingu. Kwenye tukio hilo vijana wa duka hilo zaidi ya watatu na wateja wao walipigwa kuna waliojisaidia haja kubwa na waliojikojolea .

Msafara wa Sabaya ulikuwa wa magari mawili ambapo gari moja liliwabeba vijana wawili wa dukani na lingine ambalo alikuwepo Sabaya mwenyewe alipakiwa diwani Msangi.

Sabaya ametumia gharama kubwa kuhakikisha habari hii haiandikwi kwenye chombo chochote cha habari. Siku moja baada ya tukio hilo waandishi walianza kuifuatilia.

Sabaya alipopata taarifa majira ya saa 2 usiku waandishi hao wakiwa wameweka kambi polisi aliwasiliana na mmoja wa wao kisha akawatumia kiasi cha shilingi laki nne kwenye simu ya mwandishi mmoja.

Hata hivyo, alipata taarifa bado kuna waandishi wengine wanne wanafuatilia habari hiyo aliwasiliana na mmoja wao akawaita ofisini kwake Hai akawapa fedha kila laki .

Baada ya hapo alikuwa akijipongeza kuwa suala hilo limekwisha kwa kile alichowaeleza watu wake wa karibu kuwa suala hilo lingekuwa gumu kulimaliza endapo vyombo vya habari vingeandika ila kwa hatua iliyopo anajua namna ya kulimaliza.

Hata hivyo amekuwa akiendelea na jitihada za kumshawishi diwani Msangi wayamalize na yuko taysti kumpatia hata fedha milioni 20 lakini imeshindikana.

Sabaya amekuwa akizunguka mara kwa mara jijini Arusha huku akilazimisha wafanyabiashara kumpa fedha vinginevyo atawafungulia kesi za uhujumu uchumi.

Amekuwa akizunguka na magari yake binafsi matatu ambayo hubandika namba za usajili tofauti tofauti ikiwemo za umoja wa mataifa (UN) na ya Miradi inayofadhiliwa na watu kutoka nje ya nchi, (DFP) ambapo huwa na mabaunsa kati ya watatu na sita na hupenda kufikia hoteli za kitalii za Tulia, Mount Meru, Orlando Garden na Lush garden.

Sabaya amekuwa akitumia muda mwingi jijini Arusha wakati yeye ni Mkuu wa wilaya ya Hai jambo ambalo limekuwa likiibua maswali mengi kutoka kwa wananchi na wafanyabiashara ambao ndiyo wahanga wa matukio yake ya kitapeli.

Taarifa hizo zilipofika Ikulu Sabaya aliitwa na alishikiliwa kwa siku tatu ili atoe maelezo ambapo yeye mwenyewe anasema kilichomsaidia wakati ule alikuwa akinunua madiwani na viongozi wa Chadema Hai .Mwaka 2019 Sabaya alikusanya zaidi ya milioni 300 kutoka kwa wafanyabiashara jijini hapa akiwaahidi kuwatafutia fursa ya kuwa miongoni mwa wafanyabiashara watakaoshiriki kikao cha Rais John Magufuli na wafanyabiashara jijini Dar es Salaam.

Sabaya ambaye huongea kwa kujidai na kujiamini mbele za watu anasema alimweleza Rais, Magufuli fedha ni kweli alichukua na ndiyo anazitumia kutekeleza mpango huo a na kamhakikishia Rais Magufuli atazitumia kumng’oa Freeman Mbowe kwenye ubunge jimbo la Hai hivyo akasamehewa.

Sabaya amekuwa akitumia mamlaka yake ya ukuu wa wilaya kuwatisha wafanyabiashara kwenye mikoa ya kilimanjaro na hasa Arusha huku ambapo kwa wenye vituo vya mafuta hutumia mabavu kulazimisha magari yake matatu anayozunguka nayo yajazwe mafuta.
Hata hivyo tayari baadhi ya wafanyabiashara hao wameamua kutoa taarifa kwa mkuu wake wa mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mugwira ndipo akapunguza kuwatisha.

Sabaya amekuwa na kawaida ya kuongozana na mabaunsa wake na amekuwa akionekana kwenye maeneo mbalimbali ya starehe ila amekuwa na tabia ya kutokulipa bili mara baada ya kuanya matumizi.

