Dumas the terrible
JF-Expert Member
- Jan 20, 2021
- 4,779
- 9,999
Jamaa ana furushi la kesi
Haina namna ajitwishe tu!
Tunaendelea kuupiga mrefu Sana mbaka utoke nje!
Haina namna ajitwishe tu!
Tunaendelea kuupiga mrefu Sana mbaka utoke nje!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio aone raha ya kutumika kama dodoki,aliyemponza keshajifia zake yeye anaangaika.Kesi bado za kutosha lazima ajinyonge,kilimanjaro ziko za kutosha
Hiyo nyingine na ile nyingineKwa kweli! Mbona kama tuliambiwa utetezi/ushahidi ulikamilika na tunasubiri hukumu tarehe 1 Oktaba. Imekuwaje tena?
Mmojawapo ni huyu hapa Profesa Idugunde! Siku zote anaamini General wake Lengai Ole Sabaya hana hatia.Wale waliodai huyu mtu atachomoka basi kama kweli atachomoka na kesi zote hizo nitaamini kweli uchawi upo.
Ile kesi nyingine iliisha inasubiri hukumu.Sijaelewa,ni hukumu au mashtaka?
Ohoooo!!!Ile kesi nyingine iliisha inasubiri hukumu.
Hii kesi ya leo ni mpyaaaa kabisa, nayo itaenda itaisha itasubiri hukumu.
Zitakuja nyingine nyingi hadi za ubakaji...
Dogo ana miaka 34 ukijumlisha miaka 30 atatoka na 64.
Huoni kwamba wamizikusanya zote kwa pamoja ili wazibutue once and for all.....tafakari brotherWale waliodai huyu mtu atachomoka basi kama kweli atachomoka na kesi zote hizo nitaamini kweli uchawi upo.
tatizo ni kuwa wale waliokuwa mashahidi wa kubakwa na kulawitiwa waliingia mitini kwahiyo unavyoona hizi mza uhujumu uchumi hazina nguvu?Hizo kesi bila zile za ubakaji na ulawiti kuunganishwa zitakuwa kazi bure
Hiii ni keai nyingine tofauti na ile muwe mnaelewa.. ile inasubiri hukumu hii ni mpya imeanzaKwa kweli! Mbona kama tuliambiwa utetezi/ushahidi ulikamilika na tunasubiri hukumu tarehe 1 Oktaba. Imekuwaje tena?
Siku hiyo nitakunywa bia hatariiNasubiri za Bashite
Atafakari nini? Ile nyingine inasubiri hujumu hii ndio imeanza huoni tofauti?!tatizo ni kuwa wale waliokuwa mashahidi wa kubakwa na kulawitiwa waliingia mitini kwahiyo unavyoona hizi mza uhujumu uchumi hazina nguvu?
Mashitaka mapya banaSijaelewa,ni hukumu au mashtaka?
Taaaratibu huenda dpp anapitia bado mafaili ya kesi juu ya kesi..huyu na mbowe hadi maji wataita maaaHizo kesi bila zile za ubakaji na ulawiti kuunganishwa zitakuwa kazi bure
ulifia wapi wewe jamaa,umefufuka?Mashitaka mapya bana
Silioni hilo.Huoni kwamba wamizikusanya zote kwa pamoja ili wazibutue once and for all.....tafakari brother
Kwa Ccm hilo ni jambo la kawaida. Sifa kuu ya kuwa kiongozi Ccm ni uwe mwizi jambazi.09 September 2021
Mahakama ya Hakimu Mkazi
Arusha
Tanzania
SABAYA ASOMEWA MAKOSA MAPYA MATANO "ALICHUKUA MILIONI 90 KWA MFANYABIASHARA"
Aliyekuwa mkuuu wa wilaya ya hai Lengai Ole Sabaya na wenzake sita wamesomewa shtaka la uhujumu uchumi lenye makosa matano kwa madai yakuchukua million 90 kutoka kwa mfanyabiashara ili wasimchukulie hatua kwa kosa la ukwepaji wa kodi.
Ole Sabaya na wenziwe wakituhumiwa makosa ya uhujumu uchumi, unyang'anyi wakutumia silaha na utakatishaji fedha.
---
DPP aipa mamlaka Mahakama Hakimu Mkazi kusikiliza kesi ya Sabaya na wenzake
Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) imeipa mamlaka Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, kusikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake.
Ole Sabaya na wenzake wanakabiliwa na mashitaka matano ikiwemo kujihusisha na rushwa na utakatishaji fedha haramu Sh90 milioni.
Ofisi ya DPP imewasilisha hati ya kuipa mamlaka mahakama hiyo, leo Alhamisi Septemba 9, 2021 kupitia Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tarsila Gervas wakati kesi hiyo ilipofikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa.
Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi namba 27, 2021 ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.
Mbele ya Hakimu Mkazi, Patricia Kisinda, Wakili Tarsila ameieleza Mahakama kuwa DPP ametoa hati na ridhaa hiyo ya mahakama hiyo ya chini kusikiliza kesi hiyo.
"Mahakama Kuu ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi hii, ila DPP chini ya Kifungu cha 12(3) cha Sheria ya Uhujumu Uchumi ameona kwa maslahi mapana ya Taifa shauri hili lisikilizwe mahakama hii ya chini.
“Tutaanza kuwasilisha hati hizi alizotoa DPP na kwa kuwa Mahakama imekuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hii ni rai yetu kuwasilisha hati ya mashtaka na kuwasomea," amesema.
Baada ya Mahakama kupokea nyaraka hizo Wakili huyo aliwasomea upya mashitaka matano yanayowakabili ambayo ni kuongoza genge la uhalifu, kujihusisha na kitendo cha rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na utakatishaji fedha haramu Sh90 milioni, makosa ambayo washitakiwa hao walikana kuyatenda.
Kati ya makosa hayo matano, Sabaya peke yake anakabiliwa na makosa matatu ambayo ni kujihusisha na kitendo cha rushwa, kujihusisha na vitendo cha rushwa na kuchukua rushwa Sh90 milioni kutoka kwa Francis Mrosso na matumizi mabaya ya madaraka akiwa DC.
Mengine ni kumtishia Mrosso kuwa atamfungulia mashtaka ya kukwepa kodi kitendo ambacho ni kinyume na sheria kwa lengo la kujipatia fedha ya Sh90 milioni.
Baada ya kusomewa mashitaka hayo na kuyakana kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 13, 2021 ambapo watasomewa hoja za awali za kesi hiyo.
Chanzo: Mwananchi