Ole Sabaya apanga kutoroka nchini, huenda akajificha Nairobi nchini Kenya

Ole Sabaya apanga kutoroka nchini, huenda akajificha Nairobi nchini Kenya

Hii ndiyo Taarifa ya uvunguni ambayo imevuja , kwamba yule kijana katili aliyetesa watu na kupora pesa za wafanyabiashara wa Hai anapanga kukimbia nchi hii baada uchunguzi dhidi yake kumkalia vibaya .

Lengo la kuleta Taarifa hii nyeti ni kuvitaarifu vyombo vinavyomchunguza kuhakikisha wanamuweka kwenye Zero distance ili asiwaache solemba na kukimbilia Nairobi ambako Sheria za Kenya zaweza kumlinda na asiletwe Tanzania kujibu mashitaka yake , Tafadhalini sana vyombo vya dola msije mkathubutu kumsaidia Sabaya kutoroka , hatutawaelewa na huenda mkasababisha machafuko , mwacheni afikishwe Mahakamani akajibu tuhuma zake na akawataje wote alioshirikiana nao .

Mara nyingi sana humu JF kupitia jukwaa hili hili , mimi binafsi na waungwana wengine wengi sana tumesisitiza sana vijana wanaopata bahati ya kuteuliwa kwenye uongozi kutumia uongozi wanaopewa kwa kutenda haki , wahakikishe wanafanya kazi zao kwa mujibu wa katiba ya nchi , wasithubutu kutekeleza unyama hata kama wametumwa na mkubwa , Biblia ilishaonya tangu enzi kumtegemea mwanadamu (YEREMIA 17:5) , Kila aliyetenda kinyume cha Katiba tumwache avune alichopanda .
Mod hii habari ya uongo imekaa muda mrefu sana.Lakin mmeiacha tu.Hamuoni JF itaonekana kama sehemu ya ubabaishaji tu na uong😵ndoa hii
 
Mod hii habari ya uongo imekaa muda mrefu sana.Lakin mmeiacha tu.Hamuoni JF itaonekana kama sehemu ya ubabaishaji tu na uong😵ndoa hii
unadhani kwanini alikamatwa tarehe 25 siku 2 baada ya uzi ? halafu huu uzi uliletwa kama tetesi baada ya nzi mmoja wa kundi la Sabaya kututonya , baada kila kitu kuwa hadharani tetesi ikaondolewa .
 
Kwani uchunguzi ukiendelea dhidi yake anakuwa nyumbani? sio yupo kwenye "mikono salama"
kwa mujibu wa Takukuru amekamatwa siku 2 baada ya uzi huu akiwa na mabaunsa wake , kumbe alikuwa huru tu .
 
Kitendo cha Yeye Kuchunguzwa tu kwa Amri ya Mheshimiwa Rais ( Amiri Jeshi Mkuu ) tayari Kimedani yuko chini ya Ulinzi na kamwe hawezi Kutotoka nchi kwani hata Wao waliomkamata wanalijua hili kuwa Wazo Mama ( Kuu ) la Ole Sabaya ni Kukimbia ( Kutoroka ) nchi hivyo nao ( Mamlaka ) wameshalidhibiti hili mapema tu.
I like your name. Wazee wa How to end a figjt in 1-3 minutes
 
Sabaya asikimbie mazao yake alivyopanda ni wakati wa kuvuna
 
Naipongeza serikali kwa kuingia JF na kusoma uzi huu
 
Back
Top Bottom