“Sabaya akiingia hapa kila mtu hataki kumhudumia. Huwa anakunywa na kula lakini halipi. Unashangaa wanaanza kuondoka mabaunsa wake halafu yeye anakuwa wa mwisho kuondoka akiwa anaongea na simu hata ukimfuata mpaka kwenye gari anaendelea kuongea na simu huku gari inaondoka,” alisema mhudumu wa bar moja iliyopo maeneo ya Sakina.

Hadi tunaenda mitamboni, Sabaya hakupatikana kujibu hoja na tuhuma zinazomkabili. SAUTI KUBWA inaendelea kumsaka.

Source: Sabaya matatani kwa kumshambulia Diwani wa Sombetini Arusha - Sauti Kubwa
 

Diwani Msangi wa Sombetini afunguka juu ya kipigo alichopewa na Sabaya​


DIWANI wa Kata ya Sombetini, Wilaya ya Hai, Bakari Msangi, amefunguka namna alivyoshambuliwa na mkuu wa hiyo, Lengai Ole Sabaya akiwa na walinzi binafsi.

Anadai kwamba Sabaya wakati akimshamblia, alikuwa na walinzi wake binafsi sita waliobeba silaha ikiwamo bastola mbili.

Diwani huyo ameiambia SAUTI KUBWA kwamba ameamua kuyasema hayo baada ya Sabaya na wapambe wake kusambaza taarifa kuwa Februari 9, mwaka huu, alipigwa na baaadhi ya watu baada ya kumfumania “akiwa na mke wa mtu.”

Msangi akielezea namna tukio hilo lilivyokuwa anasema, Februari 9, mwaka huu majira ya saa 11 jioni alipokea simu kutoka kwa Mohamed Asaad, akimweleza kuwa mkuu huyo wa wilaya amevamia dukani kwake, hivyo kama anafahamiana naye anaomba akamsikilize na kumsaidia. Assad ni mmiliki wa duka la mapazia la Shaahidi Storea lililopo Barabara ya Nyamwezi karibu na Soko Kuu jijini Arusha.

Msangi anasema: “Mimi nikaenda pale dukani nikakuta mlango wa chuma umefungwa nikagonga hawakufungua, nikaamua kuuvuta juu nikaingia. Kweli nikamkuta Sabaya na vijana wake sita wamewaweka chini ya ulinzi wafanyakazi na wateja waliokuwa kwenye hilo duka, wanawapiga,” anasema Msangi na kuongeza.

“Nikamuuliza Sabaya kuna shida gani? Akaniambia hawa Waarabu ni wahujumu uchumi, wanafanya biashara haramu wanauza dola feki, wanauza bidhaa hawatoi risiti, akaniorodhesha makosa kibao…

“Nikamwambia mimi kama diwani wajibu wangu ni kuwatetea wananchi wa Arusha, lakini wewe hapo ulipo siyo TRA, (Mamlaka ya Mapato Tanzania), siyo Takukuru wala Usalama wa Taifamna siyo polisi, iweje uwanyanyase hawa badala ya kutumia vyombo husika vikaja kuwakamata hawa watu?”

Msangi anasema kuwa kauli hiyo ilionekana kumuudhi Sabaya ambaye bila simile alimgeukia na kuanza kumshushia kipigo.

“Aliwaamuru vijana wake waninyang’anye simu zangu, wakachukua na fedha walizonikuta nazo kama laki tatu na elfu tisini, wakanipiga vibao wakanikalisha chini,” anasema Msangi na kuongeza.

“Walipokuwa wananikalisha, niligoma, wakaamua kunifunga pingu mikononi. Wakaanza kunipiga, nikamwambia Sabaya haki ya Mungu mtaniua, lakini sitaondoka hapa mpaka nisimamie haki ya hawa watu.

“Wakati haya yakiendelea, Sabaya alimchukua mdogo wa mwenye duka na kuingia naye chumba kingine ambako walikuwa wakizungumza. Baadaye nikagundua kuwa alikuwa akimuamuru ampigie simu kaka yake, Asaad ili aje dukani kwake…”

Diwani huyo anasema kuwa iIlipofika saa tatu usiku alimwambia Sabaya awaache, lakini aligoma na baadaye kuwapiga vibao wateja waliokuwamo ndani ya duka na wadogo wa Asaad, kisha aliwaambia waondoke.

“Sabaya akapiga simu kwa OC CID akamwambia kuna watu nimewakamata ni wahujumu uchumi nataka kuwaleta hapo polisi. Wale ndugu zake Assad wawili wakaingizwa kwenye gari la walinzi aliokuwa nao – mabaunsa, mimi nikaingizwa kwenye gari alilokuwa amepanda Sabaya…

“Msafara ukaanza kuelekea Central, tulipofika tukamkuta OC CID, Gwakisa kasimama nje anatusubiri na mimi nikataka kushuka, lakini Sabaya akanizuia.”

Diwani Msangi anasema Sabaya alimwambia hajamshusha polisi kwa sababu hajamaliza kazi naye, anataka akamuonyeshe nyumbani kwa Ally Assad Ajirin na kwa kaka yake Mohamed Assad Ajirin. Anazidi kusimulia:

“Tukaenda kwa Ally Assad Ajirin, tukafika tukagonga mlango hawakufungua. Kidogo wakati tunatoka, tukakutana na mzee mmoja anaongea na simu akajua labda ni mzee wa familia hiyo akamkamata baadaye akamuacha” anasema Msangi na kuongeza.

“Tukaondoka tukaenda kwa Mohamed Assad tulipofika akavunja mlango akaingia ndani akawaluta mke wa Mohamed na watoto. Hawakumkuta Mohamed, hivyo tukaondoka.

“Tukatoka tukazunguka mjini mimi nikiwa nimefungwa pingu. Baadaye wakaenda supermarket ya Panone pale Ngarenaro wakanunua vinywaji wakawa wanakunywa, kisha tukaondoka mpaka pale Hoteli ya Tulia, iko pale WhiteRose,”.

“Tulipofika hapo wakaingia ndani wakaniacha mimi kwenye gari wakawa kama wamenisahau. Palepale nikaona mfuko waliokuwa wameweka simu, nikavivuta nikafanikiwa kuchukua simu.

“Simu kubwa nikaiicha ndani ya chupi nyingine ndogo nikaitumia kumpigia mke wangu. Nikamwambia yote yaliyonikuta, nikamwambia anifuate ila aje na jirani yetu hapo nyumbani.

“Baadaye kidogo, Sabaya akatoka akiwa kabadili nguo, mwanzo alikuwa kavaa kaunda suti sasa ametoka kavaa koti, akaja kwenye gari akaniambia nasikia kuwa watu wanakutafuta ni nani, nikamwambia sijui…

“Sabaya akasema itakuwa ana simu huyu embu mpigeni ‘teru’ (mkagueni). Walinikagua, lakini walishindwa kuziona kwa sababu zilikuwa ndani ya suruali.

“Sabaya alimuona mke wangu eneo lile, jirani na gari lake, akahoji akisema ‘huyu malaya anayekufuatilia ni nani?’

“Akawa anawaagiza mabaunsa wake waende wakamchukue, nikawaambia mtamchukuaje mke wangu, baadaye nikaamuriwa kwenda kuzungumza naye nikiwa chini ya ulinzi…

“Sabaya akaja akamtolea mke wangu bastola akamwambia leo naenda kumuua Bakari. Mke wangu akapiga ukunga, Sabaya akaona kuna shida, lakini mimi nikamwambia mke wangu asiwe na wasiwasi kwani hapo walipofika hawezi kufanya chochote nikamwambia akanisubiri Arusha Technical …

“Mabaunsa wakaniingiza kwenye gari tukaondoka tulipofika pale Petrol Station ya Mount Meru, kabla ya taa za barabarani, wakasimamisha gari wakaniambia nishuke nikimbie. Nikagoma, wao wako na bunduki na bastola nakimbia vipi? Wangeweza kunipiga risasi nikawaambia wanipeleke mahali mke wangu yupo…

“Wakaenda wakanishusha pale Arusha Technical ambapo mke wangu alikuwa wakanipiga mkwara. Nikaondoka kufika nyumbani ndiyo nikaanza kusikia maumivu, nikawapigia viongozi wenzangu sikuwapata ….

“Nikaamua kumpigia simu Mkuu wa Mkoa, Iddi Kimanta nikamweleza kila kitu, yule mzee alilia kabisa wakati naongea naye. Akawapigia RPC na OCD akawaeleza kisha akaniambia tukutane Polisi, nilipofika nikawakuta viongozi wamejaa …

“Ilikuwa saa sita usiku, wakaniandikia PF3 nikaenda hospitali kutibiwa, hivi napokwambia naendelea na matibabu na polisi wako kwenye uchunguzi.”

Diwani huyo alisema kuwa hakuweza kutambua namba za gari alilokuwa akitumia Sabaya kwani wakati wakitoka dukani kwa Assad alikuwa ameweka namna za DFP na walipokuwa wakitoka hoteli ya tulia alikuwa amebandika namna za UN.

Kamanda wa Takukuru mkoani Arusha, James Ruge alisema endapo tukio hilo lilitokea, halina uhusiano na taasisi anayoiongoza, na kubainisha kuwa “hiyo ni jinai.”

Sabaya hakujibu simu za mwandishi wetu wala ujumbe mfupi wa simu uliomtaka azungumzir sakata hili na tuhuma hizi.

Chanzo: Sauti Kubwa
 

Diwani Msangi wa Sombetini afunguka juu ya kipigo alichopewa na Sabaya​

012b0c359b0d3e4beca9ed8b3b1445f3

Philip Kana 4th April 20210 Comments

DIWANI wa Kata ya Sombetini, Wilaya ya Hai, Bakari Msangi, amefunguka namna alivyoshambuliwa na mkuu wa hiyo, Lengai Ole Sabaya akiwa na walinzi binafsi.
Anadai kwamba Sabaya wakati akimshamblia, alikuwa na walinzi wake binafsi sita waliobeba silaha ikiwamo bastola mbili.
Diwani huyo ameiambia SAUTI KUBWA kwamba ameamua kuyasema hayo baada ya Sabaya na wapambe wake kusambaza taarifa kuwa Februari 9, mwaka huu, alipigwa na baaadhi ya watu baada ya kumfumania “akiwa na mke wa mtu.”
Msangi akielezea namna tukio hilo lilivyokuwa anasema, Februari 9, mwaka huu majira ya saa 11 jioni alipokea simu kutoka kwa Mohamed Asaad, akimweleza kuwa mkuu huyo wa wilaya amevamia dukani kwake, hivyo kama anafahamiana naye anaomba akamsikilize na kumsaidia. Assad ni mmiliki wa duka la mapazia la Shaahidi Storea lililopo Barabara ya Nyamwezi karibu na Soko Kuu jijini Arusha.
Msangi anasema: “Mimi nikaenda pale dukani nikakuta mlango wa chuma umefungwa nikagonga hawakufungua, nikaamua kuuvuta juu nikaingia. Kweli nikamkuta Sabaya na vijana wake sita wamewaweka chini ya ulinzi wafanyakazi na wateja waliokuwa kwenye hilo duka, wanawapiga,” anasema Msangi na kuongeza.
“Nikamuuliza Sabaya kuna shida gani? Akaniambia hawa Waarabu ni wahujumu uchumi, wanafanya biashara haramu wanauza dola feki, wanauza bidhaa hawatoi risiti, akaniorodhesha makosa kibao…
“Nikamwambia mimi kama diwani wajibu wangu ni kuwatetea wananchi wa Arusha, lakini wewe hapo ulipo siyo TRA, (Mamlaka ya Mapato Tanzania), siyo Takukuru wala Usalama wa Taifam na siyo polisi, iweje uwanyanyase hawa badala ya kutumia vyombo husika vikaja kuwakamata hawa watu?”
Msangi anasema kuwa kauli hiyo ilionekana kumuudhi Sabaya ambaye bila simile alimgeukia na kuanza kumshushia kipigo.
“Aliwaamuru vijana wake waninyang’anye simu zangu, wakachukua na fedha walizonikuta nazo kama laki tatu na elfu tisini, wakanipiga vibao wakanikalisha chini,” anasema Msangi na kuongeza.
“Walipokuwa wananikalisha, niligoma, wakaamua kunifunga pingu mikononi. Wakaanza kunipiga, nikamwambia Sabaya haki ya Mungu mtaniua, lakini sitaondoka hapa mpaka nisimamie haki ya hawa watu.
“Wakati haya yakiendelea, Sabaya alimchukua mdogo wa mwenye duka na kuingia naye chumba kingine ambako walikuwa wakizungumza. Baadaye nikagundua kuwa alikuwa akimuamuru ampigie simu kaka yake, Asaad ili aje dukani kwake…”
Diwani huyo anasema kuwa iIlipofika saa tatu usiku alimwambia Sabaya awaache, lakini aligoma na baadaye kuwapiga vibao wateja waliokuwamo ndani ya duka na wadogo wa Asaad, kisha aliwaambia waondoke.
“Sabaya akapiga simu kwa OC CID akamwambia kuna watu nimewakamata ni wahujumu uchumi nataka kuwaleta hapo polisi. Wale ndugu zake Assad wawili wakaingizwa kwenye gari la walinzi aliokuwa nao – mabaunsa, mimi nikaingizwa kwenye gari alilokuwa amepanda Sabaya…
IMG-20210223-WA0457-1015x1024.jpg
(Sabaya)
“Msafara ukaanza kuelekea Central, tulipofika tukamkuta OC CID, Gwakisa kasimama nje anatusubiri na mimi nikataka kushuka, lakini Sabaya akanizuia.”
Diwani Msangi anasema Sabaya alimwambia hajamshusha polisi kwa sababu hajamaliza kazi naye, anataka akamuonyeshe nyumbani kwa Ally Assad Ajirin na kwa kaka yake Mohamed Assad Ajirin. Anazidi kusimulia:
“Tukaenda kwa Ally Assad Ajirin, tukafika tukagonga mlango hawakufungua. Kidogo wakati tunatoka, tukakutana na mzee mmoja anaongea na simu akajua labda ni mzee wa familia hiyo akamkamata baadaye akamuacha” anasema Msangi na kuongeza.
“Tukaondoka tukaenda kwa Mohamed Assad tulipofika akavunja mlango akaingia ndani akawaluta mke wa Mohamed na watoto. Hawakumkuta Mohamed, hivyo tukaondoka.
“Tukatoka tukazunguka mjini mimi nikiwa nimefungwa pingu. Baadaye wakaenda supermarket ya Panone pale Ngarenaro wakanunua vinywaji wakawa wanakunywa, kisha tukaondoka mpaka pale Hoteli ya Tulia, iko pale WhiteRose,”.
“Tulipofika hapo wakaingia ndani wakaniacha mimi kwenye gari wakawa kama wamenisahau. Palepale nikaona mfuko waliokuwa wameweka simu, nikavivuta nikafanikiwa kuchukua simu.
“Simu kubwa nikaiicha ndani ya chupi nyingine ndogo nikaitumia kumpigia mke wangu. Nikamwambia yote yaliyonikuta, nikamwambia anifuate ila aje na jirani yetu hapo nyumbani.
“Baadaye kidogo, Sabaya akatoka akiwa kabadili nguo, mwanzo alikuwa kavaa kaunda suti sasa ametoka kavaa koti, akaja kwenye gari akaniambia nasikia kuwa watu wanakutafuta ni nani, nikamwambia sijui…
“Sabaya akasema itakuwa ana simu huyu embu mpigeni ‘teru’ (mkagueni). Walinikagua, lakini walishindwa kuziona kwa sababu zilikuwa ndani ya suruali.
“Sabaya alimuona mke wangu eneo lile, jirani na gari lake, akahoji akisema ‘huyu malaya anayekufuatilia ni nani?’
“Akawa anawaagiza mabaunsa wake waende wakamchukue, nikawaambia mtamchukuaje mke wangu, baadaye nikaamuriwa kwenda kuzungumza naye nikiwa chini ya ulinzi…
“Sabaya akaja akamtolea mke wangu bastola akamwambia leo naenda kumuua Bakari. Mke wangu akapiga ukunga, Sabaya akaona kuna shida, lakini mimi nikamwambia mke wangu asiwe na wasiwasi kwani hapo walipofika hawezi kufanya chochote nikamwambia akanisubiri Arusha Technical …
“Mabaunsa wakaniingiza kwenye gari tukaondoka tulipofika pale Petrol Station ya Mount Meru, kabla ya taa za barabarani, wakasimamisha gari wakaniambia nishuke nikimbie. Nikagoma, wao wako na bunduki na bastola nakimbia vipi? Wangeweza kunipiga risasi nikawaambia wanipeleke mahali mke wangu yupo…
“Wakaenda wakanishusha pale Arusha Technical ambapo mke wangu alikuwa wakanipiga mkwara. Nikaondoka kufika nyumbani ndiyo nikaanza kusikia maumivu, nikawapigia viongozi wenzangu sikuwapata ….
“Nikaamua kumpigia simu Mkuu wa Mkoa, Iddi Kimanta nikamweleza kila kitu, yule mzee alilia kabisa wakati naongea naye. Akawapigia RPC na OCD akawaeleza kisha akaniambia tukutane Polisi, nilipofika nikawakuta viongozi wamejaa …
“Ilikuwa saa sita usiku, wakaniandikia PF3 nikaenda hospitali kutibiwa, hivi napokwambia naendelea na matibabu na polisi wako kwenye uchunguzi.”
Diwani huyo alisema kuwa hakuweza kutambua namba za gari alilokuwa akitumia Sabaya kwani wakati wakitoka dukani kwa Assad alikuwa ameweka namna za DFP na walipokuwa wakitoka hoteli ya tulia alikuwa amebandika namna za UN.
Kamanda wa Takukuru mkoani Arusha, James Ruge alisema endapo tukio hilo lilitokea, halina uhusiano na taasisi anayoiongoza, na kubainisha kuwa “hiyo ni jinai.”
Sabaya hakujibu simu za mwandishi wetu wala ujumbe mfupi wa simu uliomtaka azungumzir sakata hili na tuhuma hizi.
IMG-20210404-WA0375-1.jpg
Siku zake zinahesabika
 
Watu wa Chuga na K'njaro nawalaumu sana. Zamani walifahamika kama watu wa misheni town na deals sasa wameshindwa kumshughulikia huyu jamaa?

Hata kumuendea Congo kumroga? Hata kumpiga bomba (chuma)?
Huyo mroho wa pombe mbona huwa rectum inakutwa ikining'inia

Unamkodia ndugu wa Mashekhe wa Uamsho wakeshe nae mtaroni
 
Ole Sabaaya amedhulumu wafanyabiashara wengi sana Arusha, hasa wenye makampuni ya Tours & Hotels. Huyo akifika hotel yoyote halipi hata akae mwezi mzima, yeye na wapambe wake hata wakiwa watu 8, watalala na kula bure. Akidaiwa anakimbilia mambo matatu;
1) Kukutolea bastola.
2) Kukutolea kitambulisho chake cha TISS.
3) Kukutishia kukupa kesi ya Uhujumu Uchumi.

Ametumia kila aina ya njia kuwadhalilisha na kuwatisha wafanyabiashara na raia. Amechezea na kudhalilisha sana mpaka wake na watoto wa kike. Mtu akikosana nae au akigoma kumpa hela anaweza akamchukulia mke halafu akawaambia wapambe wake hata wawili wampige mtungo.

Huyu sio binaadamu kabisa kabisa, yani ni mshenzi kweli, ni shetani kabisa.

Wapoloo wa chuga walikua wanamsubiri sana kwa hamu, na sasa wanajua muda umefika, wanasubiri Mama Samia amlipue tu arudi mtaani. Haki ya mungu wanampasua mchana kweupe labda ahame mkoa.
 
Huyu Sabaya inakuwaje anafanya kazi hizi za Kihakifu wilayani Hai na Arusha pia.Huyu Jamaa mbona anatesa watu hivyo...Nilisikiliza clip ya wafanya Niagara wa Hai..The guy doesn't deserve to hold a public office even one day more.Serikali yoyote yenye kuwajibika kwa watu wake huyu Jamaa hata Ubalozi wa nyumba Kumi Hafai.
 
Kabisa Mkuu Mwenyezi Mungu katunusuru na maovu mengi sana ambayo yangeweza kuwa chanzo cha machafuko ya kutisha nchini.

Why I hated that dead man with all my heart ni sababu aliwalea watu kama hawa
Asante Mungu kweli unaipenda Tanzania
 
Wakati wa Mungu wa HAKI ukifika hakuna kitakacjojificha. KARMA KARMA... hapa hapa duniani tutashuhudia
 
Back
Top Bottom